Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,707
Mwanzo ilikua ni familia yenye upendo yenye watoto wawili,Kati ya Jonson Nyathi na Annie Khumalo waliokuwa wakiish Soweto,Afrika ya kusini,mambo yalibadilika baada ya mke wa bwana Nyathi kukutana na mwanadada Deborah Mphulela na kuanzisha mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja yaliyosababisha Annie kudai talaka ili akaishi na Deborah,hakumficha mumewe bali alimwambia ukweli,mume alijaribu kumsihi mke wake na kumkumbushia kiapo walichoapa kanisan lakin mke hakujali,ndipo bwana Nyathi alipopeleleza na kujua alipokuwa anaishi Deborah kisha usiku wa kuamkia jumapili alikwenda kwa mwanadada huyo na kumpiga risasi na kumuua,kisha jumapili mchana akamwambia mke wake kuwa siku hiyo atampa talaka lakini angalau watoke out na watoto wao kabla hawajatengana,Annie hakukataa,mchana wa jumapili majira ya saa kumi jioni Familia yote ya bwana Nyathi ilikuwa ndani ya gari ndipo bwana Nyathi akayumbisha gari kulifuata lori walilokuwa wanapishana na kuligonga na kusababisha ajali iliyochukua maisha yao wote wanafamilia ya bwana Nyathi!Jamani kuweni makini na ndoa zenu!