jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Mkuu jmushi1,
1.Tukianza na mapambano dhidi ya ufisadi, hebu nitajie kimojawapo tu ya mafanikio ya Augostine Lyatonga Mrema.
2. Tukirudi kwenye harakati za mageuzi nitajie angalau moja alilolifanya A. L. Mrema kufanikisha hayo mageuzi.
Mimi nimesema nina makovu ya marungu ya polisi dhidi ya wanamageuzi kati ya 1991 mpaka 1994 wakiongozwa na Mrema. Wakati Mrema anadandia hiyo meli, mageuzi yalishapatikana na vyama vya kumsetiri asibaki uchi alipoihama CCM vilishakuwapo. Na hapa naomba usiingize ukabila kwa sababu ni njia ya kukosa hoja.
Alipokuwa mbunge alipigania maslahi ya wanyonge na pia mazao ya biashara kama kahawa nk.
Alipokuwa waziri wa mambo ya ndani pia alisolve matatizo mengi sana ya ujambazi na kwa kweli majambazi walijuwa Mrema si wa kuchezewa.
Issue za mirathi, haki za wanawake nk. Alishapata pia kuwa waziri wa vijana kama sijakosea...Naomba kuwa corrected.
Alikuwa akisimamisha shilingi kila mara ilipobidi na hakuwa na damu ya kifisadi hilo lilimfanya kuonekana mwana ccm wa tofauti sana na ndio maana hata akapewa uwaziri na mwinyi.
Wapi nimeingiza ukabila na wapi nimekosa hoja?