This is Too Much For Me....!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Wakuu,
Niko kwenye hard time!

Nimeachiwa familia ya Mzee mmoja ambae ameenda zake kijijini kulima baada ya kustaafu, ili niwaangalie watoto wao, lakini wanaendelea kuishi kwenye nyumba yao!

Familia hii ina binti aliyemaliza form 4, lakini baada ya kuondoka wazazi wao ameanzisha tabia ya uchangudoa wa hatari. Kila nikirudi nyumbani napewa taarifa kwamba leo alijifungia ndani na fulani, kesho na mwingine...ni aibu!

Siku moja tukamwita na wife kumuuliza kwanini ameanzisha ushenzi huo, lakini anasema huwa wanaongea tu, hajawahi kufanya!, na ananunua viwalo vipya kama kazi wakati hana hela!

Kuwafahamisha wazazi wao tutaonekana tumeshindwa malezi, tufanyeje na huyu binti, wakati watu wanatishia kum'mimba, na lawama zote zitaangukia kwetu!
 
hapo hakuna ujanja, ni kuwajulisha wazazi wake kuliko hali izidi kuwa mbaya.....heri nusu shari kuliko shari kamili....ila wa kwetu huyo baba hana mke au ndugu zake wa kuwaachia hao watoto
 
hapo hakuna ujanja, ni kuwajulisha wazazi wake kuliko hali izidi kuwa mbaya.....heri nusu shari kuliko shari kamili....ila wa kwetu huyo baba hana mke au ndugu zake wa kuwaachia hao watoto
Yeye na mkewe ndo wamehamia huko shamba Singida!
Labda Mahusiano na Jiografia ya mahali tunapoishi ndo iliyomfanya atuachie sisi hiyo familia!..Nyumba tunazoishi zinatazamani, jirani sana!
 
Huyo mtoto sidhani kama kaanza hiyo tabia mara tu baada ya wazazi wake kuhama.
Alikuwa nayo siku nyingi
Ninachokushauri ni hivi: waarifu wazazi mapema iwezekanavyo kwa sababu hata usipowaambia sasa hivi lazima iko siku utalazimika kuwaambia. Ni bora sasa hivi ili pia uepuke lawama
 
Mrudishe kwao. Hasara za kubaki nae ni kubwa zaidi kuliko za kumuondoa. Kwanza una uhusiano gani na huyu mzee? Maana hauwezi kuachiwa tu watoto wake out of no where.
 
Anadai anajifungia ndani na mwanaume bila kuliwa? Lol, hiyo bado sijakubali. Mwambie tu acheze salama! Kama vipi mpeleke kwa baba yake shamba akalime! Au mvizieni na hao jamaa zake mwozesheni tu kabisaaa kieleweke!
 
Kaka mtihani huo! Kama kaweza kuthubutu kujifungia nao ndani home, akiwastahi sana, mechi zake atahamishia away, lakini si kuacha. Sijui, laaabda anaweza!! Ila inabidi umtafune jongoo, wapasulie wazee wake kuliko yaje kumfika kimya kimya yale yatokanayo na hako kamchezo. Mtaja ulizwa hamkuyajua haya? Mbona msituhabarishe? ....
 
Mkuu PJ,
Ukweli unauma sana lakini ni vizuri wazazi waju now before it is too late.
Watafute bwaga huu mzigo, angalu wawe na taarifa.

Pole mkuu, ahwa watoto wa .com ni balaa.
 
Usikate tamaa endelea kumpa ushauri huku ukiktajia majina ya wanawake kama yeye waliomua kutulia na ni watu wa maana mno duniani! Aelewe hakuna malaya aliewahi kuwa mtu wa maana duniani na wazaziwe pia uwaambie.
 
huna budi kuwajulisha wazazi wake!
maana kwanza wewe anakudanganya halafu inaonekana ana uhuru sana maana wkt mwingi nyie wakubwa mko makazini!
 
na atapata ukimwi na lawama zitakuangukia...
ataletaje mabwana nyumbani??????
mfukuze haraka........
 
Ukweli unauma sana lakini ni vizuri wazazi waju now before it is too late.
Watafute bwaga huu mzigo, angalu wawe na taarifa.

Pole mkuu, ahwa watoto wa .com ni balaa.
Aksanteni sana jameni kwa kunishauri hili...

Hakyanani, bora lawama kuliko fedheha, naenda kumwekea hazarani baba yao ajue kinachoendelea!!
 
Mkuu usitake bure kupata kombe la ushindi katika malezi, hii ni kazi ngumu ambayo inahitaji zaidi ya wewe na mkeo. Wajulishe wazazi wake na pengine ni wakati sasa wa ninyi kutambua kazi mlioachiwa ni kubwa na si lelemama ni ya ulezi
 
Pole kaka, ndo unauonja ukubwa huo. Fikiria kama angekua mwanao, ungempeleka kwa nani? Handle the issue head on. Ongea nae, muelimisheni wewe na mkeo jinsi gani mliweza kuivuka hiyo foolish age. Msisahau kumuelimisha pia ukimwi, na unplanned pregnancies etc. na impacts zake in the bright future ahead of her. Kama akiendelea, wazazi wanaweza kujulishwa. Mkiwa rafiki zake, mtaweza kumsaidia, and she will thank you one day.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom