Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,060
- Thread starter
- #21
Mie niliandika mapema kabisa kuwa sipo hapa Kumtetea Zitto au kusema Zitto hana hatia.
Pia sipo hapa kusema Waandishi wa habari wanasema uongo.
Nafahamu kuwa ukweli siku zote uko katikati.
Ninachosikitika ni kuwa Magazeti yanahusiana na Chadema, kuanza kutumia njia za Zitto. Ni juzi tu hapa watu walimkalia kooni Zitto kwa kwenda TBC na kuongea aliyoongea. Hilo wengi hawakulipenda. Sasa hawa Waandishi, wanafanya hilohilo la kutatua matatizo ya CHADEMA kwenye Media. Hili linaongeza tatizo badala ya kulitatua.
Kila chama kina matatizo yake na hata watu kwenye familia wana matatizo yao. Ila ningelitegemea watu wenye akili zao na Wasomi kama wanavyojulikana Chadema na huku wana wanasheria wazuri sana na wazee wenye busara kama akina Baregu, Slaa nk watakaa na kutatua mataizo yao ndani ya mikutano ya chama na si kuja kushambuliana hapa kama vita ya Iran na Iraq.
Kama mtu anaona kuwa Matatizo ya CHADEMA yatatatuliwa kwa Zitto kwenda TBC na CDM wanamsiliba kwenye magazeti kwa ule msemo "wewe mwaga mboga, mie namwaga ugali........" basi endeleeni hivyo na kila la kheri.