Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #41
Nilitaka kuonyesha tu ni njisi gani sisi wote ni wezi tu na ndiyo maana nivigumu sana kukemeana. Ukianza tu kukemea roho inakusuta inakuambia kuwa hebu piga matumizi yako ya mwezi halafu toa kipato chako halafu nieleze hii difference umetoa wapi. Of course watu walio wengi wanapenda kuishi maisha ya haki na wanajikuta tu wameingia kwenye hii circle ya ufisadi kwa mazingira. Hebu fikiria fedha kiduchu halafu kuna hawa wenzetu wenye fedha basi utaona wanakopesha kwa Riba ukikopa laki mbili basi mwisho wa mwezi unaripa 240,000.
Kwa sasa ni mafisadi tu ndiyo wanaofaidi maana ukiwa na cash kidogo tu basi inaongezeka kwani raia ni choka mbaya
Shalom, mwishoni mwa mwaka jana niliandika makala moja ambayo nilisema kuwa wakazi wa Dar ndio wanufaika wakubwa wa ufisadi; nilichomaanisha ni kama hicho ulichosema; kwamba watu wa mjini wameweza na wanaweza kuishi katika mazingira ya kifisadi kwa sababu wao wenyewe vile vile wananufaika na ufisadi huo. Hii inafafanua ni kwanini upinzani hauwezi kushinda katika miji ya Tanzania kiurahisi, isipokuwa pale ambapo watu hawanufaiki sana na ufisadi huo.