The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
chama cha mapinduzi hakitaaungushwa na watu kugombea nafasi nyingi, hilo lilifanyika 1995, 2000, na 2005.

Hivyo hoja siyo kusimamisha wagombea ni mfumo mzima. CCM itaangushwa kwa mikakati ya kisiasa, ambayo imekosekana sana kwa upande wa wapinzani. Hadi hivi sasa wapinzani wanaenda siasa kama sanaa, badala ya kuchanganya sanaa na sayansi. CCM wameshafuzu mambo haya, ni mabingwa wa usanii na pia hufanya mambo yao kwa sayansi ya siasa.

Mnachokiona CCM ni matunda ya Kivukoni na Bulgaria na Chekoslovakia n.k!! Hivyo kuweza kushinda ni lazima upinzani ubadiliki mtindo na mikakati.
 
Wananchi naomba mchangia mada hii ajikite kwenye maana na nia ya mada yenyewe. Kusikia na mambo ya kuungana haya endani na ninacho kisema .

Naomba nirudie kwamba naomba mtu ama watu waseme ama waitikie ombi langu bila ya kutoka nje . Tuache kusema sanaa . Tuache kuwa onyesha watu njia kwa mbali .Tuingie humo ndani sasa .Nakubaliana na wazo la Pressure groups lakini kwa sasa naomba tuchague majimbo na tutembelee huko ili kuweka sawa mambo .

Mgombea huru ruksa Tanzania wengien tutaingia huko ambao hatuna vyama na hatuamini katila vyama .
 
Kwa sasa huwezi kugombea kama mgombea binafsi kwa vile mahakama iliamuru serikali iweke utaratibu wa kuhakikisha kunakuwa na wagombea binafsi; hivyo mpaka kurudi tena bungeni! Back to square one.
 
Sasa kama serikali haitaki kuweka utaratibu na chaguzi zinakuja dawa ni ipi ? Kwenda mahakamani tena ama kufanyaje ?
 
Sasa where do you start from ? Wacha mimi niende Tunduru nichukue form ya kugombea waninyime then niende Mahakamani kusimamisha uchaguzi hadi shauri lipate uamuzi Mahakamani kwa mara nyingine bila hivyo CCM will never learn hata mara moja .
 
Mimi nitarusha kadi yangu tu mtake msitake .Na wengine nasema njooni twende .
 
Kutakuwa na Takrima?

A valid question lakini naona hakuna aliyetaka kulijibu.

Lunyungu et al mnaotaka kugombea nawatakieni kila kheri katika mapambano hayo lakini kumbukeni TAKRIMA rukhsa!

Kugombea for the sake of kugombea wakati mnajua fika mtapoteza ni matumizi mabaya ya raslimali zenu. CCM wataelekeza nguvu zao zote, uongo wao wote, rushwa zote, matumizi ya dola yote na kila mbinu safi na chafu kwenye uchaguzi wa Tunduru. Upinzani uungane usiungane jimbo lile hawawezi kushinda.

Lunyungu,
tatizo si kwamba majimboni hakukuwa na wagombea, bali mfumo wetu nchini ndio mbovu. Rejea watu Kama huyo Chitalilo aliweza kushinda huko Buchosa ni nini kitafanya nyie mnaotaka kwenda kugombea mshinde?

Kila anayetaka kugombea labda atafute tiketi ya CCM na hapo ndipo mnatakiwa mwanze na takrima, kuchafuana majina na mengineyo kibao. vingine bakini huko mliko mtengeneze maisha yenu.
 
tatizo si kwamba majimboni hakukuwa na wagombea, bali mfumo wetu nchini ndio mbovu. Rejea watu Kama huyo Chitalilo aliweza kushinda huko Buchosa ni nini kitafanya nyie mnaotaka kwenda kugombea mshinde? Kila anayetaka kugombea labda atafute tiketi ya CCM na hapo ndipo mnatakiwa mwanze na takrima, kuchafuana majina na mengineyo kibao. vingine bakini huko mliko mtengeneze maisha yenu.

ahaa sasa nimeelewa kwa nini jezi ya kijani muhimu!! na nnaanza kupata wasi wasi kuwa hizi hizi jezi huenda ndio chanzo cha CCM kuanguka, maana kwa nilivyoelewa sasa kila mtu atahisi abanane humo humo, maana ukiwa nje watagundua kuwa ww umakini kwa hio by any means watakuramba.

Hivi ni sawa nnavyoamini kuwa huenda wengine wanaovaa hizo jezi wanajua fika kama CCM bomu ila no means ila kulengesha ili ufike ukutakako?

nnaomba nipatiwe shule,
 
Tabasamu
Msimamo wangu ni ule ule kwamba mimi naenda kule kama Mgombea binafsi. Nia yangu ni kutaka kuifanya sheria ya Mgombea binafsi iwekwe wazi na watu wajimwage.

Loook here hatuwezi kuogopa na ku back off then tunaishia jambo ku direct no . Huo si uzalendo ni uoga . Sheria zao za kuwabana wapinzani lakini aina Zitto walipatikana .Twendeni , takrima hakuna ilisha sema kwamba ile ni rushwa . Ilifutwa baada ya kumpa Muungwana ukuu . Kazi ni kubwa sana mbeleni. Tuache uoga tuingie nma swala la kusema tunajua tutashindwa na mawazo ya uzembe . Hujaingia unasema kushindwa ?

Nenda panda mbegu ukishindwa kubali lakini baadaye wananchi wakikiona cha moto watakukumbuka.

Nasema tena twendeni Tunduru tusitafute excuse
 
Uchaguzi wa 2010 na Wachambuzi wa siasa

Tuache dhana ya kutoa majibu rahisi kwamba kiongozi ni lazima aongoze vipindi viwili na ni lazima atoke CCM. Tujaribu kufikiri ndani zaidi.

Wachambuzi wa siasa hebu tupeni uchambuzi wa uchaguzi wa 2010 utakuwaje!

1. Nani atakuwa Raisi wa jamhuri na ni kwanini atashinda?
2. Vyama vitasimamisha wagombea gani katika nafasi ya uraisi?
3. Je CCM itaongeza viti vya ubunge? au wapinzani wapata vingi zaidi
4. Idadi za kura za wapinzania itaongezeka ama itashuka?
5. Ilikuongeza ushindani wa kisiasa vyama vifanye nini?
 
Mi nahisi kutoka CCM hizi namba mbili zitachuana;
- Edward Lowasa
- Fredrick Sumaye
 
Mi nahisi kutoka CCM hizi namba mbili zitachuana;
  • Edward Lowasa
  • Fredrick Sumaye

Samahani Saikosisi,
Mie nadhani bado wewe unatoa majibu rahisi.
Hapo haujachambua bali umetaja,tafadhali njoo na hoja za msingi na mawazo tofauti. Sawa hata kama bado CCM kwanini hiwe hivyo.

Mimi nataka kujifunza kutoka kwako tafadhali.
 
Raisi anayefuata atatoka CCM kwa sababu ndio wenyewe wenye usukani saa hii na wanazidi kujiimarisha.

Pili, wapinzani bado hawana nguvu kabisa hasa kwa wapiga kura kibao waliopo vijijini.

Kisha wapinzani wanaogombea ni hao hao kila uchaguzi wame-expire hakuna mwenye mvuto!
Wachambuzi wa mambo ya siasa leteni hoja.
 
Nahisi mzee Zero atachuana na mfugaji ,lakini mfugaji anayo nafasi nzuri kwa sababu tiyari yupo kwenye system pia kunaweza kuibuka makundi mengine ndani ya chama cha mafiluni maana wao wapo kama mafisi maji yaonapo uchi.
 
Mi nadhani muungwana JK, as long as Maulana kampa uzima kama wengine, atagombea nafasi ya uraisi wa jamhuri yetu kwa mara nyingine. Na kama akigombea nina imani "hatapingwa ndani ya chama".

Unless ndo upinzani aliotabiri mwalimu uanzie hapo! Na kwa hali ya kisiasa TZ ilivyo sasa, CCM still have a lease of chances to occupy ikulu kwa sababu so far MIMI naona hakuna credible opposition with credible alternative views and solutions for the current plight of our motherland.

By the way in politics there are always suprises. Kwa hiyo anything can happen. But so Far Mr. Tluway, if he is really interested to join the race, has an uphill battle to mend fences with his foes and also repair his image which has been shattered by corruption allegations especially in the eyes of wananchi.

Very few have trust in him. And never undermine the power of incumbency in African countries! Maana mtu akiwa madarakani..he has virtually everything to make him succeed in his mission. FS KNOWS IT BETTER, BECAUSE HE WAS ONCE THERE.
 
Mimi nadhani uchaguzi ujao utakuwa na nguvu kubwa sana ikiwa wapinzani wataweza sikiliza wananchi badala ya kusikiliza nyoyo na mapenzi yao.

Mathalan wafanye kama Kenya. Waungane kisha nafasi ya mgombea Urais waiache hadi dakika za mwisho baada ya CCM kutangaza mgombea wao! iwe JK, Lowassa au Achumani kisha wao ndio walitoe BOMU....(Wamemvuta kiongozi mzito toka CCM - yaani mtu neutral kwao wote! mathlan Salim au Malecela kama alivyovutwa Kibaki..

Hapo mzee wangu ngoma ipo kwani kumbuka CCM miaka yote wamekuwa wakiogopa sana mtu maarufu toka kwao kuingia Upinzani.

JK mwenyewe alitishia kufanya hivyo na kama kweli CCM ni imara kama ilivyokuwa wakati wa Mwl. Nyerere, JK asingepita yangemkuta ya Malecela! JK alifanya kosa kubwa sana ndani ya chama hicho!...KUTISHIA! lakini waliogopa matokeo kwani wanafahamu Tanzania watu bado wanachagua sura za watu na pia kuna baadhi ya watu wameisha kuwa na mvuto....
 
Mathalan wafanye kama Kenya. Waungane kisha nafasi ya mgombea Urais waiache hadi dakika za mwisho baada ya CCM kutangaza mgombea wao! iwe JK, Lowassa au Achumani kisha wao ndio walitoe BOMU....(Wamemvuta kiongozi mzito toka CCM - yaani mtu neutral kwao wote! mathlan Salim au Malecela kama alivyovutwa Kibaki..

wazo kiboko hili. Lakini sio jipya na nafikri limeshajaribiwa sana. Labda kama mwaka huo kutakuwa na watu daring kutoka CCM. Siku zote hao wenye mvuto unaowataja wamesita kabisa kuingia kambi ya upinzani.

Pengine tofauti kubwa kati yetu na wakenya (maybe Ugandans as well) ni kwamba kwetu risk takers/daring people ni shida kuwapata. Sisi ni hodari wa kutoa visingizio linapokuja swala la harakati.
 
Back
Top Bottom