this is a biasness way of reporting(BBC)

anatropia

Member
Sep 27, 2007
23
5
Nilitakaa kushangaa kama BBC swahili wasingerusha habari za chadema na machafuko Morogoro,kama walinisikia wakarusha,habari yenyewe too bias, eti polisi wasingeruhusu maandamano wakafunga barabara inayotumiwa na wagonjwa na wasiokuwa mashabiki wa chadema,swali je?chadema hawakuwa na haki nahiyo barabara?na suppose wangewaruhusu yaliyotokea yangetokea?

Patamu zaidi,polisi wanasema hawajatumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji,na Je kamanda Ally alipigwa na nini kichwani?na wanajinasibu polisi haohao wameunda tume kuchunguza kilichompata.wito polisi elevukeni zama zimebadilika watanzania hatudanganyiki tena.:A S cry:
 
Ni vituko vonavoendelea tanzania., sjui nani atwokoe make kila mtu mwoga kwemda kwenye ukombozi
 
Hata mimi nimeisikia hiyo habari ina mapungufu mengi sana, tatizo ni reporter wao lakini pia Msimamizi wa Matangazo kuruhusu habarI yenye mapungufu makubwa kama haya kuruka hewani, hatujasikia upande wa pili(Chadema), Upande wa tatu(Raia) kwa mfano
1/Chanzo cha habari ni Kamanda wa Polisi
2/Uthibitisho wa tukio ni Kamanda wa polisi
3/Mshitakiwa ni jeshi la polisi
4/Shuhuda ni jeshi la polisi
5/Mchambuzi ni reporter mwenyewe kwa hisia zake mbovu zisizokuwa na uelewa mpana

*Sauti ya Amerika nahisi wata-cover vizuri hii habari.
 
Nimelisikia hilo tena mtanagazaji aliyekuwepo studio alilikuwa amenamuuliza maswali ya msingi lakini yeye alikuwa anajibu anayoyajua yeye, mfano aliulizwa kwenye mkutano wa CHADEMA je viongozi waliswema nini juu ya tukio la mauaji ajabu sana yeye hakujibu alibaki kusema maandamano hayakuwa na kibali cha polisi.
 
Kama BBC wataendelea na mtindo huu wa kurusha habari zenye upungufu mkubwa kama huu, nafikiri ndio utakuwa mwanzo wa kuanza kukosa wasikilizaji huku TZ.
 
Back
Top Bottom