The tale of Famed British Investor - Unleashing smear campaign against Tanzania?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
He accuses the Tanzanian government of corruption. From the lowest ranked member of Police force in Moshi to the highest officer, from a local magistrate to Chief Justice, from a DC to the President, all of them are corrupt. Why is Mr. Stewart Middleton continues to carry a smearing campaign against Tanzania? Well lets find the answers. This is the first part of my take on the topic. You can read the background of the case on HIS BLOG

The worst part of this is that he claims there is a widespread land invasions against British citizens like what we witnessed few years back in Zimbabwe. He caution other investors to think twice before coming to Tanzania. Do we have a land invasions problem that the international community need to be aware off? Is Kikwete, Police and other judicial officers supervising or enabling groups of locals to grab land from British citizens in Tanzania?

[video=dailymotion;xepzf0]http://www.dailymotion.com/video/xepzf0_the-tale-of-famed-british-investor_news[/video]
 
Hon Mwanakijiji,
Hawa ni walewale wanaokuja kwa unyenyekevu wakikataa kutoa fungu kwa ajili ya uchaguzi wataundiwa kila sababu ya kufukuzwa.Hakujua kuwa ushirika na ccm ni njia rahisi ya kufyonza kuku kwa mrija.ana bahati mbaya huyo.ajifunze kutoka kwa wahindi na makaburu na waarabu wa loliondo
 
Mbona hilo liko wazi jamani Rushwa Tanzania inalidwa na system yote na hata mwananchi wa kawaida sasa ndiyo unatakuwa wale decent investers hawataki hata kuiona TZ.

Wanaokuja wale wajanja tu ambao hawana nia nzuri bali kuja kutajirika kwa mgongo wa watanzania na huku viongozi wetu wakishirikiana nao kwani wanapata 10%. Hata mimi kama nina hela zangu basi Tz inakuwa ndiyo last possible option yangu,rushwa,kukosa uaminifu umesaambaa kila sehemu ya nchi.

Mimi naona siyo smeering bali jamaa anahakikisha anaipata haki yake kwa njia yeyete ile....
 
He accuse the Tanzanian government of corruption. From the lowest ranked member of Police force in Moshi to the highest officer, from a local magistrate to Chief Justice, from a DC to the President, all of them are corrupt.[/URL]

Can't argue with this part
 
He accuse the Tanzanian government of corruption. From the lowest ranked member of Police force in Moshi to the highest officer, from a local magistrate to Chief Justice, from a DC to the President, all of them are corrupt. Why is Mr. Stewart Middleton continues to carry a smearing campaign against Tanzania? Well lets find the answers. This is the first part of my take on the topic. You can read the background of the case on HIS BLOG

I think the Guy is right and it is not only the government but the society as a whole is corrupt, I am wondering whether he change we are expecting may come along soon enough?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu sijui wewe mara ya mwisho ulikuwa lini Bongo lakini babu kuhusu Rushwa wala sii Uongo, Sema labda kinachowatatiza wengi ni hayo majina ya watu lakini mkuu wangu weee acha tu!
 
The problem is not just his accusations which for some of us would give him the benefit of the doubt; the problem is that he has gone to great length to scare British citizens that there is a systematic Zimbabwean style farm invasions widespread in Tanzania. Our famed British investor would have people to believe that his land dispute with Benjamin Mengi is unique to him simply because he is a British investor. While acknowledging the level of corruption in different parts of our society it will be wrong to believe that Tanzanians inmasse are grabbing land from British investors with official help of our government and thus British investors and other people should refrain from coming to Tanzania.

Unless I'm missing something.. do we have a Zimbabwean style land invasions going on in Tanzanian that foreign investors should be aware of?
 
He accuse the Tanzanian government of corruption. From the lowest ranked member of Police force in Moshi to the highest officer, from a local magistrate to Chief Justice, from a DC to the President, all of them are corrupt. Why is Mr. Stewart Middleton continues to carry a smearing campaign against Tanzania? Well lets find the answers. This is the first part of my take on the topic. You can read the background of the case on HIS BLOG

[video=dailymotion;xepzf0]http://www.dailymotion.com/video/xepzf0_the-tale-of-famed-british-investor_news[/video]

Mwanakijiji bana....mbwembwe nyiiingi....lol

Halafu kumbe KLH News bado ipo hai?
 
Jamani, jamani, ina maana nyie mnataka kupingana na Kikwete ambaye anatembea kifua mbele akitamba kuwa ameshughulikia rushwa kwa kuiongezea nguvu za kisheria Takukuru? Na kuonyesha jinsi walivyowakamata watoa rushwa wa chama chake mwenyewe?

Nilisikia diplomat mmoja akimsifu kikwete na utawala wake kwa kushughulikia rushwa na kuwafikisha mahakamani washitakiwa akiwamo mme mwenzie na Mkapa. Sasa si kwamba huyo mzungu anatuonea kwa kutusingizia?
 
unakubaliana kuwa wawekezaji wasije Tanzania kwa sababu Watanzania wanaendesha kampeni ya kuwanyang'anya ardhi raia wa Uingereza kama ilivyokuwa Zimbabwe?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu ni vizuri kufanya uchunguzi kwanza kisha ndio unakwenda mbele. Bongo Utapeli ni mkubwa sana kiasi kwamba hadi vyombo vya serikali na sheria vinatumika kuwanyang'anya watu mali zao..Siwezi kushangaa kabisa kama wapo wawekezaji wametapeliwa wakapewa ardhi kisha wakageukwa na viongozi waliowapa vibali.

Inaweza kuwa staili tofauti na ile ya Zimbabwe na ukubwa wa matukio haya lakini bado ukweli unabakia kwamba wawekezaji wananyang'anywa mali zao. Acha wao mkuu wangu wewe Mzawa pia ni mchezo huo huo. Wakikuweka sawa wanakumaliza na vibali vyako mkononi wapo watajiri mjini wanajulikana kwa kazi hizi hivyo usishangae kabisa mkuu wangu watu wameliwa in billions..
 
Je hili linawahusu wawekezaji tu? Je kuna watanzania wa kawaida ambao wananyang'anywa ardhi zao na viongozi?

Hapana yeye anasema kwa staili ya Zimbabwe na hivyo wawekezaji wasije Tanzania hasa wale wa UK. Hoja yangu siyo hata kidogo kusema kuwa havitokei ninachozungumzia ni kuwa huyu jamaa ameanzisha kampeni ya kutaka UK isitishe misaada yote kwa Tanzania hadi suala lake limalizwe na watu ambao tayari amewahukumu kuwa ni mafisadi wa kutupwa. Nafahamu yanayotokea Kilosa na Tarime, yapo yanayotokea Kigamboni na Kilombero; je watu wameacha kutafuta haki zao mahakamani?

Ninawafahamu watu wa karibu kabisa ambao baada ya muda wa kuhangaikia ardhi yao iliyouzwa kinyemela waliweza kupata haki yao kwenye Mahakama ya ardhi. Wapo pia watz wengine wengi ambao wanatumia mfumo huu huu pamoja na mapungufu yake tunayoyajua kuweza kupata haki zao. Na hadi hivi sasa sijaona kiasi cha kulinganisha matatizo hayo ya ardhi na kile kilichotokea Zimbabwe. Unless unaweza ukanipa maelekezo kidogo.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nadhani wewe unafikiria kama Mtanzania na kwa maslahi ya Tanzania (mzalendo safi) lakini kama utakuwa huru na ukajiweka hata katika nafasi yake basi ungeweza kumwelewa kwani huyu ni mmoja kati ya wawekezaji wengi waliokuwa frastrated na hali halisi ya uwekezaji nchini ambapo unaweza kupoteza mtaji ambao ni maisha yako yote.

Kwa hiyo kama ingekutokea wewe na ukarudi Marekani au UK ambako ndiko kwenu ungehakikisha kitendo cha kudhulumiwa wewe kiweze kuchukua uzito mkubwa zaidi kukomesha Ufisadi wa nchi husika. Na binafsi nadhani malalamiko kama haya badala ya sisi kumtazama huyu Mzungu na kuanza kumlaumu kwamba kaenda nje ya ukweli ni bora zaidi tukijitazama sisi na kufanya marekebisho makubwa ktk kuhakiikisha haki ya wananchi haipotei kwa Utapeli uliokithiri nchini.

Huyu mtu hakuzoea kabisa kuona vitu hivi na pengine hata yaliyotokea Zimbabwe hayajui kwa mapana yake ila anachojua yeye ni kunyang'anywa ardhi na mwananchi (mtu mweusi) kwa sababu tu yeye ni mgeni, mzungu na mwekezaji. Hivyo aka draw conclusion yake kuwa ndio sababu ya dhulma inayotendeka na kwamba yeye sii wa kwanza ila wapo wazungu wengi wamepigwa kama yeye, pasipo kufahamu kwamba Utapeli Tanzania hauna formula na sheria inawalinda hawa Matapeli ambao wengi wao wanashirikiana na viongozi pamoja na vyombo vya sheria..

Mkuu wangu Tanzania tumefikia sehemu ambayo hata mimi ningependa wawekezaji wasije tena kwa sababu hawana faida nasi kama sii wao kupoteza mali zao. yaani mfumo wa uwekezaji nchini ni pata potea kama kamali vile hivyo ni bora hata wasije hadi pale tumejiweka sawa kwani hata Zimbabwe leo hii wawekezaji wamerudi baada ya... na nchi inarudi vizuri kiuchumi kwa sababu Policies zimerekebishwa na kuna guarantee ya sheria kuwawezesha kuwekeza.

Nilipokuwa Bongo pale TRA nilikutana na mzungu mmoja Mswedesh ambaye pia alikua na vifaa kibao vya kufungua kiwanda akakwamishwa ushuru ktk vifaa ambavyo aliambiwa (ubalozini Sweden) vinapata msamaha (ujenzi wa beach Hotel) kufika Bongo picha tofauti kabisa ikabidi kuingia gharama nyingine kurudisha mali zake zote Sweden, tena baada ya mimi kumshtua laa sivyo Wabongo walikwisha mweka sawa atumie kampuni yao vitapata msamaha hali wakipanga jinsi ya kummaliza.

Ndio Bongo tulikuwa nayo leo mkuu wangu.....
 
Mkandara, tatizo ni hili la kutaka wawekezaji watendewe tofauti na wabongo wenyewe; wakati miminajaribu kupanua wigo huu kwamba tuna matatizo haya haya kwa Watanzania wenzetu. Sipendi kuona mwekezaji ati kwa vile ni mgeni basi anataka kuonesha ulimwengu kuwa kuna kitu kinaendelea against wawekezaji kumbe ni kitu ambacho tunakipigia kelele kila siku na kinawahusu Watanzania wote.
 
unakubaliana kuwa wawekezaji wasije Tanzania kwa sababu Watanzania wanaendesha kampeni ya kuwanyang'anya ardhi raia wa Uingereza kama ilivyokuwa Zimbabwe?
Nilijua hutanielewa. hahahahahahahaha. Mwanakijiji you always knows my side on this issues na nilitegemea utanielewa. Angalia avatar yangu. hahahahahahahaha
 
Je hili linawahusu wawekezaji tu? Je kuna watanzania wa kawaida ambao wananyang'anywa ardhi zao na viongozi?

Mwanakijiji ebu fikiri kidogo je kama anakuja mwekezaji kwenye madini Buzwagi na kukuta juu ya ardhi unadhani utaambiwaje? Wakikupendelea watakupa pesa ambayo huwezi kununua hata ng'ombe 5 na kwa msukuma hizo ataona nyingi na atahama anapenda hapendi. Je hawa si ni sawa wamenyang'anywa ardhi yao bure?
 
Mkandara, tatizo ni hili la kutaka wawekezaji watendewe tofauti na wabongo wenyewe; wakati miminajaribu kupanua wigo huu kwamba tuna matatizo haya haya kwa Watanzania wenzetu. Sipendi kuona mwekezaji ati kwa vile ni mgeni basi anataka kuonesha ulimwengu kuwa kuna kitu kinaendelea against wawekezaji kumbe ni kitu ambacho tunakipigia kelele kila siku na kinawahusu Watanzania wote.
Mkuu sisi tutaeleza matatizo yetu na wao wataeleza matatizo yao. Kama mtu kaweza fika kwenye sheria yetu na ikashindikana unafikiri huyu jamaa atakata tamaa kama sisi na kumwachia Mungu?.

Hivi hujiulizi kwa nini nchi kama Marekani wanavamia nchi nyinginezo kwa kusingizia Utawala uliopo hali ni ktk maswala yanayohusu zaidi maslahi yao!.. Tukumbuke tu kwamba tuna deal na wazungu ambao wao wapo pamoja na wameungana kama kitu kimoja ktk huu mfumo wa mpya. Auawe mzungu mmoja Tanzania utaona jinsi watakavyo kuja na hata kuulazimisha utawala wetu utoe maamuzi wanayowafikiria wao. Lakini wakifa Watanzania 10 hata 100 hata iwe kwao hawatajali (gang related case) hivyo ni jukumu letu sisi kuwa na nguvu ya kuhoji kama wao.
 
Back
Top Bottom