The Radar Scam: Chenge & Rashid...

kwa kweli wakati mwingine nashindwa kupima kwenye mizani mabaya na mazuri ya nkapa, mwishowe naishia kuangalia tu kwa macho. Yaani madudu mengi yalianzia wakati anamaliza muda wake pale ikulu. Cha ajabu aliyemfuata naye hakuchelewa, fasta akaanza na yake...........hatujui atakayekuja atakuwa na deal gani.
 
na hiyo ndo kitu ambayo ******, pengine na watakaomfuata, ameshindwa kuelewa, kwamba katu watu hawatakaa kimya hadi haki itakapotendeka kwa wahusika kufikishwa mahakamani ndo watu watakaa kimya.........
 
Wakuu,chenji ya rada imerudi,lkn cha ajabu watuhumi wa hawajadiliwi,hivi wana JF waizi wetu ni nani ktk gumashi la rada?
 
Nadhani wanafahamika sana tu ila tulishaambiwa kwamba wanatakiwa kuachwa wapumzike!!
 
Na hiyo change inakwenda wapi?

Nakumbuka kuna kipindi bwana Membe aliisemea sana hiyo!
 
Brother Mwanakijiji, usiumize kichwa bure! FELESHI KAMWE HAWEZI KUMSHITAKI CHENGE, ANALIPA FADHILA! Hata akilazimishwa yuko tayari kujiuzulu alimradi mzee wake hasimamishwi kizimbani!

Eliezer Feleshi amevunja rekodi kuwa DPP wa kwanza, si Tanzania tu bali Afrika ya Mashariki, kushika wadhifa huo mkubwa akiwa na umri mdogo chini ya miaka 40 na akiwa na uzoefu mdogo katika uongozi na katika taaluma ya sheria. Uteuzi wake uliacha vinywa wazi miongoni mwa wanasheria wote nchini maana Feleshi hana sifa ya pekee kuweza kuwaruka mawakili waandamizi lukuki walio katika wizara ya sheria. Aliyewezesha yote haya kufanyika si mwingine ni Andrew Chenge. Alijua alichokuwa anafanya: alikuwa anawekeza kwa kijana mdogo, Msukuma mwenzake na ndugu yake kiukoo akijua kuwa siku moja atasimama kidete kulipa fadhila kwake! Sasa yanaonekana: faili la Chenge litazungushwa wee mpaka Waswahili msahau kuhusu majambo ya mzee wa vijisenti.

Ndiyo maana nasema, Mzee Mwanakijiji achana na hoja nzito unazotaka kuingiza kwenye suala hili: hapa hakuna jurisprudence ni WIZI MTUPU!!!
Chenge ni mwanasheria na ali exploit hilo, watu walikuwa hawajui nguvu ya DPP?Yule hana haja ya kutoa sababu akifuta kesi.Na Chenge kwa kutumia uelewa wake, karata yake aliyopewa kwenye mtandao ya ku call a shot baada ya ushindi wa JK ili kupigiana mapande ya fadhila, aliitumia kupachika mtu wake sehemu nyeti, ndo bongo hiyo.
 
SKENDO YA RADA NA BAE SYSTEMS. CHENGE ALIHUSIKA KUFACILITATE TRANSACTION NA KULIPWA 1.5 MILLIONS USD DOLLERS. ALIPEWA RUSHWA KUWEZESHA MANUNUZI. USD 12 million ALILIPWA Shailesh Vithilan, BAE’s former marketing adviser based in Dar Es Salaam. SASA NA USHAHIDI WOTE HUU KWA NINI CHENGE HAYUO JELA WALA HAFILISIWI? MH. JAKAYA KIKWETE NATUMAINI UNALIONA HILI NA LIFANYIE KAZI IMMEDIATELY.

VYANZO; Tanzania: Ten Year BAE Systems Aviation Radar Purchase scandal that just won https://www.facebook.com/chademadiaspora https://www.facebook.com/chademadiaspora


View attachment 57536
 
Kumbe habari zenyewe zinatoka chadema? kwi kwi kwi teh teh teh.

Vipi Simbachawene, jeraha la kukatwa na mapanga limepona kwa madakika tu?
 
Jamani msimtafute ubaya rais wetu dhaifu, hana ubavu wa kumshughulikia Chenge kwani akijaribu tu Chenge naye atamwaga mboga kwa kueleza mgao wa mkulu katika hili dili.
 
Wadau wa JF natumaini ni wazima poleni na mapumuziko ya weekend!

Lipo jambo nyeti linanikera sijui wenzangu mnaliona kivipi???

Serikali yetu ya Tanzania imeamua kuweka pamba kwenye masikio kwenye jambo lililo nyeti kwa maendeleo ya taifa letu!!! Zililetwa taarifa za rushwa ya RADA serikali akakaa kimya hadi Waingeraza kwa aibu ya vyombo vyake kushiriki kwenye rushwa hiyo ya RADA wakaleta fedha za fidia waziri mhusika akachekelea kuwa wameleta fedha serikalini, wahusika kwa upande wa TZ hawajachukuliwa hatua yoyote!!! Mpaka mtu mmoja akaleta kitabu chenye kuonyesha mkakati mzima wa ngawanyo wa hiyo rushwa hiyo serikali yetu tunayo itegemea kimyaaaa!

Zikaja taarifa za fedha zimefichwa huko SA Matrilion lakini hakuna hatua iliyotajwa kuchukuliwa kurudisha hizo fedha na kuchulia wahusika hatua!!! Zikaletwa taarifa za fedha zilizofichwa huko USWISS Mabilon ya dola hakuna linlosemwa na serikali ni kimyaaa!!!! Juzi mbunge wetu amejitolea kuleta taarifa za fedha zilizo hamishwa kwenda nje ya nchi mabilon ya dola sijui kama kuna hatua yoyote inachukuliwa kiuwazi!!! Does it mean Tanzania we accept and tolerate corruption as a normal system of life, business as usual?

Sasa tunadai kuwa hakuna fedha za kulipa walimu, madaktari, kujenga miradi mikubwa ya mabwawa ya maji ya mitambo ya umeme, kujenga reli, fedha zetu zimelala kwenye mabenki nje ya nchi!

Naomba tafadhari tujadili hili hivi kweli tumeridhika?
 
Ndugu, waliokwapua pesa hizo na kuzipeleka huko ndio hao hao tunaowategemea wachukue hatua ya kuzirudisha. Hapo ni sawa na kuchukua kesi ya nyani unampelekea ngedere.

Kama kweli tunataka pesa zirudi sisi sote tuchukue hatua ya kuwalazimisha, sio kuwaomba wazirudishe.

Na tutakapokuwa tayari kufanya hivyo, tusiende kuomba kibali kwa polisisiem.

kama hutuko tayari kufanya hivyo basi tuendelee kuugulia machungu.
 
Ndugu utaumia bure na uchungu wa nchi hii watu walishachoka maendeleo ya jumla(nchi) wanaangalia binafsi zaidi. Na kwa hao mafisadi wanaitwa WAJANJA WACHACHE kama vile mwizi ni mjanja badala ya kuwaita wajinga na majizi. Inauma sana tena sana ndugu zangu wazalendo.
 
Ndugu utaumia bure na uchungu wa nchi hii watu walishachoka maendeleo ya jumla(nchi) wanaangalia binafsi zaidi. Na kwa hao mafisadi wanaitwa WAJANJA WACHACHE kama vile mwizi ni mjanja badala ya kuwaita wajinga na majizi. Inauma sana tena sana ndugu zangu wazalendo.
Ndugu yangu nashangaa hata wabunge wanazungumza kwa jaziba kama kweli wako serious lakini mbona hakuna wa kuleta mswada bungeni wa kuomba fedha zetu zilizo kwapuliwa zirudishwe????

 
Serikali imewekwa pamba masikioni, serikali legele haina nguvu ya kujiweka pamba masikioni
 
Back
Top Bottom