This is Dowans HQ in Costa Rica - (Pictures)

jmk kumbuka wakati wa mgao ULIAPA KUWA TATIZO HILI LA MGAO HALITATOKEA TENA. USHAURI WA ORCHE HAUNA MJADALA
 
Tk umeingizwa kwenye mtego wa mafisadi! Dowans siyo solution ya matatizo ya kukosekana kwa umeme bali kukosekana kwa umeme ni mradi wa wakubwa. Upungufu wa umeme ulijulikana zaidi ya mwaka sasa, lakini wakubwa wakasubiri tu ili Dowans or IPTL itumike!
Kwanza kumbuka Dowans walipofikisha mitambo yao connection ilishindikana kwa muda gani, sasa leo wanatudanganya kuwa ni dakika tano unawaelewa?
Five min. is part of ufisadi but not reality kwa sababu mgao huu ulitengenezwa kurahisisha mazingira ya kurudishwa Dowans kama si kelele za watanganyika!
Good one Orche!! but watanzania tukumbuke kitu kimoja" To Vote for the man who promises least; he'll be the least disappointing" this guy jk
Deep down he is shallow.
 
Tatizo la watz wengi ni wivu wa kijinga uliowajaa ndio maana hata kuokoa Taifa mnashindwa!
 
tatizo ni si mitambo tatizo ni 'kuchanganya mambo binafsi (au siasa) na utaifa!la IPTL na owans ni yaleyale hakuna alie bora why kama utaifa upo mbele mtambo uliopo tayari uwashwe? ni tamko tu la JK basi,unainusuru nchi huku mpambano ukiendelea, hela ya kufufua IPTL tungenunua mitambo ya Dowans, la hasha itaifishwe, kitafutwe kipengele cha wao kukiuka tender kinasimamiwa mitambo inakuwa ya nchi
 
Hatuhitaji kununua mitambo ya Dowans kumaliza tatizo la umeme

TATIZO la ukosekanaji wa umeme wa uhakika wa kuendesha “gurudumu la maendeleo” na uchumi wa nchi yetu, ambalo lilianza kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1994, hivi sasa limekuwa la kudumu pasi na taasisi yoyote ile – ama ya kiserikali au ya kibinafsi – kupata ufumbuzi wa kudumu. Kimsingi, tatizo hili ni la kisera zaidi kuliko kiutendaji, kwani, bila sera thabiti, ufumbuzi hautapatikana.

Ni jambo la kushangaza na kusikitisha, licha ya jitihada nyingi za asasi za kiraia zinazofanya utafiti na kuvumbua mbinu nyingi endelevu za nyenzo bora na za gharama nafuu za nishati, Serikali na vyombo vyake imeshindwa kutumia matokeo ya tafiti hizo. Mshangao zaidi unatokana na ukweli kwamba Serikali imepuuzia jitihada hizo, kana kwamba hazina manufaa yoyote yale kwa Taifa kwa ujumla. Kwa mfano, hivi majuzi, asasi inayoitwa Appropriate Rural Technology (ART) ilizindua kinu kidogo cga kuzalishia umeme kinachotumia gesi ya kibaologia (biogas), ikiwa ni uvumbuzi uliofanyika baada ya kufanya marekebisho katika mfumo wa kuchoma mafuta wa injini ya kinu cha kawaida kinachotumia mafuta ya petrol. Ubunifu huo umewezesha kinu hicho, ambacho kinapatikana kwenye maduka yanayouza vinu hivyo, kuweza kutumia gesi hiyo ya kibaolojia ambayo inazalishwa kwa gharama nafuu, na baada ya kuzalishwa inapatikana bila ya gharama yoyote nyingine ya nyongeza. Kinu hicho kinazalisha umeme katika kiwango cha KVA 650 hadi 800, kutokana na mahitaji ya mtumiaji.

Shamba la mkonge mkoani Tanga nalo limezindua kinu cha kuzalisha umeme kinachotumia gesi hiyo ya kibaolojia inayotokana na mabaki ya zao la mkonge, katika kiwango cha Mega Watt 1, jambo ambalo linatoa matumaini kwamba jitihada zaidi zinaweza kufanyika ili kuiwezesha Tanzania kuwa na vyanzo vingi mbadala vya umeme.

Lakini kinachoshangaza zaidi ni kwamba licha ya kwamba TANESCO ilitambua wazi kuwapo kwa tatizo la upatikanaji wa umeme wa uhakika, hakuna mbinu zozote mbadala zilizowekwa bayana. Kinachoonekana wazi wazi ni kwamba, hakuna ubunifu wowote au mawazo yoyote mbadala yaliyojadiliwa kwenye himaya ya uongozi mzima wa TANESCO, badala yake, TANESCO na watendaji wake wamekuwa wakitegemea vyanzo vya kawaida vya uzalishaji wa umeme, kama vile generator (turbines) za Dowans, Songas, IPTL na vinu vya mabwawa ya maji ya Kidatu, Kihansi na Mtera!

Tumekuwa tukipata taarifa mbali mbali kwenye vyombo vya habari vya kidunia, kama vile CNN, kupitia vipindi vyake – kama vile Eco Solutions – kwamba vyanzo vya nishati ya mafuta ya petrol vinaelekea kukauka, jambo ambalo linasababisha gharama ya mafuta kwenye masoko duniani kuongezeka mwaka hadi mwaka. Taarifa hizi, angalau, zingetuzindua kutoka kwenye usingizi mkubwa tulionao, na tukaanza kuendeleza jitihada za tafiti zilizofanyika, pia pamoja na kuanza kutumia vyanzo mbadala vya upatikanaji wa upepo, jua, na kadhalika.

Kupungua kwa upatikanaji wa mafuta yatokanayo na petroli ni jambo ambalo lilitabiriwa miaka mingi iliyopita, kwani, mafuta hayo yanayochimbwa kutoka ardhini hupatikana kwa viwango tofauti na hatimaye kila kisima kinachochimbwa hufikia wakati kikakauka kabisa. Jambo hili lingetuzindua kutoka kwenye usingizi tulionao, kama walivyofanya wenzetu wa Marekani, ambao tayari wamekamilisha tafiti mbali mbali na kuweza kubuni teknolojia madhubuti za uzalishaji wa umeme kutokana na nishati itokanayo na joto la jua, kwa jina lingine, Stirling Energy Systems, utafiti uliodhaminiwa na Wizara ya Nishati ya Marekani na kuendeshwa na Chuo Kikuu cha California, cha mjini Berkeley, jimboni California.

Marekani kwa sasa ni nchi inayoongoza katika teknolojia hii ya Stirling, na kwenye kada mbali mbali, ikizingatiwa kwamba nchi nyingi barani Afrika zinapata jua kwa muda mrefu zaidi – kwa kuwa wakati wa msimu wa baridi kwenye nchi za Ulaya/Marekani, muda wa jua kuwaka unapunga – teknolojia hiyo imeonekana kuwa hatari kwa nchi zinazozalisha mafuta ya petroli, kwani, ikipatikana kabla ya muda muafaka (ambapo itapatikana kwa bei ya juu zaidi kuliko sasa), nchi nyingi barani Afrika zitaacha kabisa kutumia mafuta ya petroli kwa kuzalishia umeme, na zitakuwa zinajitegemea katika uzalishaji wa umeme, kutokana na urahisi na ubora wa teknolojia hii ya Stirling.

Wadau wengi wa nishati nchini Tanzania wanaona kwamba kuanza kuzungumzia teknolojia ya Stirling ni sawa na ndoto za Alinacha, kwani, kama kawaida ya Watanzania wengi, wanaonesha udhaifu wa kifikra kwa kusema kwamba “… hayo ni mambo ya wakubwa… walioendelea”. Lakini cha ajabu ni kwamba, hata siku moja hawajiulizi ni nani aliyewateua hao “wakubwa” kuwa na ukiritimba wa fikra na telnolojia, na kutuacha sisi “wadogo” kuwa mafukara wa teknolojia na fikra?

Hata kama hatutaanza kuzungumzia teknolojia ya Stirling, basi, tuanze kuweka mikakati ya matumizi ya nishati ya upepo – unaopatikana kwa wingi sana hapa nchini – kwa madhumuni ya kuzalisha umeme. Hata kama tutaanzia kwenye mitambo midogo midogo, yenye uwezo wa kuzalisha Kilo Watt 1 hadi 10, mitambo hiyo ikiwa mingi itaondoa kabisa tatizo hilo la upatikanaji wa umeme. Si lazima Tanzania yote iwe kwenye umeme wa gridi, kwani hapo ndipo tunapokosea, kwa kudhani kwamba ni lazima umeme unaopatikana nchini uzalishwe na TANESCO peke yake.

Wakala wa Umeme Vijijini (REA) tayari wameweka mazingira mazuri ya Watanzania kuwekeza kwenye sekta ya umeme, kuanzia kwenye viunga vya miji mikubwa hadi vijijini. Lakini fursa hizi hazijatumiwa ipasavyo kwa kuwa Watanzania walio wengi wanaona kwamba wao hawana nguvu ya kujishughulisha na uzalishaji wa umeme, badala yaka fursa hizo zinatumiwa na watu wachache – hususan wageni – ambao wanajiamini kwamba wanaweza.

REA ina nafasi kubwa ya kuwaelimisha wananchi kuhusu wajibu wao na haki zao katika uzalishaji wa nishati ya umeme, jambo ambalo watalifanya katika siku za usoni. Lakini Watanzania “wakiamka”, umeme utapatikana.
Hatuhitaji kununua mitambo ya Dowans kumaliza tatizo la umeme. Ufumbuzi wa tatizo hili uko mikononi mwetu.

Kwa maoni, maswali, mapendekezo:
Tuma email kwa info@strategos.co.tz

P.S. Nilikuwa mmoja wa wajumbe walioshiriki kwenye kongamano la Siku ya Viwanda ya Afrika, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee, takriban wiki mbili zilizopita. Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Bashir Mrindoko, alizungumzia nafazi za uwekezaji zilizopangwa (kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Nishati) ambazo ziko kwenye hatua mbali mbali za utekelezaji. Ni nafasi moja tu ya uwekezaji kwenye nishati mbadala, ambayo imewekwa, nayo ni ya uzalishaji wa MegaWatt 100, kwa kutumia teknolojia ya umeme unaotokana na nguvu za upepo (Wind Power). Je, Serikali inatambua upepo peke yake kama teknolojia kuu ya nishati mbadala, au kuna nyinginezo? Jambo lingine ni kwamba, kwa Sasa, kwa mujibu wa Mrindoko, Serikali yetu inaona kwamba Watanzania hawana uwezo (au hawataki?) wa kuwekeza kwenye sekta hii nyeti ya nishati! Je, hii ni kweli? Kama si kweli, kwa nini Serikali haiwapigii kelele wawekezaji wazawa kujikita kwenye uwekezaji wa uzalishaji wa umeme, kuanzia MegaWatt 100 na kuendelea? Penye nia PANA NJIA!
 
Dowans conspiracy back in full swing

By ThisDay Reporter
13th January 2010



A SECRET plot is allegedly underway to revive the controversial plan to purchase second-hand 100-megawatts power turbines from Dowans Tanzania Limited by creating an artificial power shortage in the country, it has been revealed. According to latest THISDAY findings, the plot hatched by prominent local business tycoons is allegedly being implemented by a far-reaching network including senior government officials, politicians from both the ruling and opposition parties, and local journalists.

It is understood that architects of the dubious move have not given up on their original plan to dupe the government into buying the rusty turbines at inflated cost, contrary to the Public Procurement Act of 2004. “The Dowans conspiracy is still in motion...

These people simply won’t rest until the government does buy the turbines,” a senior official in the Ministry of Energy and Minerals told THISDAY in an interview. “If Bunge hadn’t intervened, the government would have bought those turbines at a price that is more than twice what the equipment actually cost,” the official added.

The initial move to buy the Dowans turbines, famously backed by Energy and Minerals Minister William Ngeleja and the ex-managing director of the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO), Dr Idris Rashidi, was blocked by parliament in 2008. However, several energy sector experts have confirmed to THISDAY that far from being shelved once and for all, the plan has been kept alive by some senior officials in both TANESCO and the ministry, with several leading local businessmen secretly bank-rolling it.

“Apart from the ministry and TANESCO officials, there are also members of parliament from both CCM and the opposition camp involved. Not only that...several journalists are also in on the conspiracy,” a reliable source in the energy sector asserted. While the dubious Richmond Development Company/Dowans Tanzania Limited collaboration is understood to have spent around $30m (approx. 40bn/-) to install the power turbines at Ubungo in Dar es Salaam, the government was seeking to buy the thermal electricity generators for a whopping $69m (approx. 92bn/-).

The government itself will still neither publicly confirm nor deny if it has abandoned the plan to buy those turbines. When confronted with the question by THISDAY last week, minister Ngeleja said: “I have no comment - please don’t drag me into a matter that has already been closed”. As part of the plot, members of the Dowans conspiracy network are alleged to be systematically sabotaging rival projects that could boost electricity inflows into the national power grid, and thus effectively pushing the Dowans turbines to the top of the options list.

“The IPTL (Independent Power Tanzania Limited) gas conversion project is one of those being targeted by the pro-Dowans network. They don’t want to see IPTL producing cheap electricity from natural gas simply because that won’t bode well for their own plan,” the energy sector source said. Meanwhile, latest investigations by THISDAY show that Dowans Holdings S.A, which is the parent company of Dowans Tanzania Ltd, has a murky background that bares striking similarities with the dubious Richmond Development Company.

Richmond entered into a power purchase agreement with TANESCO in 2006, but then later re-assigned the contract under dubious circumstances to Dowans. It now turns out that Dowans Holdings S.A, which claimed to be registered in Costa Rica, has no records in that country.

According to official documents at the Business Registration and Licensing Authority (BRELA) in Dar es Salaam, the proprietor of Dowans Tanzania Ltd is listed as one Brig. Gen. Suleiman Al-Adawi of the United Arab Emirates (UAE). There are also increasing hints that at least one member of the royal family in the UAE is also strongly linked to the mysterious Dowans company.
 
THISDAY naye akae chonjo atafungiwa sasa hivi! Uchokonozi wa mambo ya Serikali katika kipindi hiki 'kigumu' hayatakiwi.
 
Haya yanatokea Tanzania tu. Why should we deal with Dowans anymore? Kwa sababu JK yumo ndani na RA.

Kwa nini bado tunasikia IPTL? Kwa sababu ufisadi wa Dowans unahitajika kusafishwa na kuonyesha uozo mungine.
 
Dowans alipanda na haondoki mpaka amevuna na kwa kuwa kipindi cha mavuno kinakaribia, lazima aongezewe awamu nyingine aweze kuzicheza zile ngoma za mavuno.
 
Serikali yaitaka Dowans yasema mitambo yake ya umeme ni gharama nafuu

Imeandikwa na Stella Nyemenohi; Tarehe: 21st January 2010


WIZARA ya Fedha na Uchumi, imeipigia chapuo mitambo ya gesi ya kufua umeme inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans ikisema nchi itaendelea kupata hasara ya Sh bilioni 5.4 kwa mwezi kama Serikali haitaitumia.

Taarifa ya Wizara hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi, imechambua gharama zitokanazo na mikakati ya dharura huku ikionesha kwamba gharama za mitambo ya IPTL inayotumika sasa, iko juu ikilinganishwa na ya Dowans.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa juzi Dar es Salaam, jumla ya gharama za Dowans kwa mwezi ni takribani Sh bilioni 6.4 ikijumlishwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati IPTL gharama yake kwa mwezi ni Sh bilioni 20.

“Iwapo Serikali itatoa tamko la kutumia mitambo ya Dowans … ina uwezo wa kuzalisha megawati 105 na kupunguza kwa kiasi kikubwa si tu pengo la uzalishaji katika Gridi ya Taifa, bali pia hasara inayoweza kujitokeza katika uchumi,” sehemu ya taarifa kwa wabunge ilisema.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Abdallah Kigoda, ilielezwa kwamba kwa upande wa Dowans, gharama za gesi kwa mwezi ni Sh 10,665,010.98 na matumizi kwa gharama ya vipuri na vilainishi vya mitambo ni Sh 4,203,576,000 .

Kulingana na taarifa hiyo, kama mitambo hiyo itatumika kwa kiwango cha chini ya asilimia 100, Serikali italipa uniti za umeme zitakazozalishwa pamoja na tofauti ya capacity charge.

Kuhusu IPTL, taarifa hiyo inaonesha kwamba kwa mwezi mtambo unatumia mafuta tani za ujazo 14,125 ambayo yanagharimu Sh 13,552,531,200; matumizi kwa gharama za vipuri na vilainishi vya mitambo ni Sh 966,126,200 na mishahara ni Sh bilioni 2.

Hata hivyo, kuhusu IPTL ambayo mitambo yake ndiyo inatumika sasa, Kamati ya Bunge iliambiwa, kwamba licha ya gharama zake kuwa kubwa, hasara inayoweza kupatikana kwa kutoitumia ni kubwa karibu mara sita ya gharama ya Sh bilioni 20 kwa mwezi.

“Mitambo ya IPTL ikiwa inafanya kazi ina uwezo wa kuzalisha megawati 64,800 kwa mwezi. Hivyo kwa kutozalisha na kusambaza, kilowati 64,800,000 za umeme wa IPTL, nchi ingekuwa inapata hasara ya dola 71,280 za Marekani sawa na Sh 92,664,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa.

Pamoja na kwamba mtambo wa IPTL umeshatolewa uamuzi na Serikali kutumika, makubaliano yaliyofikiwa ni ya dharura kwa miezi sita kuanzia Novemba mwaka jana hadi Aprili mwaka huu.

Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba wa Richmond baada ya kushindwa kuzalisha umeme wa dharura katika muda wa makubaliano. Hata hivyo, Dowans pia ilisitishwa baada ya kubainika kuwa mkataba wa mwanzo haukuwa halali.

Umekuwepo mjadala juu ya hatma ya mitambo ya kampuni hiyo, huku baadhi wakitaka itaifishwe wengine wakitaka Serikali iinunue. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe ni miongoni mwa watu walioshauri Serikali inunue mitambo hiyo.

Wakati huohuo, Kamati hiyo ilielezwa kwamba bajeti za baadhi ya sekta ziko katika hatihati ya kupunguzwa au miradi ya maendeleo kusitishwa ili kufidia gharama zinazotumika katika mitambo ya dharura.

Wizara ya Fedha na Uchumi ilisema, “gharama zote za kutumia mitambo ya IPTL na Dowans na ya dharura ya kukodi ni mpya na hazikuwa kwenye bajeti ya awali ya Serikali ya mwaka 2009/10.

“Hivyo kuna uwezekano wa bajeti za baadhi ya sekta kulazimika kupunguzwa au kusitisha miradi ya maendeleo iliyokuwa imepangwa katika sekta hizo, ili kufidia gharama hizi. Italazimika kufanya hivyo ili kunusuru uchumi usiendelee kudorora,” wabunge waliambiwa.

 
Naona hili bomu halitakufa. Waheshimiwa mpaka wanahakikisha senti zao zinarudi na faida juu yake>
 
Naona hili bomu halitakufa. Waheshimiwa mpaka wanahakikisha senti zao zinarudi na faida juu yake>

Mkuu Jasusi, inaelekea mahesabu ya CCM kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao bado yanagomba hivyo lazima walipue bomu kubwa kama hilo la Dowans ili mahesabu yakae sawa na wao wawe na helicopters zao za kumrusha msanii toka mkoa hadi mkoa ili kufanya kampeni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom