ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,460
Sahihisha thread yako kwanza Kijana. Sio Phil ni Phiri
Kijana, si wazee wa bara hatuna "R" na "L". please note that.
Sahihisha thread yako kwanza Kijana. Sio Phil ni Phiri
CECAFA imetuonyesha MAXIMO ni nani, WaTZ mnasemaje? Hii sio aibu ya nchi? Uzalendo na nidhamu anavyotoa kama vigezo vya kuwakataa wachezaji hawa mbona yeye vimemshinda? Ni jana tu amelimwa barua ya utovu wa nidhamu na CECAFA. Kocha gani huyu mhuni. Mie binafsi nimemuona kwenye TV baada ya mechi na RWANDA akimshambulia wazi wazi kwa matusi kocha wa Rwanda. Je, kocha wa Rwanda alikuwa anacheza au alikuwa Refa. Mpira umeisha matokeo yamipatikana kutokana na maelekezo yake au aina ya uchezaji alitaka. Sio hapo tu TZ ni timu iliyoonyesha nidhamu ya hali ya chini sana. Kufunga kumechangiwa na kuwa na wachezaji pungufu kutokana na wachezaji kutojua kuwa makosa au rafu zisizo na maana uwanjani zinaigharimi timu. Haya kila mechi TZ walikuwa wakimaliza mpira wakiwa pungufu. Jamani mnakubali kuwa refs walikuwa wanatuonea kama sio reflection ya quality ya COACH. PIMA NA TOA UAMUZI.
Mshirikina tena? duuh! unahasira inaonyesha ukikutananae mitaa furani unampa za chembe teh tehTuna imani tunaweza kuliko kuwa na kocha MSHIRIKINA kama huyu, hatufai kwa lolote, majungu tu ka kakulia Tandare kwa bi nyau.
Walio mleta nchini chukueni mzigo wenu huo umetushinda kuubeba - HAUBEBEKI. kama contract ataimalizia kwao brazil.
simba ingewakilisha vp Tz wakati yenyewe ni klabu yenye wachezaji kutoka Uganda na nchi nyinginezo, mkuu vikilia kwanza kabla hujamwaga maoni...... kwa busara na hekima maximo aachie ngazi amuachie mwingine na kama tatizo sio yeye tutaliona coz ameifundisha timu kwa muda mrefu sasa, kuna uwezekano mkubwa hakuna jipya atakaloliongeza zaidi ya kuhangaika jinsi ya kuweka mambo sawa,...its tym 2 go now max!..Kwa nini Simba isingewakilisha Tz kwenye challenge lazima wangerudi na kombe!!! Phiri yuko juu!!..utawasikia sasa hivi wale wa homa ya manjano!!!!!!!!!!!!!!
Jee huyu mtangazaji wa michezo wa kimataifa wa Redio 1 Abdulmuhammed anaubia na Maximo? Kwani imekuwa kawaida ktk kipindi chake cha michezo akimtetea na akisema hafai kulaumiwa. sasa kama yeye maximo hafai kulaumiwa nani wa kulaimiwa ktk timu yetu ya taifa?
...Mtangazaji wa kimataifa??!!!Jee huyu [COLOR="Blue"[/COLOR]wa Redio 1 Abdulmuhammed anaubia na Maximo? Kwani imekuwa kawaida ktk kipindi chake cha michezo akimtetea na akisema hafai kulaumiwa. sasa kama yeye maximo hafai kulaumiwa nani wa kulaimiwa ktk timu yetu ya taifa?
Nyie acheni unazi bwana, miaka kadhaa iliyopita hakuna hata aliyekuwa akijishughulisha na timu ya taifa....tena kuna wengine walikuwa wakitabiri kufungwa kabla hata timu haijaingia uwanjani....nasema mwacheni afanye anavyoweza.
Kwanza mlishajiuliza akitoka maximo atakuja nani? Huyo mzirai anaesambaza fitina yuko hoi bin taabu atuonyesha basi kwanza kwa soka la wadada limefikiwa wapi. Mnanikera sana mnaojifanya mmemchoka kocha maximo. Jengeni uvumilivu na subra eboo! Nyie mliona wapi mtu katoka jela tu anaanza kujenga majumba au kutanua na mihela kibao.
Nasema tena mwacheni kocha maximo afanye kilichomleta nacho ni kujenga soka la tanzania, leo wapo watu wanatamani kushuhudia japo mazoezi ya timu ya taifa wakati zamani ilikuwa kichekesho kutaja neno taifa stars. UKWELI UNABAKI PALE PALE MAXIMO BADO ANAHITAJIKA SANA NCHINI KWENU....mkiweza tutajie mbadala wake. Mnataka kuleta haditth za Riki Abadalah na takwimu za intaneti.
Yawezekana Maximo anafaa kufundisha Kabumbu, lakini hadhi yake siyo ya Kocha wa Timu ya Taifa bali angefaa zaidi kama angeenda sehemu kama Shule ya Makongo hivi ambapo angepata fursa ya kufundisha tu pasipo kuhitajika keshinda vikombe. Kocha wa Timu ya Taifa au Timu inayoshiriki ligi ufanisi wake unapimwa kwa vikombe na siyo kufukuza wachezaji kwenye Timu. Kama ni nidhamu nayeye ameonyesha kutokuwa nayo kiasi cha kupelekea kuonywa na CECAFA.
Kimsingi Maximo hastahili kuinoa Timu yetu, ila tu bahati mbaya iliyopo ni kwamba ni Mwajiriwa wa Mkuu wa Kaya sasa TFF inawawia vigumu kumtupia virago.
Maximo mwisho atagombea ubunge tu hapa bongo..
..Halafu Maximo amelainika na kuikubali zanzibar kuwa ana-feel proud kwa kupata nafasi ya 3 eti ni sifa kwa Tanzania....??!!yote kwa yote... Hongera Zanzibar kwa kumfunga mdomo Maximo....