The Secret: IPTL kuwasha mitambo miezi 3 ijayo!?

Hii nchi ni ya kuliwa. Watendaji wanaogopa kusema haiwezekani. Huyo Rugonzibwa na Ngeleja wanajua kila kitu na Rugo alikuwapo kikao cha wataalamu ambacho Wartisala iliweka bayana kwamba hadi miezi mitatu baada ya wao kulipwa.

Wanaogopa kumwambia JK hayo, wanawabembeleza IPTL, "Jamani washeni tu, tusimwaibishe Rais" alaaaa!!!! Yaani wakati anazungumza kwanini musiwe mumemshauri kabla? Au sasa kwanini asiseme "nimeona kuwashwa kwa mitambo hakuna maslahi kwa Taifa, maana tutaingia hasara" badala yake wanatoa fedha HAzina na kuwapa!!!

Miezi hiyo mitatu mvua za elnino zitakuwa zimeanza, mwabwawa yatajaa, na hizo fedha zingetolewa kama advance kuagizwa mitambo yetu ama wangepewa Tanesco wakapanga mambo yao na si kwa amri za wanasiasa tungetarajia agueni.
 
Umeme wa IPTL sasa kuwaka 2010

  • Wataalamu wasema ni hatari kuwashwa haraka
  • Wanahitaji miezi mitatu ya maandalizi

NA WAANDISHI WA RAIA MWEMA

MATUMAINI ya kuwashwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme ya inayomilikiwa na kampuni tata ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), yanazidi kupungua baada ya wataalamu kusema wazi kwamba mitambo hiyo haiwezi kuwashwa hadi mwaka 2010, zaidi ya miezi mitatu kuanzia sasa.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kwamba pamoja na maelezo ya kutia moyo kutoka kwa viongozi na watendaji wakuu serikalini, hali ni tofauti baada ya kuelezwa kwamba hata Serikali ikifikia makubaliano na IPTL, hakuna uwezekano wa kuwashwa kwa mitambo mwaka huu.

Sababu mahususi zilizobainika na kuthibitishwa na nyaraka rasmi za Serikali na IPTL, ni pamoja na za kiufundi na zile za kisheria; zote zikiwa zinaonyesha kwamba inahitajika zaidi ya miezi mitatu kuwezesha mchakato wa kuwashwa mitambo hiyo kwa usalama bila kusababisha athari.

Raia Mwema inazo nyaraka ambazo zinaonyesha kwamba kampuni inayoendesha mitambo ya IPTL ya Wartsila Tanzania Limited, imeiarifu Serikali waziwazi kwamba ni vigumu kuwasha mitambo hiyo katika kipindi cha miezi mitatu baada ya makubaliano kati ya pande zote husika kufanyika.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kwamba mara baada ya kuingiwa kwa makubaliano hayo, inahitajika miezi mitatu kuruhusu uagizwaji wa vipuri na maandalizi mengine kwa kuwa si salama kuwasha mitambo hiyo kabla ya maandalizi muhimu kukamilika.

Maelezo ya Wartsila na habari za ndani ya vikao vya majadiliano zinaonyesha kwamba Wartsila wameonyesha kwamba haiwezekani kuweza kuwasha mitambo hiyo kwa usalama ndani ya miezi mitatu kwa kuwa kunahitajika pia kuwaandaa wataalamu watakaofanya ukarabati wa mitambo hiyo, ambayo imekaa muda mrefu bila kutumika, na pia wa kuendesha mitambo hiyo.

Mwenyekiti wa kikao cha majadiliano kati ya Tanesco na IPTL alikuwa ni Gregory Chegere kutoka Tanesco akiwa na wataalamu wenzake watatu kutoka shirika hilo, Lewanga Tesha, John Kabadi na Stephen Manda wakati IPTL iliwakilishwa na Magesvaram Subramaniam na Veneralis Jigge.

Theophil Mujunangoma Rugonzibwa aliingia kama mfilisi na msimamizi wa IPTL wakati Wartsila iliwakilishwa na Kari Kaivola na Jaakko Kaihua. Karel Daele anatajwa kuwakilisha kampuni ya uwakili ya Mkono & Company na Ryan Kerchn akiwakilisha kampuni ya Hunton & Williams.

Mbali ya hitaji la uagizwaji vipuri na kuandaliwa kwa wataalamu, Wartsila wameieleza Serikali kwamba kutahitajika ukaguzi na uwashwaji wa awali wa majaribio na upatikanaji wa fedha kutoka serikalini.

Hata hivyo, pamoja na maelezo hayo kutoka kwa Wartisila na wataalamu wa Serikali walioshiriki katika majadiliano hayo, Serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, imedai kwamba mitambo ya IPTL itawashwa wiki hii.

Raia Mwema haikuweza kumpata Ngeleja mjini Dodoma jana Jumanne, lakini alinukuliwa na gazeti la Serikali la Daily News, toleo lake la jana, akisema kuwa mitambo hiyo itawashwa “wakati wowote wiki hii” baada ya kukamilika kwa mchakato wa kufikisha mafuta katike eneo la Tegeta ilipo mitambo hiyo.

Mbali ya mafuta, Ngeleja alisema fedha kwa ajili ya kuilipa IPTL kwa kazi hiyo zilikwisha kuingizwa kwenye akaunti ya kampuni hiyo juzi, na kwamba kuchelewa kuwashwa kwa mitambo hiyo kumetokana na kuchelewa kwa hundi kutoka Hazina kabla ya kupatikana mwishoni mwa wiki.

Pamoja na Ngeleja, mfilisi wa IPTL, Rugonzibwa, ambaye ni mmoja wa washiriki wa vikao vya Serikali vilivyoelezwa wazi kwamba mitambo hiyo haiwezi kuwashwa kabla ya miezi mitatu, amesema itawashwa wiki hii.

Rugonzibwa amenukuliwa akisema kwamba fedha ndio zilizokwamisha kuwashwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme mwishoni mwa wiki na kwamba inatarajiwa kuanza kuzalisha umeme wiki hii.

Rugonzibwa amesema kwamba kiasi cha Sh. bilioni 15 zimekwishatolewa kwa ajili ya kuanza kuwashwa kwa mitambo hiyo na kwamba hata mafuta kutoka TIPER kwa ajili ya kuwasha mitambo hiyo yanatarajiwa kuwasili Tegeta wakati wowote.

Fedha zilizotolewa zimeelezwa kwamba ni kwa ajili ya malipo ya awali (advance) kwa ajili ya miezi mitatu ya kwanza na ada ya maandalizi.

Habari za ndani zimeeleza kwamba maelezo ya Ngeleja na Rugonzibwa yametokana na kuogopa kutoa kauli ya kumkatisha tamaa Rais Jakaya Kikwete ambaye ametoa maagizo ya kuwashwa kwa mitambo hiyo. Ngeleja ni mteule wa Rais na Rugonzibwa ni mtumishi wa Serikali kupitia Wakala waUsajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

Rugonzibwa alisema fedha zilizotolewa zinalenga kuwalipa Wartisila, Kampuni ya mafuta ya Total na wataalamu waliopo pamoja na wengine ambao wanatarajiwa kufika nchini muda wowote kwa ajili ya kushughulikia mitambo hiyo.

Pamoja na maelezo kwamba fedha zimetolewa kupitia Hazina, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo amenukuliwa akisema kwamba wanaopaswa kujua kuhusu kuwashwa kwa mitambo ni Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), wakati shirika hilo limeelezwa kusubiri mitambo iwashwe na wao kusambaza umeme kwa kuwauzia wateja.
 

Attachments

  • RAIAMWEMA_Umeme.JPG
    RAIAMWEMA_Umeme.JPG
    33.2 KB · Views: 36
Giza, hakuna anayejali, mambo kwenye SIII HASSAAAA!!!! Kazi kweli kweli
 
Watu wameshasahau Richmond wanasikiliza ngonjera za kina Sophia Simba!!!! Hii kweli Tanzania. KWanini hawa jamaa wanatuchezea akili lakini....ngrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!
 
JK aliagiza iwashwe. Hakutaja tarehe kama alivyofanya Zitto. Wanaoijua mitambo ile kwa karibu wanasema hata ikiwashwa haitamaliza mwezi. Ilichoka tangu inasimikwa pale Tegeta-Salasala.


Huo ni uongo mkubwa, mitambo ile ni mizima sana tu waulize Tanesco wanijua vizuri sana, kila wakifanya capacity test kila mwaka ilikuwa inafaulu vyema sana. kupafom capacity test muda ni saa 4 mfululizo at full load ie.103 MW.Record zipo tanesco ukibisha hulazimishwi.

Kwamba itachelewa kuwashwa hilo halina ubishi, kitalam ni lazima taratibu zote za kiusalama wa mitambo na waendeshaji zizingatiwe. Kama gari yako iko juu ya mawe kwa miaka 2 kisha unaikumbuka na kuamua kuiendesha umbali mlefu, say 500km bila kufanya checkup ya kujiridhisha, unaweza usirudi nayo au ikakupoteza (kufa)........Jamaa wako kwenye mkondo sahihi tu wakulaumiwa ni WANASI-HASA wetu!

**********
amani yetu inatumika vibaya.
 
Wartsila wana contract ya maintenance kwenye hii plant ya IPTL.Hawajalipwa kwa miaka yote hiyo miwili tangu isimamishwe.Wawekezaji walivyo, that is an opportunity to return their money.

But as well kuna plant nyingine pembeni ya IPTL inayomilikiwa na Tanesco yenye capacity ya 45MW.Itawashwa lini?

Kwanini tusijenge power plant zetu wenyewe badala ya kuwatumia watu kama IPTL? Mbona ile ya 100MW ya ubungo na 40 MW ya mwanza ambazo zilikuwa kwenye plan hazisemwi zimeishia wapi?


Hiyo ya 45 MW ikiwahi ni january 2010 ingawa SIHASA ilisema nayo iwe tayari come 1st of Nov 09 kana kwamba kusema ndiyo kutenda
 
What? Hapa tunapoongea mgao ulikuwepo au ulipunguzwa au ilikuaje? Maana mi sielewi hapa hadi kichwa kinauma, naomba kufahamishwa wakuu

Nilikua najiandaa kuteremka huko
Nenda na Generator lako tu. Bongo tambarare!
 
What? Hapa tunapoongea mgao ulikuwepo au ulipunguzwa au ilikuaje? Maana mi sielewi hapa hadi kichwa kinauma, naomba kufahamishwa wakuu

Nilikua najiandaa kuteremka huko

mkuu kabla hujapewa jibu la hiyo swali. habari mpya ni kwamba bei ya mafuta imeshuka kwa wastani wa 9% kuanzia kesho.
 
I think Invisible is part of the problem

Threads kama hizi ndizo zilitakiwa ziwekwe hapa sio kutuletea mambo ya CHADEMA vs CCM

Threads ulizozistick zimejaa ushabiki mptupu mimi sielewe kuweka threads za nyerere au za Nape na bashee kutaka tuwape maoni juu ya mabadiliko ya katiba za vyama vyao zitatusaidia nini kwenye sticky wakati kuna Issues kama hizi zimekaa tuu


Bro you need to go back to the basics
 
I think Invisible is part of the problem

Threads kama hizi ndizo zilitakiwa ziwekwe hapa sio kutuletea mambo ya CHADEMA vs CCM
Mkuu,

Slogan ya "Where we Dare to Talk Openly" inatubana... Lakini Great Thinkers hawatakiwi kuwa carried na hoja za wanasiasa na kusahau masuala muhimu kama haya.

Well, tuliombwa tuache kuziweka hizi kwa sana maana watu walianza kuwa 'confused'; tukawambia TUNASITISHA KWA MUDA ili kuweza kuiweka JF iwe user friendly.

Kumbuka JF imepita katika mazingira magumu tu
 
Mkuu,

Slogan ya "Where we Dare to Talk Openly" inatubana... Lakini Great Thinkers hawatakiwi kuwa carried na hoja za wanasiasa na kusahau masuala muhimu kama haya.

Well, tuliombwa tuache kuziweka hizi kwa sana maana watu walianza kuwa 'confused'; tukawambia TUNASITISHA KWA MUDA ili kuweza kuiweka JF iwe user friendly.

Kumbuka JF imepita katika mazingira magumu tu


Kaka tatizo ni kuwa nchi iko gizani na tushaambiwa kila mmoja afanye analoweza kuleta solutions lakini pia katika kuleta solutions lazima tujue tulikotoka na pia kujua tatizo lilianza vipi.

Tazama threads ulizozifanya sticky. ... ile heshma ya sticky ishaondoka

what we need ni kuachana na mentality ya kuwa against kila kitu na kuwa more kwenye ku CHANGE the system kwa namna mbali mbali kama vile kuwa vocal kwenye mambo ambayo tunajua wa tawala watayaona na mabadiliko yanaweza kutokea

Mfano sioni sababu ya BRELA kupewa green light na uhuni wao wakati issues zilishakuwa addressed kuwa software ya 1 billion haifanyi kazi na walichofanya vijana wako wakaenda kuificha kule BIASHARA ilihali ungeaiacha hapa tukakamua mpaka kieleweke tena ikawa ni sticky...kwa sababu ni jambo lililondani yetu


Kuna issue ya PPF ambako kuna matatizo ya staff kuzuiwa kutumia JF lakini kwa hizi post mbili tatu tumeweza kufanikisha walau akina zito wameweza kuwabana akina erio na impact inaonekana

Kuna issue hii ya leo uliyoleta ya pesa za bajeti kupunguzwa....someone should have sticked that thread

and of course WEBSITE ya ikulu nayo tungeweka thread hapa ya ku count na kuendelea kumpiga maswali Salva na crew yake

kaka thats how people make changes....

we DONT NEED THESE:

UVCCM: Maoni juu ya Reform [Survey]
Nyerere: The Man, The Myth and the LegenD
Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze
Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: JK anayo




 
Wakuu gharama ya kununua mitambo mipya ya angalau 100MW ni kiasi gani, tuanzie hapa

Hili ndilo swali langu kila siku, nashkuru siko mwenyewe

kwanini tunakuwa reactive instead of being pro-active??????????

%^$(^*&%^($^%(*) AAaaaaaaghhhhhhhh

kuna mitambo ili inayokwenda MWANZA NI billioni 300+
Tatizo bei zetu zimekaa kirada rada sana

ila kama ziko sahihi ni hela ndefu
 
Back
Top Bottom