This is Rostam I know... The Story Behind the Man

Asante Prince W na karibu sana JF. Umetukumbusha ukweli utashinda. Hivi huyu RA alikuwa na nyadhifa CCM hata enzi za baba wa taifa? Hivi kuna nchi nyingine kama bongo wawezaingia kihunihuni tu bungeni bila hata kumbukumbu zako binafsi kuwa wazi/kamili? Kwa vielelezo hewa au pungufu mtu kama RA kuwa mbunge ni usanii wa kutisha na aibu kwa kila anayejaribu kumtetea katika hili. Kwa mtaji huu si vigumu kukubali kuwa RA ni fisadi na mwisho wake umekaribia. Mnaomtetea kwa kutoelewa poleni na twawasamehe bure.
 
eh!? Wakuu wa mashirika ya umma wanateuliwa na nani na bodi zao zinateuliwa na nani? Mahesabu yao yanakaguliwa na nani na yakiingia matatani nani anawapa ruzuku? Unless unamaana nyingine unaposema "mashirika ya umma yako nje (ya) mfumo wa serikali kuu".

Halafu ukijenga hoja wewe jenga tu bila kurusha madongo, dharau au kwa namna fulani kuwafanya wengine wawe duni kwa sababu wana mtazamo tofauti.

Mzee Mwanakijiji unachanganya serikali na serikali kuu ( Central Government). Tunazungumzia Central government kiutawala. Kwa urahisi tu, wafanyakazi wa mashirika ya umma sio civil servants kama walivyo wafanyakazi wa serikali kuu. Civil servants maslahi na stahili zao zinashughulikiwa na idara ya utumishi. Kama walikuwa wanastahili kupewa nyumba, walikuwa wanazipata kutoka wizara ya ujenzi. Ninavyofahamu mimi hata mfumo wa accounting na auditing inatofautiana. Serikali kuu inakaguliwa na wizara ya fedha moja kwa moja wakati mashirika ya umma yako huru ku-appoint auditors wao. Hata wahasibu katika serikali kuu wanatoka wizara ya fedha na wanapangiwa kituo ha kufanyia kazi na wizara hiyo! Audit reports za hawa wote zinapelekwa kwa CAG.

Mnataka mifano? Baadhi ya nyumba zilizoko Oysterbay zilikuwa za shirika la National Development Corporation (NDC). Kwenye kona ya mtaa wa Toure na Karume kulikuwa na nyumba yao waliyoigeuza klabu ya waitaliano kama sikosei. Nadhani ilikumbwa na mgogoro na sijui hatma yake. Baadhi ya nyumba Masaki zilikuwa za ATC na mashirika mengine. Mali ya mashirika ya umma yaliyobinafsishwa yalipelekwa PSRC na wao ndio walioamua namna ya kuzi-dispose. Mali hizi zilijumuisha nyumba n.k. PSRC ilizipiga mnada na wenye nazo walizipata. Nyumba za serikali kuu ( Central Government) hazikuhusika kwenye hili.

Ni baadae baada ya zoezi la kuwauzia wafanyakazi wa serikali kuu nyumba ndipo utaratibu ulibadilishwa na nyumba za mashirika ya umma zikaanza kurudishwa serikali kuu. Hatua hii ilileta misuguano kwa sababu baadhi ya nyumba walikabidhiwa wafanyakazi wa serikali kuu na baadae kuuziwa. Kitendo hiki hakikuwafurahisha wafanyakazi wa mashirika ya umma.

With all due respect, Mzee Mwanakijiji, mbona hata wewe kuna wakati unajibu kwa lugha ya dharau? Sisi wote si malaika, na kuna wakati tunashindwa kujizuia. Lakini kama kuna mtu nimemuumiza feeling zake kutokana na namna nilivyomjibu, naombamsamaha. Siku nyingine, aniambie tu, kuwa Fundi Mchundo, haujanitendea haki nami nitajirekebisha!

Amandla......
 
Last edited:
Africa Business, February 1, 2006


Not in the cabinet, but perhaps the most powerful person after Kikwete is the president's long-term political associate Rostam Aziz, the Oxford-educated economics graduate, business tycoon and parliamentarian.


Aziz is a Tanzanian of Iranian extraction with family links in http://www.allbusiness.com/africa/1112936-1.html Iran and business links in the other Gulf countries. He has been described as the 'king maker', having played a pivotal role - over a 10-year period - in getting Kikwete nominated by the CCM as its presidential candidate. Content to play the role of the 'power-behind-the-throne', Aziz has not been keen to be in the cabinet as that would have prevented him from concentrating on his vast business interests.


A nickle for your thoughts:

.. mwaka 1980 Rostam alikuwa na miaka 11 (ukiamini tovuti ya Bunge). Alikuwa shule na kwa wazazi wake au mahali fulani katika utoto wake. Miaka 15 baadaye (1995) anaanza kuibuka Igunga (akiwa na 26 years). Baada ya hapo amekuwa katika biashara n.k na sikumbuki kama ni baada ya hapo alienda Oxford. So, kwa vyovyote atakuwa oxford kabla ya 1995 (angalau miaka 3) (tovuti ya Bunge inasema amehitibu Uchumi). Hiyo inaturudisha miaka 23. Kama ni kweli alikuja TZ akiwa na miaka 22 hiyo inatupeleka mwaka 1992.

Hivyo Chuo Kikuu itakuwa ni kabla ya hapo. Hivyo tukitoa miaka mitatu toka 1992, inaturudisha kwenye 1989. Hii inatupa umri wa RA kuanza Chuo Kikuu akiwa na miaka 20. Which is almost the age of graduating High School in Tanzania (kwa mtu aliyeanza shule ya msingi na miaka 7 atamaliza akiwa na miaka 21 so kwa vyovyote kama mahesabu yangu yanakwenda sawasawa atakuwa ameanza shule kama na miaka 6 hivi.

Kama amemaliza kidato cha sita 1989, tunakabiliwa na swali jingine kabisa.. alienda jeshini wapi? Au ndipo hapo aliporuka na kwenda Chuo Kikuu cha Oxford?

Najua mahesabu yangu yatakuwa na + or - few years ..
 
Last edited by a moderator:
Usitake kumharibia unaejifanya unamtetea kwa kukumbushia hii habari. Kamuulize kwanza kama angependa hii ishu irudi kwenye public domain!
.

- Mkuu leo asubuhi kuna mahali umeshambuliwa kwamba unatumwa, ukadai hutumwi na ukanitaja kama shahidi wako na kweli nikaweka ushuhdua wangu kwamba hutumwi ni mawazo yako tu kumtetea fisadi papa Rostam,

- Sasa tizama hapa na wewe unarudia yale yale ya kumtuhumu Prince kwamba anayejaribu kumsafisha na akaamuulize, una maana gani? Kwamba aakamuulize aliyemtuma? Kumbe na wewe umetumwa?

Again acha personal, kata ishu mkuu kama imekushidna waachie wengine ila tu kwa taarifa yako sio rahisi kumsafisha fisadi papa, ndio maana hata wenziwe wengi wa Mtandao wameshamtema tayar, jaribu kukata ishu bila personalization!

Respect.

FMES!
 
Prince William, Karibu sana JF. Mchango wako ni muhimu kwenye ukombozi wa wanyonge.

Huyu jamaa Rostam Aziz, kweli alisoma wapi? Manake isije ikawa tuna misukule kila mahali mpaka bungeni!
Ni kweli! nani kasoma na Rostam A, popote palee? na kama Mzee Mwanakijiji anavyosema alikuwa wapi before 1980, nani kawahi kumuona? maana kuna watu wanasema alikuwa wa kwanza darasa la saba! wapi? na shule gani? Kweli jamaa hana marafiki wa utotoni? Kama alipewa uraia ni lini? na wapi?
 
Sisi wote si malaika, na kuna wakati tunashindwa kujizuia. Lakini kama kuna mtu nimemuumiza feeling zake kutokana na namna nilivyomjibu, naombamsamaha. Siku nyingine, aniambie tu, kuwa Fundi Mchundo, haujanitendea haki nami nitajirekebisha!

Amandla......

- Hukumtendea haki Mkulu sana Prince, tunashukuru sana kwamba umeliona hilo na kuomba radhi, ndio uungwana tunaoutaka hapa JF, ndio maana niliwahi kusema huko nyuma kwamba wewe ni the man of class.

Heshima mbele sana.

FMES!
 
I am ending here but very soon I will reveal all things about Rostam.


There is no one dragging for tribalism sentiment s here, but based on the political calculations this is the fact on what has happened in the past and what is continuing to happen.

Tunahitaji tuseme ukweli wa mambo ambayo yanatugawanya katika vita hii ya aufisadi, Kukuhakikishia this is a big polical weapon that dragging us to hell ninajua hutaki kuamini but this is the truth.

Why did Mkapa ordered the money to be given to Rostam? The Main answer is that he was strategically well positioned in Lake Zone right? Why Rostam?

Secondly, You said Mpaka called Ballali to ask him to Give RA money to elect Kikwete, that means the Operations to steal money from BOT was planned and initiated by CCM Chairman for the Benefit of CCM? Which means RA was just an implementer

Third MENGI and RA they are in same shoes they are both Mafisadis , Mengi through ITV he was a benefitery of EPA money, not only that Mengi kwa kupitia ITV he missleaded all Tanzania on how Good CCM was in returns he has access to all guarantees and loans na ndio maana MENGI anamwita RA fisadi na sio CCM because he still love CCM and what it does to him personally .

Mwisho ninacho wapinga mwanakijiji na wengine kama wewe kwenye Hii forums ni kule kusema kwamba RA ndie FISADI peke yake na mnaitoa CCM kwenye Discussion .

Maelezo yako yanijitosheleza kwamba Mkapa kwa niaba ya CCM alimwambia Balali Atoe pesa BOT,ampe RA . Which Proves to me that CCM ndio walioiba pesa za EPA, kwahiyo tunapo mpa nguvu mtu mmoja na tunasahau mmliki na mwanzailishi wa huu wizi wa epa, tunakuwa hatujawa Objective
 
In conducting all bank transactions, Rostam used his personal secretary Tabu Abdulah as a cover-up. There's all evidence.

I am ending here but very soon I will reveal all things about Rostam.
Na juzi huyu tapeli akawa na guts kusema hadharani kuwa he has never met nor does he know that man. (Meaning Ballali) The man is a liar na wanaomtetea wanapaswa kuchunguzwa akili zao.
 
- Mkuu leo asubuhi kuna mahali umeshambuliwa kwamba unatumwa, ukadai hutumwi na ukanitaja kama shahidi wako na kweli nikaweka ushuhdua wangu kwamba hutumwi ni mawazo yako tu kumtetea fisadi papa Rostam,

- Sasa tizama hapa na wewe unarudia yale yale ya kumtuhumu Prince kwamba anayejaribu kumsafisha na akaamuulize, una maana gani? Kwamba aakamuulize aliyemtuma? Kumbe na wewe umetumwa?

Again acha personal, kata ishu mkuu kama imekushidna waachie wengine ila tu kwa taarifa yako sio rahisi kumsafisha fisadi papa, ndio maana hata wenziwe wengi wa Mtandao wameshamtema tayar, jaribu kukata ishu bila personalization!

Respect.

FMES!

Usitake kugeuza kila kitu personal! Sijamtukana Prince bali nimempa ushauri wa bure kuwa haitakuwa vyema kuanza kurudisha tena ishu ya aliyekuwa waziri wa ujenzi na zoezi la kuwauzia nyumba wafanyakazi wa serikali. Nimesema akamuulize kwa sababu siamini kuwa ana hata habari na kinachoendelea humu! Sasa kutumwa kumetoka wapi?

Ushauri wangu ni kuwa ni lazima tuwe makini tunapojaribu kuwatetea watu humu. Wakati mwingine badala ya kuwatetea tunawabomolea. Huyu waziri hakuwemo katika hii ishu sasa anamwingiza wa nini?

Amandla......
 
Africa Business, February 1, 2006


Not in the cabinet, but perhaps the most powerful person after Kikwete is the president's long-term political associate Rostam Aziz, the Oxford-educated economics graduate, business tycoon and parliamentarian.


.

- Really? Rostam amesoma Oxford? Ipi hiyo na mwaka gani kwa wenye info zaidi tuhabarisheni, yaani unaona sasa ndio maana nilisema ameharibu sana kujitokeza Kempiski! Duh! vihiyo bwana, wakuu hebu wekeni dataz hapa tukawape wabunge wakamlipue bungeni ngoja kwanza nimshitue mbunge mmoja sasa hivi kumbe mkulu hakusoma shule!

FMES!
 
Fundi Mchundo,

Stori ya maelezo ya Ballali nina uhakika ina ukweli kwa over 90%, unganisha dots taratibu huku ukirejea maelezo ya wakili Sanze. Stori ya maelezo ya Sanze nadhani imeandikwa kwenye gazeti la MwanaHalisi kama sikosei.

Jiulize kwanini Maregesi Law Chambers mpaka leo hii hajaingia kuzimbani? Nina uhakika kuna kampuni nyingine kibao ambazo hazijaburuzwa mahakamani kwa kuwa wahusika wana inside information ya "deals" za EPA na iwapo wataguswa basi mambo mengi yatakuwa hadharani na hata serikali iliyo madarakani inaweza kujikuta inadondoka kwa kuwa chain ni ndefu na kubwa.

Kwa kuwa Ballali alishakufa, swali lako la yupi Fisadi kati ya Rostam na Ballali, mimi naona halina nafasi kwa sasa. Kama Ballali angekuwa bado yuko hai jibu langu kwa jumla lingekuwa ni moja kwamba Ballali na Rostam wote ni mafisadi na hayo yalikuwa yakisemwa hata kabla Ballali hajafa. Halafu kwenye hiyo orodha nitaongeza jina la Mkapa maana ndiye aliyemwagiza Gavana akatoe hela.

Maswali ya ziada, je ni kwanini Ballali aliacha hayo maandishi kama ushahidi? Hapo kuna mengi sana, nadhani inauma sana unapoona kwamba unaandamwa kwa kitu ambacho ulilazimishwa kukifanya kwa maslahi ya watu wengine na hatimaye unakuja kubebeshwa mzigo.

Kabla Ballali hajafa kwanini akina Mwanyika, Hoseah na Mwema hawakumfuata hospitali kumhoji kuhusu hela za EPA? Walikuwa wanaogopa nini na wakati Ballali ndiyo alikuwa shahidi namba moja wa kuwapatia details zote? Kuna mengi sana behind the scene ambayo hatuyajui na mizigo yote alitwishwa Ballali baada ya kuona afya yake imedhoofu na hatimaye tukaambiwa kwamba amefariki.
 

With all due respect, Mzee Mwanakijiji, mbona hata wewe kuna wakati unajibu kwa lugha ya dharau? Sisi wote si malaika, na kuna wakati tunashindwa kujizuia. Lakini kama kuna mtu nimemuumiza feeling zake kutokana na namna nilivyomjibu, naombamsamaha. Siku nyingine, aniambie tu, kuwa Fundi Mchundo, haujanitendea haki nami nitajirekebisha!

Amandla......

mzee utaona nawajibu vile wale wanaoanza kunishambulia...lakini pia (niliwahi kusema huko nyuma) kwenye lugha inaruhusiwa sarcasm, rhetorics n.k So, si kila wakati ni vibaya kutumia lugha ya kejeli pale inapotumiwa vizuri huongeza utamu wa hoja. Lengo ni kuonesha uduni wa hoja siyo uduni wa mtu.

ndiyo maana utaona siulizi motives za mtu anaponijibu kama wametumwa au wanalipwa.. nachukulia hoja zao tu. Simtukani mtu anayeshindana nami hata wale ambao wanatumia vibaya vitu hivyo isipokuwa pale ninapoamua tu kuwa fyatu for a second! (which does happen sometimes if i don't take my medication)..
 
- Zoezi la kuuza nyumba za serikali halikwua na tatizo, isipokuwa tatizo lililetwa kwanza na yeye mwenyewe Magufuli alipoanza kuuzia nyumba hizo ndugu zake na marafiki zake na mwisho kuuzia wasiohusika, otherwise it was a good thing,

- Mtandao never wanted Magufufli kwenye Cabinet yao, lakini ni umaarufu wa Magufuli kisiasa ndio ulioawalazimisha kumpa uwaziri, lakini toka siku ya kwanza walikuwa mbioni kumtafutia sababu za kumuondoa, infact nilisema mara ya kwanza baada ya cabinet kutangazwa, kwamba Mramba na Magufuli watatemwa mapema sana kwa Prince hayuko mbali sana na ukweli, ingawa tu masahihisho kwenye habari yake yanaweza kua ni neno Transparent na nyumba, hapana hakukuwa na transaprency kwenye lile zoezi, otherwise Prince is right 100% na the rest of the story!

Respect.

FMES!

Ndiyo huu ushauri wa bure niliokuwa nikiuzungumzia! Sasa mmeanza kumjadili Magufuli!

Amandla....
 
There is no one dragging for tribalism sentiment s here, but based on the political calculations this is the fact on what has happened in the past and what is continuing to happen.
Tunahitaji tuseme ukweli wa mambo ambayo yanatugawanya katika vita hii ya aufisadi, Kukuhakikishia this is a big polical weapon that dragging us to hell ninajua hutaki kuamini but this is the truth.

- This is the fact on what happened in the past and is what continuing to happen!

Mkuu umeniacha nje hapo, what is the fact as far as you are concerned ya mtu kama mimi ku-support hoja za Mengi dhidi ya Rostam? Unasema ni wka sababu ya ukabila au rangi?

With all due respect, naomba ufafanuzi hapo mkuu kama unaweza!

FMES!
 
I hope mawakili wa Mzee Mengi wanasoma hapa, na kama hiyo kesi ipo mwambieni jamaa aonyeshe alizaliwa wapi, kusoma wapi na raia wa wapi, najua wanasheria wanaweza kuingiza hizi issue kinamna zao. Chukueni nondo hapa. Mnaowajua please waambie wasome na muwape kabisaa.
 
the Oxford-educated economics graduate, business tycoon and parliamentarian

Nina uhakika mtu akitafuta data base ya oxford University atajua ukweli, hopefuly they have good records of their graduates

Kwi kwi..
Bravo mzee Mengi uliye mtoa nyoka Pangoni, bubu akasema, sasa kila kitu kimesanuka !
 
Unajua... si kwamba hajasoma Oxford.. nadhani atakuwa amesoma huko lakini point yangu ni kuwa hakuwa anatokea Tanzania... on the other hand, kama hakusoma Oxford ali graduate wapi? Tovuti ya Bunge inasema yeye ni graduate wa Economics labda Mlimani ...
 
Mwanakijiji,
Mkuu wangu nadhani kuhusiana na Elimu ya Rostam na shule zipi kasoma sio issue hapa zaidi ya kutafuta ukweli unaohusiana na Rostam fisadi..

Binafsi nimesoma na Wahindi, wairan na Waarabu kibao, leo hii wengine wako Oman, UAE, US canada na UK na hawa watu wamezaliwa Tanzania huko Kibara sehemu ambazo huwezi kuamini na nina hakika kabisa nikiweka majina yao hapa wengi mtatoka kapa..

Nakumbuka udogo wangu nakua pale kibara kulikuwa na mzungu mmoja akiitwa John Walker (Welder) sijui kama hilo lilikuwa jina lake au la laa! lakini mkuu wangu mzungu yule amekulia pale na kafa kama Mtanzania.. amezikwa hapo Kibara na hakuna mtu hata mmoja aliyejali Uzungu au uraia wake kwa sababu ya rangi yake..

Mimi naona tunatoka ktk issue yenyewe na sababu hasa mnayowekea mashaka uraia wake ni kutokana na rangi yake.. nothing else.. wapo weusi kibao ambao sii wazawa na wanatuongoza.. Uhuru wetu wenyewe ulipatikana tokana na watu wengi wa kuja.. kina Kreist asili yao ni South Afrika lakini leo huwezi kuhoji Uhalali wa uraia wa wajukuu zake..

Binafsi naamini kabisa kutokana na lafidhi yake huyu Rostam bila shaka amezaliwa kama sio amekulia Tanzania, hivyo anaweza soma shule yoyote ile isipokuwa labda tunahoji nafasi yake ktk uongozi kulingana na Elimu yake. Maadam tumeambiwa kasoma Oxford basi na tuamini hivyo hadi pale itakapo kuja issue inayohusiana na elimu hiyo na sii Ufisadi..
 
Back
Top Bottom