The Rise and Fall of Hamad Rashid, L.Mrema, J.Cheyo and small boy Kafulila

King Suleiman

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
496
327
Salaam wana JF,
hakika nimeshuhudia anguko kubwa sana kwa hao wazee na kijana mmoja katika siasa za Tanzania. mwanzoni wote walijijenga kama wanasiasa mahiri na wakombozi wa Tanzania, lakini sasa wanaanguka na kupotea kabisa kama dola ya Rumi au Mnara wa babeli kwa matendo wanayoonyesha watanzania kwa uroho na ubinafisi wa kung'ang'ania madaraka.

H.Rashid
rise: alijitengenezea jina kubwa sana kisiasa kiasi cha kuwa mwanasiasa nguli hapa Tanzania kwa hoja zake makini na kuhakikisha anatetea maslahi ya Tanzania na Z'bar. aliwahi kupinga srikali ya Amoor na baadae Karume, pia kiongozi mahiri wa upinzani Bungeni.
fall: toka chama chake kikose wabunge wengi kulinganisha na Chadema akaanza vitimbi kwa kujua kakosa ulaji, na sasa kapitisha hoja kidhalimu kuiadhibu chadema kwa kushirikiana na ccm, ni huzuni sana kwa mwanasiasa huyu.

L.Mrema
rise: alijitangaza na kujiimarisha kama mzalendo wa kweli Tanzania enzi zake akiwa waziri, na ni miongoni mwa watu wa mwanzo kupinga serikali dhalimu ya ccm, kagombea uraisi mara 3.
fall: baada ya kuhamia tlp toka nccr akaanza kuisha kisiasa, uchaguzi uliopita alimsusa mgombea wake na kuanza kumshabikia mgombea wa ccm wazi wazi ili apate msaada toka kwao, hakika kaishiwa kisiasa, sasa anashadadia chadema wagomvi kama vile yeye ni kada wa ccm.

Kafulila
rise: kijana mdogo aliyekuzwa na Chadema na akajiimarisha kwa mda mfupi
fall: toka alipofukuzwa chadema akaanza vita vya mamneno na sasa yupo kwenye anguko kwa kuwaopiga madongo.

Ngd zangu hawa wote rise na sasa ndio anguko lao limefika, hawana cha kukwepa wamefika saturation point, ni kama vile Roman Empire ilivyoanguka bila kutarajia au mnara wa Bableli ulivyoanguka na kwa marajio ya kuendelea kuwa juu.

wanadhani wanajinufaisha kumbe wanajiangamiza, wamesahau CCM ni zaidi ya nyoka mwenye vichwa 12 atawang'ata hata wenyewe na kuwaachia sumu wakishawatumia.

nawakilisha,
 
Hawa wote walishafall siku nyingi sasa hivi wanamalizikia tuu,wote ni viwavi jeshi,wote wana njaa kali,wote wanaugonjwa wa akili (UWAK) Upungufu wa akili Kichwani
 
ni kweli ndg yangu, sasa ndio wanamalizikia, ananiuma sana huyu kijana mdogo amabae hata hajakaa sana kwenye siasa sasa anaanguka na kufa vibaya kisiasa. i think hili ni bunge lake la kwanza na la mwisho labda abadilike
 
salaam wana jf,
hakika nimeshuhudia anguko kubwa sana kwa hao wazee na kijana mmoja katika siasa za tanzania. Mwanzoni wote walijijenga kama wanasiasa mahiri na wakombozi wa tanzania, lakini sasa wanaanguka na kupotea kabisa kama dola ya rumi au mnara wa babeli kwa matendo wanayoonyesha watanzania kwa uroho na ubinafisi wa kung'ang'ania madaraka.

h.rashid
rise: Alijitengenezea jina kubwa sana kisiasa kiasi cha kuwa mwanasiasa nguli hapa tanzania kwa hoja zake makini na kuhakikisha anatetea maslahi ya tanzania na z'bar. Aliwahi kupinga srikali ya amoor na baadae karume, pia kiongozi mahiri wa upinzani bungeni.
fall: Toka chama chake kikose wabunge wengi kulinganisha na chadema akaanza vitimbi kwa kujua kakosa ulaji, na sasa kapitisha hoja kidhalimu kuiadhibu chadema kwa kushirikiana na ccm, ni huzuni sana kwa mwanasiasa huyu.

l.mrema
rise: Alijitangaza na kujiimarisha kama mzalendo wa kweli tanzania enzi zake akiwa waziri, na ni miongoni mwa watu wa mwanzo kupinga serikali dhalimu ya ccm, kagombea uraisi mara 3.
fall: Baada ya kuhamia tlp toka nccr akaanza kuisha kisiasa, uchaguzi uliopita alimsusa mgombea wake na kuanza kumshabikia mgombea wa ccm wazi wazi ili apate msaada toka kwao, hakika kaishiwa kisiasa, sasa anashadadia chadema wagomvi kama vile yeye ni kada wa ccm.

kafulila
rise: kijana mdogo aliyekuzwa na chadema na akajiimarisha kwa mda mfupi
fall: Toka alipofukuzwa chadema akaanza vita vya mamneno na sasa yupo kwenye anguko kwa kuwaopiga madongo.

ngd zangu hawa wote rise na sasa ndio anguko lao limefika, hawana cha kukwepa wamefika saturation point, ni kama vile roman empire ilivyoanguka bila kutarajia au mnara wa bableli ulivyoanguka na kwa marajio ya kuendelea kuwa juu.

Wanadhani wanajinufaisha kumbe wanajiangamiza, wamesahau ccm ni zaidi ya nyoka mwenye vichwa 12 atawang'ata hata wenyewe na kuwaachia sumu wakishawatumia.

Nawakilisha,

dua la kuku halimpati mwewe.
 
They may be falling but they havent hit the ground yet.

Dont be suprised if they rise again.

Umesahau kutaja the Rise and Fall ya Mpendazoe.
 
Kafulila might think that he is special than the Tanzanians who wanted CHADEMA to govern the country. Im sure even Zito regrets supporting him during election 2010. I take him like CCM puppet. Alifurahia makofi ya mjengoni. Asubiri kuzomewa mtaani. Mtoto wa Makinda na Makamba. Just thinking
 
Kila mtu ana mwanzo na mwisho wake. wenyewe wanasema kutesa kwa zamu. hata Obama atshuka tuu, hilo si ajabu kwani hujui ngoma ivumayo sana haidumu? Ila kwangu mimi Kafulila ndo wakati wake anawika..
 
Salaam wana JF,
hakika nimeshuhudia anguko kubwa sana kwa hao wazee na kijana mmoja katika siasa za Tanzania. mwanzoni wote walijijenga kama wanasiasa mahiri na wakombozi wa Tanzania, lakini sasa wanaanguka na kupotea kabisa kama dola ya Rumi au Mnara wa babeli kwa matendo wanayoonyesha watanzania kwa uroho na ubinafisi wa kung'ang'ania madaraka.

H.Rashid
rise: alijitengenezea jina kubwa sana kisiasa kiasi cha kuwa mwanasiasa nguli hapa Tanzania kwa hoja zake makini na kuhakikisha anatetea maslahi ya Tanzania na Z'bar. aliwahi kupinga srikali ya Amoor na baadae Karume, pia kiongozi mahiri wa upinzani Bungeni.
fall: toka chama chake kikose wabunge wengi kulinganisha na Chadema akaanza vitimbi kwa kujua kakosa ulaji, na sasa kapitisha hoja kidhalimu kuiadhibu chadema kwa kushirikiana na ccm, ni huzuni sana kwa mwanasiasa huyu.

L.Mrema
rise: alijitangaza na kujiimarisha kama mzalendo wa kweli Tanzania enzi zake akiwa waziri, na ni miongoni mwa watu wa mwanzo kupinga serikali dhalimu ya ccm, kagombea uraisi mara 3.
fall: baada ya kuhamia tlp toka nccr akaanza kuisha kisiasa, uchaguzi uliopita alimsusa mgombea wake na kuanza kumshabikia mgombea wa ccm wazi wazi ili apate msaada toka kwao, hakika kaishiwa kisiasa, sasa anashadadia chadema wagomvi kama vile yeye ni kada wa ccm.

Kafulila
rise: kijana mdogo aliyekuzwa na Chadema na akajiimarisha kwa mda mfupi
fall: toka alipofukuzwa chadema akaanza vita vya mamneno na sasa yupo kwenye anguko kwa kuwaopiga madongo.

Ngd zangu hawa wote rise na sasa ndio anguko lao limefika, hawana cha kukwepa wamefika saturation point, ni kama vile Roman Empire ilivyoanguka bila kutarajia au mnara wa Bableli ulivyoanguka na kwa marajio ya kuendelea kuwa juu.

wanadhani wanajinufaisha kumbe wanajiangamiza, wamesahau CCM ni zaidi ya nyoka mwenye vichwa 12 atawang'ata hata wenyewe na kuwaachia sumu wakishawatumia.

nawakilisha,

Heshima kwako King Seleman [Solomon]

Mkuu analysis yako haina mashiko hata kidogo,pengine ungejaribu kutumia mifano mingine labda ungefanikiwa kidogo.

Hamad Rashid bado ni kiongozi mahiri na atakumbukwa kwa ushupavu kama KUB katika bunge la 9 kwa kuwaunganisha wapinzani wote bila kuwabania chini ya uongozi wake mahiri Dr W Slaa,Zitto Kabwe nyota zao zilichomoza vizuri katika anaga za siasa za Tanzania.Mheshimiwa Mheshimiwa Hamad Rashid bado ameweza kupenyeza hoja ya kutambuliwa wapinzani amabo hawako kwenye kambi rasmi ya upinzani Bungeni baada ya CHADEMA kuwatenga.Upo uwezekano mkubwa chini ya uongozi wake wabunge toka vyama vya CUF,NCCR,TLP na UDP kuongoza kamati muhimu za PAC,LAC na POC.Inategemewa unamwangalia Mheshimiwa Hamad Rashid katika darubini gani lakini tukitumia vigezo vya kawaida Hamad Rashid anazidi kupaaa kisiasa.

Mheshimiwa A L Mrema ni mwenyekiti wa TLP aliwahi kushika madaraka makubwa kuanzia uwaziri hadi naibu waziri mkuu.Amegombea mara tatu nafasi ya urais wa JMT na kushindwa mara zote.Mwaka 2010 aligombea ubunge akashinda laiti angebaini mapema kwamba kushinda urais ni jambo linalohitaji mtandao mkubwa wa chama angeachana na mpango wake siku nyingi.Kama kugombea urais na kushindwa ni kigezo cha kushuka kisiasa Mrema hata kuwa mwenyewe wapo wanasiasa wengi ambao baada ya kushindwa urais walirejea kugombea ubunge Mheshimiwa Mbowe ni mfano hai.

Kafulila ni kijana mdogo ambae stahili ya cheo chake unaanza na neno mheshimiwa kama kutofautiana na CHADEMA ni kushuka/kuporomoka kisiasa itabidi kamusi/dictionary zirejeshwe kwa wachapaji ili maana ya kuporomoka ipanuliwe na kupatiwa maana zaidi.

Mkuu king Solomon ukitoka ndani ya mabox ya vyama utabaini unaowaona wameanguka kisiasa wanapeta na usishangae wakaanguka unaodhani watasimama.
 
Kwa maoni yangu Mrema na Cheyo walishafulia siku nyingi, Hamad Rashid ndo anaanguka huku akiwa amefungwa minyororo na ccm, Kushuka kwake pia kunatokana na CUF kushuka umaarufu bara hasa baada ya CUF kuungana na CCM Zanzibar. Amebadili personality kutoka ustaarabu hadi mipasho na ushabiki.

Ni vigumu kumtabiri Kafulila, bado mchanga katika siasa za kitaifa, kwake yeye kutofautiana na chadema hakujaanza leo, ni mwendelezo tu.Haijulikanai kama kweli ni mtiifu kwa cuf au ccm.
 
heshima kwako ndg Ngongo,
nfurahi kwa analysis yako uliyoitoa, ila na wewe ukiangalia ukweli utabaini kwamba H.Rashidi unaemzungumzia sasa sio yeye wa miaka ya nyuma hasa bunge la tisa, HR wa sasa ni mlafi wa madaraka na mpenda vyeo aliyekithiri. angalia toka walipozidiwa na Chadema utagundua mabadilko makubwa kwake. kama kweli yeye ni mwanasiasa mahiri bado kwa nini asiwike bila kung'ang'nia vyeo vya wenzake wenye haki kikanuni? kwanini ashadadie kubadili kanuni sasa na sio kipindi chake? kwa sasa anaanguka belive me or not.

kwa Mrema ndg yangu ndio lipo wazi kabisa, umejarubu kumtetea kwa hoja dhaifu sana yeye tayari kesha anguka zamani sana, hakika ka upata ubunge kwa msaada wa ccm ili kumlipa fadhila kwa kuwasaport, kwa sasa hana impact yoyote kwenye siasa za tanzania, Mrema huyu sio yule wa miaka ya tisini( 90s).

kwa Kafulila nakubaliana nawe kdg, lakini ndg yangu kunma umuhimu wowote wa yeye kuwatupia madongo waliomkuza? ni kweli yupo juu, ila anguko lake ni karibu sana kwa mwenendo wake,

ccm ndg yangu sio wa kushirikiana nao ni zaidi ya ndumilakuwili, watawageuka muda si mrefu hao vibaraka wao wapya HR, K, na Mrema. time w'll tell ndg yangu.

huo ndio mchango wangu kwa hoja yako, nitafurahi tukizidi kuelimishana
 
Heshima kwako King Solomon,

Mkuu kabla ya kutoa hukumu kwa mheshimiwa Rashid Hamad unatakiwa kwanza kuangalia chama chake kina nafasi gani kipindi hiki.Bunge la tisa CUF walikuwa na wabunge wengi,bunge la kumi CHADEMA wana wabunge wengi.Majukumu ya sasa ya mheshimiwa Rashid Hamad ni tofauti na majukumu aliyokuwa nayo kipindi kilichopita.Mheshimiwa Rashid Hamad pamoja na kukosa uongozi lakini bado ameweza kufanikisha wabunge wa vyama vya upinzani waliowekwa kando na CHADEMA kupata nafasi ya kugombea uongozi wa kamati za POC,PAC na LAC.Mkuu wangu mtu anayeweza kufanya mambo yote haya bado unamweka kwenye kundi la kuanguka !.

Mheshimiwa A L Mrema unasema nimejaribu kumtetea lakini tayari kesha "anguka zamani sana,kwamba kaupata ubunge kwa msaada wa CCM".Mkuu ninavyojua mimi CCM walimsimamisha mgombea wao akashindwa ,CHADEMA pia wamsimamisha mgombea wao akashindwa.Naomba unijibu kwanini CHADEMA hawakuitumia nafasi ya kushinda huko Vunjo kwakuwa Mhe Mrema amekwisha ?.Taarifa nilizozipata muda huu ni kwamba Mheshimiwa Mrema ni Mwenyekiti LAC.

Mheshimiwa Kafulila umekiri unakubaliana na mimi kidogo lakini hap hapo umeshindwa kuonyesha sababu za kutokubaliana na mimi sana.
 
ndg yangu Ngong, nashukuru sana kwa majibu yako mazuri, nilisema nakubaliana na wewe kuhusu Kafulila kwa sababu he is too young na bado anang'ara kwenye siasa za Bongo, though nasikitishwa na siasa zake za majungu na ninahofu ataanguka mapema.

mkuu N' yaani kuhusu Mrema naendelea na msimamo wangu, yeye ameshajiishia anajaribu tu kumaliza vizuri. Umesahau Mrema alialikwa na ccm kwenye kikao chao akawasifia ccm sana, huyu ni mpinzani???

HR kwa sasa mkuu simuamini hata kdg, yeye lengo lake limetimia kwani nia yake ni kuikomoa Chadema kwa kukosa nguvu kamili ya upinzani peke yao bila kushirikisha wengine. Ana wivu wa kisiasa.

nakuhakikishia Cheyo na Mrema kwa post walizopewa hawatakuwa na jeuri hata kdg kuihoji serikali ya ccm
 
Mkuu A L Mrema kualikwa kwenye vikao vya CCM na kuwasifia si hoja mbona Zitto naibu katibu mkuu wa CHADEMA alimpigia chapuo Kikwete.Juzi juzi tulishuhudia Mwenyekiti wa CHADEMA wakipeana mkono kwa furaha na Rais Kikwete kwanini husemi Mbowe si mpinzani au kajiishia ?.

Mheshimiwa Hamad Rashid ni mbunge kupitia chama cha CUF haitaji kuaminiwa na wewe ili awe shujaa,maadamu chama chake na wapiga kura wake wamemwamini ataendelea kufanya na kutenda aliyotumwa na chama chake ndiyo maana mpaka sasa bado yuko mjengoni akitanua kwa kodi zetu.

Mheshimiwa Kafulila aligombea ubunge kupitia CHADEMA mwaka 2005 akashindwa,mwaka 2010 akagombea ubunge kupitia NCCR akawashinda wagombea wa CCM na CHADEMA .
 
Kwa maoni yangu Mrema na Cheyo walishafulia siku nyingi, Hamad Rashid ndo anaanguka huku akiwa amefungwa minyororo na ccm, Kushuka kwake pia kunatokana na CUF kushuka umaarufu bara hasa baada ya CUF kuungana na CCM Zanzibar. Amebadili personality kutoka ustaarabu hadi mipasho na ushabiki.

Ni vigumu kumtabiri Kafulila, bado mchanga katika siasa za kitaifa, kwake yeye kutofautiana na chadema hakujaanza leo, ni mwendelezo tu.Haijulikanai kama kweli ni mtiifu kwa cuf au ccm.

Kwa kujinasibu na ccm ambayo inakata tawi la mti huku imelikalia, anguko ni dhahiri, kwa kushindwa kutambua kuwa kwenye uchaguzi wapiga kura wake waliitosa ccm na kumpa yeye kura, hatubahatishi kafulila kwisha habari yake, ujifunze kwa zito.
 
MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!

22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
 
Back
Top Bottom