THEMI Sec. School-Arusha

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,219
370
Wana JF,

Nilipita Juzi Arusha Kusalimia ndugu na Jamaa, Lililonistahajabisha ni kijana wa Shangazi yangu Anaesoma Themi Secondary School, Aliponiambia Hawatofunga shule mapema Kwani Head Teacher wao kwa Jina Mr.Mussa, kawambia kutakuwa na masomo ya ziada kwa muda wa siku 17 tokea December Mosi na Malipo kwa kila mwanafunzi itakuwa hivi:

Form I = 5,000/= Tsh
Form II = 5,000/= Tsh
Form III = 10,000/= Tsh

Ndipo nikamuuliza kijana kwa nini mlipe kama walimu hawakumaliza Syllabus? si wajibu wao kumalizia kabla hamjaingia mwaka mwingine,? akania mbia teacher Mussa amesema ndio kisha amua hivyo.

Na Ukijakupiga mahesabu kwa muda huo wa siku 17 mwalimu huyo na walimu watakao wafundisha watakusanya kiasi cha Million 4 na usheee hivi kwa vitado vyote vitatu.

Sasa sielewi Huyo mwalimu mkuu na wenzake hawakumalizia syllabus makusudi ili wawachune wazizi wa wanafunzi hao hizo pesa kwa nguvu??

Nilimwambia shangazi yangu endapo wakianza tu akaripoti haraka kwa afisa elimu wa mkoa hilo swala bila kusita.

Hii ni elimu ya kizazi kijacho kweli ndivyo inavyo andaliwa?:confused:



 
Back
Top Bottom