The New Dr Shein's Cabinet

Zanzibar hakuna sera za kulindana wala za urafiki kama wa KJ huko bara. Wizara zimegawanywa karibu sawa sawa kati ya wapinzani na CCM. Hapo ndio mwisho wa upinzani visiwani.Ukiangalia kwa makini, zile wizara zilizokuwa zikisumbuliwa sana na wapinzani CUF sasa wamepewa
wao kazi kwao waonyeshe njia siyo kuwa wapiga debe tu. safi sana TZ bara wanatakiwa kuiga mfano huu.
 
Jamani Vuai Nahodha kulikoni? Ana bifu gani na Shein? Mbona mimi nilikuwa namuona kuwa ni mtendaji makini sana? Au Shein naye ni mtu wa visasi?

Ukiona hivyo subiri kwenye baraza la mawaziri la Muungano...
 
Dr Shein Kamtupa Vuai kama Karume alivyomtosa Bilal, anyway, ndiyo mambo ya siasa. Hivi mawaziri gani waliokuwa kwa Karume ambao Shein kawarudisha kwenye serikali yake?
 
Usawa wa jinsia sio sera ya ccm.lile lilikua zengwe tuu la kumng'oa sita uspika wa ccm!
 
Ni nzuri only that Zanzibar bado wako kwenye Mono party system of government b'ze apart from using party names and flags, the difference is the same!
 
Hivi majukumu ya Waziri asiye na wizara maalum ni nini? Mawaziri 3, hawana wizara maalum, hatujui wanafanya nini na bado wanaendelea kulipwa kwa kazi ambazo hazijulikani?

Takwimu zangu zinaonyesha kwamba Mifugo ni sekta ndogo sana Zanzibar. Kwa hiyo kuna wizara 2 ambazo zinaweza kuunganishwa na bado kusiwe na tatizo kiungozi. Wizara ya Kilimo na Maliasili ingeunganishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Bado Baraza la Mawaziri ni kubwa. Nilitarajia kwamba Jussa angekuwa mmoja wa mawaziri, naona imekula kwake.

kweli,baraza hilo ni kubwa sana kwa Zanzibar.Nafkiri still hatuna mikakati ya kuleta maendeleo. Just tuna tengeneza ajira tu. Nchi kama Ufaransa ina mawaziri 6 tu.Leo zanzibar ya wapiga kura laki nne ina wabunge zaidi ya 50 nafkiri, wawakilishi kibao, mawaziri 16..........hadi mifugo imeundiwa wizara zanzibar???? Bado tuna kazi ya kutafuta mbinu sahihi za kuiendeleza hii nchi.:peep:
 
hivi hawa mbona hawataji waziri kiongozi au ni yule yule Vuai

Nafasi ya Waziri Kiongozi ilifutwa baada ya mabadiliko ya juzi ya Katiba ya Zanzibar ambayo yameleta nafasi za Makamu wa Kwanza wa Rais na nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Makamu wa Pili wa Rais ndio anajaza nafasi ya Waziri Kiongozi. Kwa maneno mengine Balozi Seif Ali Idd ndo atakuwa kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni.

Ajabu ni kwamba nimemuona akila kiapo cha Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa sijui atahudhuria vipi Bunge na Baraza la Wawakilishi na huku bado ana majukumu makubwa ya kuongoza serikali.
 
hao mawaziri wasio na wizara maalum ni wa nini. why why why?
Dr. Shein tafadhali acha kuwa na baraza kubwa bila ulazima wowote!!! usiwaapishe haon hao wateule wasio na wizara maalum.
 
watu mil 1: mawaziri 22 ---->(zenji)
watu mil 45: ? mawazirim ----> (bara)

soln: bara tunahitaji mawaziri 45*22= 990
hii nikuweka usawa kati ya bara na visiwani
 
Du! Wengine wanabana matumizi wengine ndo wanaongeza upana wa serikali!yaani makamu wa raisi wawili na mawaziri wasiokuwa na wizara maalum wa 3 wa nini wote hoa na kwa ukubwa upi wa nchi ya zanzibar??nonesense nilijua dr angekuja na serikali ndogo effective ila naona ndo wale wale!zanziba lazima walale njaa kuhudumia serikali
 
Kwanza sio sahihi kwamba baraza la SMZ lina mawaziri 16. Nimesoma list yote nimekuta namba 5 kuna mawaziri 2, mmoja wa Makamu wa Kwanza wa Rais na mwingine wa Makamu wa Pili wa Rais na wote ni mawaziri kamili.

Namba 16 kuna mawaziri 3, ambao ni wasiokuwa na wizara maalum. Hii title ni ya siku nyingi sana na ilikuwa imepotea, naona imeibuka tena.

Hivi majukumu ya Waziri asiye na wizara maalum ni nini? Mawaziri 3, hawana wizara maalum, hatujui wanafanya nini na bado wanaendelea kulipwa kwa kazi ambazo hazijulikani?

Takwimu zangu zinaonyesha kwamba Mifugo ni sekta ndogo sana Zanzibar. Kwa hiyo kuna wizara 2 ambazo zinaweza kuunganishwa na bado kusiwe na tatizo kiungozi. Wizara ya Kilimo na Maliasili ingeunganishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Bado Baraza la Mawaziri ni kubwa. Nilitarajia kwamba Jussa angekuwa mmoja wa mawaziri, naona imekula kwake.

Ni kweli Baraza ni kubwa sana nchi yenyewe ina watu milioni moja sasa na eneo dogo hivyo ungetegemea kuwa na Baraza dogo, linalonyumbuka na hodari. Lakini mfumo wa kupeana vyeo unaendelea mtindo mmoja. Wawakilishi kibao, wabunge kibao, Raisi na Makamu wake wawili. Hapo hujazungumzia Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi wa Idara mbalimbali za serikali. Si ajabu kuwa utafiti wa kina ukifanywa utakuta kuwa kama asilimia moja na nusu ni viongozi. Je, fedha za kuwalipa mishahara zipo? Je, fedha za miradi ya kweli ya maendeleo zipo? Kwa wanasiasa wote wa bara na visiwani ni ule msemo ambao mwaka 1978 uliimbwa kabla ya kupigwa marufuku "Ponda Mali Kufa Kwaja."
 
Sera za Chadema za serikali ndogo sasa yaelekea CCM wamezivalia njuga na yeye Dr. Shein leo ITV wametuhabarisha kaunda serikali ndogo ya mawaziri 16................7 kutoka CUF na 9 kutoka CCM na manaibu wao 6..........................

Sikulisikia jina la waziri kiongozi wa zamani............nafikiri panga la kugombea uraisi na kuuokosa limempitia.................

Mkuu,

Wakati mwingine ni bora kufanya uchunguzi kwanza kabla ya kuanzisha thread.

Serikali iliyopita ilikuwa ndogo zaidi kuliko hii ya Dr. Shein, ilikuwa na wizara 13 tu.
 
Baraza ni kubwa sana, lakini kwa kuwa ndio limeshaundwa, tufanye nini? Labda tusubiri baada ya miaka miwili hivi atapolipangua, . Kwa mfano:
1. Hakuna sababu ya kuweka mawaziri watatu wasiokuwa na wizara maalumu. Kazi yao nini zaidi ya kututwisha mzigo walipa kodi?
2. Nini kazi zamawaziri wawili wa Makamo wa Kwanza na Makamo wa Pili?
2. Wizara za Kilimo na Maliasili, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko zilipaswa kuwa wzara moja, hasa tukitilia maanani kuwa ZNZ hatuna viwanda.
3. Wizara za Kazi…na Utumishi bora zilipaswa kuwa moja.
Mpaka hapa tu kuna wizara 9 hazina mpango wowote, zimezidi. Hata mawaziri wanane wangelikuwa wengi. Nahisi ile ahadi ya Dk. Shein kutaka kuujenga uchumi wa Zanzibar imeanza kufunikwa na kiwingu.
Lini Watanzania tutajinasua na "kutaka kuridhishana?" NI AIBU, AIBU, AIBU.

.
 
1. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-
Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame
2. Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo)
Mhe. Omar Yussuf Mzee
3. Ofisi ya Rais, (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
Mhe. Haji Omar Kheri
4. Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji.
5. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mhe. Mohammed Aboud Mohammed
6. Wizara ya Katiba na Sheria
Mhe. Aboubakar Khamis Bakary.
7. Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
Mhe. Hamad Masoud Hamad
8. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban
9. Wizara ya Afya
Mhe. Juma Duni Haji
10. Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto
Mhe. Zainab Omar Mohammed
11. Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo
Mhe. Abdilahi Jihad Hassan
12. Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati-
Mhe. Ali Juma Shamhuna
13. Wizara ya Kilimo na Maliasili
Mhe. Mansoor Yussuf Himid
14. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko
Mhe. Nassor Ahmed Mazrui
15. Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Mhe. Said Ali Mbarouk
16. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika
Mhe. Haroun Ali Suleiman
17. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum
Mhe. Suleiman Othman Nyanga
18. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum
Mhe. Haji Faki Shaali
19. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum
Mhe. Machano Othman Said
Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein ameteua Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:
1. Naibu Waziri, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
Mhe. Issa Haji Ussi
2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Mhe. Zahra Ali Hamad
3. Naibu Waziri, Wizara ya Afya
Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya
4. Naibu Waziri, Wizra ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo,
Mhe. Bihindi Hamad Khamis
5. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati
Mhe. Haji Mwadini Makame
6. Naibu Waziri, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko,
Mhe. Thuwaiba Edington Kissasi
Waheshimiwa wote waliotajwa wanatarajiwa kuapishwa hapo kesho jioni katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
Naomba kuwasilisha
Salma Said
 
Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42 (1) na (2), 43 (1) na (2) na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Wizara 16 na kuwateua Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-
Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame

2. Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo)
Mhe. Omar Yussuf Mzee

3. Ofisi ya Rais, (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
Mhe. Haji Omar Kheri

4. Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji.

5. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mhe. Mohammed Aboud Mohammed

6. Wizara ya Katiba na Sheria

Mhe. Aboubakar Khamis Bakary.

7. Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Hamad Masoud Hamad

8. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban

9. Wizara ya Afya

Mhe. Juma Duni Haji

10. Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto

Mhe. Zainab Omar Mohammed

11. Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo

Mhe. Abdilahi Jihad Hassan

12. Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati-

Mhe. Ali Juma Shamhuna

13. Wizara ya Kilimo na Maliasili

Mhe. Mansoor Yussuf Himid

14. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

Mhe. Nassor Ahmed Mazrui

15. Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Mhe. Said Ali Mbarouk

16. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika

Mhe. Haroun Ali Suleiman

17. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Suleiman Othman Nyanga

18. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Haji Faki Shaali

19. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Machano Othman Said

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein ameteua Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Naibu Waziri, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Issa Haji Ussi

2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Zahra Ali Hamad

3. Naibu Waziri, Wizara ya Afya

Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya

4. Naibu Waziri, Wizra ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo,

Mhe. Bihindi Hamad Khamis

5. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati

Mhe. Haji Mwadini Makame

6. Naibu Waziri, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko,

Mhe. Thuwaiba Edington Kissasi

Waheshimiwa wote waliotajwa wanatarajiwa kuapishwa hapo kesho jioni katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
Naomba kuwasilisha.
 
Huu msururu wa mawaziri wasio na wizara maalum ni kwa ajili gani? Huu ni uchakachuaji wa mali ya umma.
 
Back
Top Bottom