Birds of a feather flock together! Chenge na Hosea ni wale wale
Kuna kitu kimoja ambacho magazeti hasa Thisday na Kulikoni wanakipotosha kuhusu uchunguzi wa Rada na kuwapa wananchi matumaini hewa. Mtakumbuka katika tume ya NEC inayoongozwa na Rais mstaafu Mwinyi wakati wa majibishano Waziri wa Utawala Bora Mama Sophia Simba alinukuliwa akisema kwamba SFO walishaandikia serikali kwamba vile vijisenti vya Chenge kule New Jersey, Uingereza havikutokana na ufisadi wa Rada labda na vyamzo vingine. Kwa maana hiyo Chenge sio "interest" tena kwa wachunguzi wa SFO.
Mtu amabaye alipewa rushwa ni Gaileshi na ndio maana alitoroka hapa nchini. Bila Gaileshi kupatikana na kusema alimpgawia nani ni kazi bure. Sijui kwa nini vyombo vya habari vinapotosha habari hii. Bila Gaileshi kupatikana kina Chenge na wenzake watatesa na vijisenti vyao mpaka liamba. Vyombo vya habari visitupe matumaini hewa kama kwenye kesi ya Zombe