jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Kitila,
Could it be possible kwamba hata JF sasa inaelekea huko huko. Maanake baada ya kupitia post zingine humu ndani nabaki tu kinywa wazi. Ni kweli kuna mawazo yanatolewa yenye nguvu ya hoja, lakini ukurupukaji unaanza kutawala mijadala na hii inaanza kunitia hofu. Kuna watu ama hawasomi na kuelewa kinachoendelea au kwa makusudi mazima wanaleta upotoshwaji wa mada. Mimi sikushiriki kabisa kwenye mjadala wa sakata la unga bungeni kwa sababu mantiki yake haikuweza kuniingia akilini, la hasha. Lakini wako wengi wasiotambua kuwa kunyamazia jambo usilolielewa kimsingi ni bora kuliko kurukia bila mpangilio halafu unabaki unaonekana ama juha au mwehu.
Kuna hoja zimejificha na inabidi uzisome mara mbili kama wewe ni mzito kiakili kama mimi, kabla hujakurupuka. Ninao rafiki zangu wengi wanaosoma JF na hivi sasa wanasononeka na kiwango cha majadiliano humu ndani. Mambo mazito hayashupaliwi kama ilivyo kwa mambo yasiyo na umuhimu wowote. Ukipitia humu ndani utakuta tulivyo wepesi katika kuchangia mada za ovyo. Hali hii inatisha.
Mada hii si ya HOVYO LABDA WEWE NDIYO HOVYO!
NA WEWE NDIO UMEKURUPUKA!
Kama umekiri HUKUFUATILIA MJADALA WA UNGA UNGA TOKA MWANZO THEN KAA KIMYA NA USOME MJADALA UNAVYOKWENDA NA SI KUJA NI VIJIMANENO VYA KUJIDAI WEWE UNA BUSARA!
Watu wanauliza maswali kutokana na KAULI ZILIZOWAHI KUTOLEWA NA PANDE ZOTE..IWE YA KUMTETEA CHENGE AMA SPIKA.
Kweli UNATISHA!