Crucifix
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 1,651
- 588
Hawa jamaa ninawafananisha kama Medvedev na Putin wa Russia ambao wanatawala tangu miaka ileee kwa kupishana urais na uwaziri mkuu. Ni wazi Mkapa hawezi kuwa waziri mkuu wa Tz lakini ujio wao na ushawishi waliionesha katika vikao vya NEC, kuna dalili jamaa wamejipanga kurejea (au pengine wanashiriki) katika medani za siasa kitu kinacheweza kumweka Sumaye katika ukuu wa nchi na Mkapa akiwa mshauri mkuu endapo jitihada za Lowassa kujisafisha zikishindikana. Swali alilouliza Sumaye juu ya kuchafuliwa Lowassa halikuwa na nia ya kumtetea Lowassa bali kuibua mambo zaidi ili kambi ya Lowassa na ile inayompinga zote zipoteze mvuto katika jamii. Na mbinu hii ikifanikiwa, basi CCM hawatahitaji kuendelea na marafiki wa JK bali watarudi nyuma kuanzia pale Mkapa alipoishia na itakuwa ni return ya Mkapa-Sumaye Era.