Hukumuzuku
JF-Expert Member
- Aug 29, 2008
- 6,676
- 5,027
Mkuu! Hata wapenda kunyonga wamarekani wamekubali kuwa mtu aliye chini ya miaka 16 hastahili kunyongwa hata akifanya nini! Huyu ni mtoto bado na si ajabu kwa akili zake alikuwa anaona ndiyo anaonyesha mapenzi kwa huyo jamaa. Nadhani kubaka nayo ni felony. Miaka 30 si mchezo katika jela zetu. Kwa upande ni sawa na hukumu ya kifo.
Habari inasema kwamba mlalamikaji anao umri wa miaka 16 (na siyo chini ya miaka 16 kama unavyodai). Huyo si mtoto tena kisheria kwenye majimbo yaliyo mengi zaidi (majority of states) kule Marekani, na penginepo hata Tanzania. Isitoshe, felonies zinatofautiana. Kubaka kamwe haiwezi kusababisha mtuhumiwa akapewa adhabu ya kifo, na adhabu ya kifo si sawa na kifungo cha miaka 30. Kama huyu msichana angefanikiwa kuwaua wenzake wawili kwa sumu aliyopewa na mwenyewe akapona, nadhani hata huko Marekani kwa vyovyote wangemnyonga tu, mitigating circumstances notwithstanding.