The Legacy of Kingunge Ngombare Mwiru

katika mazingira ambayo wewe hutaki kujadili watu, unachotakiwa kufanya ni kwenda thread nyingine. Kwani kwa maneno yako mwenyewe unataka kujadili watu. Anayejadiliwa ni kiongozi wa umma hao wengine wakiwa viongozi wa umma una uhuru wa kutaka kujua wamefanya nini kama legacy yao.

Vinginevyo itabidi tuishie kujadili miti!

Kila jambo linamipaka si kwa vile ni kiongozi lazima wasifu binafsi wake wa ndani na nje ujadiliwe unakua unaelekea ktk UMBEYA.

Na mtu ukitaka kujadili wasifu binafsi wa mtu kwa swali hilohilo unalotaka kumuuliza ANZA kujiuliza kwanza wewe mwenyewe swali hilo hilo na ukipata jibu lake kutoka kwako mwenyewe ndipo NENDA hatua nyingine zaidi kuhoji ndg yako.
 
Moja ya mafanikio yake ni kusaini kesi zote za vifo ambazo zilipaswa kusainiwa na Mwalimu kama Rais wa nchi.Mwalimu kama raisi alikuwa anatakiwa kisheria kusaini kesi za vifo ili watu wanyongwe! Ila yeye kutokana na imani yake aliamua kutofanya hivyo.Ni Kingunge ndiye aliyetekeleza hayo kutokana na yeye kutokuwa na dini.
Na Kingunge bila ya hiyana alisaini na kuidhinisha unyongwaji wa watanzania kwa muda mrefu sana.
 
hakuna anayejadili wasifu binafsi wa mtu; sijauliza Kingune analala wapi, amekula nini, mke wake ni nani n.k Sijauliza swali lolote nje ya huduma na utumishi wake kwa Taifa. Kama hujui tofauti ya vitu hivi viwili itakuwa vigumu kukujulisha.

So, soma tena swali na jaribu kulielewa.
 
ok MAMAJUSI : keep it up.

Theory -inatokea wakati ule kila kitu tunakijua Lakini hakuna hata kimoja kinachofanya kazi.

Practical-Inatokea wakati ule kila kitu kitu kinafanya kazi barabara Lakini hakuna anayejua kwa nini.
 
well, ukweli unabakia kuwa hukulielewa swali ukajaribu kulijibu kama umelilewa na kwa kufanya hivyo umeonesha ni jinsi gani hukuliewa.
 
Najiuliza hivi historia ya Tanzania itaandika nini kuhusu mchango wa Kingunge katika Taifa letu ukiondoa jina hilo la "Kingunge" ambalo limebakia kuwa alama ya mtu ambaye ni kigogo na kiongozi mkubwa? Ni nini hasa mchango wa Kingunge katika siasa, uchumi, na maisha ya Tanzania? Ni kitu gani tunaweza kusema kuwa kisingefanyika kama Kingunge asingekuwepo? Je historia itaandika nini juu ya Kingunge au atabakia na alama ya nyota tu katika footnote ya historia?

Mwankjj,

Mimi kwa mtazamo wangu yafuatayo ni mao yatakayoweza kutufanya tumkumbuke KIngunge...!

1. Ni kiongozi wa pekee Tanzania ambaye alikula kiapo bila ya kutumia kitabu cha dini yoyote, haijawahi kutokea tena.

2. Ni kiongozi pekee aliyewahi kuteuliowa kuwa Waziri kwenye Wizara iliyokua haina katibu mkuu, haina mfanyakazi yoyote hata tarishi na ofisi zake zilikua Ikulu (Wizara ya Ustawi wa Jamii).

3. Ni moja ya kiongozi aliyewahi kuwa na Mtoto mkorofi na asiyeheshimu wala kuogopa mtu Bw. Kinjekiitile.

4. Tutamkumbuka pia kwani ni kiongozi pekee ambaye hajawahi kubadilisha vazi zaidi ya Kaunda Suti, kama kuna mtu amaeshawahi kumuona Kingunge mevaa vazi lingine ajitokeze hapa...!

Bado ntawaletea mengine baadae....!
 
Mwankjj,

Mimi kwa mtazamo wangu yafuatayo ni mao yatakayoweza kutufanya tumkumbuke KIngunge...!

.............................................

2. Ni kiongozi pekee aliyewahi kuteuliowa kuwa Waziri kwenye Wizara iliyokua haina katibu mkuu, haina mfanyakazi yoyote hata tarishi na ofisi zake zilikua Ikulu (Wizara ya Ustawi wa Jamii).

..........................................!

Bado ntawaletea mengine baadae....!

Mhafidhina, masahihisho kidogo katika hilo #2.

Alikuwa ni Waziri asiye na Wizara Maalumu (Minister of State, President's Office). Kwa kumbukumbu yangu, wa kwanza kuishika hiyo wizara isiyo na Katibu Mkuu, wafanyakazi na hata tarishi alikuwa ni Mzee Rashid Kawawa baada ya kuachia Ukatibu Mkuu wa Chama miaka ya 80s, wakati Mwinyi anaingia.

Huyu Mzee ni sharp sana ukikaa kuzungumza naye, lakini ni wale ambao utekelezaji au ufuatiliaji wa yale wayasemayo ni karibu na sifuri. Kwa maana nyingine ni kwamba wanajua tu kumwaga sera (Makamba type).
 
Iweje "mnamkumbuka" Kingunge, kwani hayuko nasi tena? Siku ataacha kuwa nasi sijui atamwambia nini "Mzee"? Maana Mzee atamwuliza kwanini alisema "hayupo"? Labda atjibu "you did not give me enough evidence".

That is neither here nor there. Mwenzetu kataka kujua "mchango" wa Kingunge. Kweli "mchango" wa Kingunge ulikuwa ni mkubwa sana. Kashiriki sana kutufikisha hapa tulipo (ambapo ni pabaya). Maana hii michango si lazima iwe positive.

Kingunge alikuwa ni Suslov (Party Ideologist) wa Tanzania. Alichangia sana mawazo ya kukamata maduka, kukamata majumba yote yaliyokuwa na gharama zaidi ya shilingi laki moja, na kulazimisha watu wahame makwao wakakae vijiji vya ujamaa.

Imagine mtu na mkeo na wanao mnatolewa mkuku kwenu mnakwenda kukaa kwenye nyumba zilizojengwa kwa mstari, na kwa kutumia bush material! Kingunge, Mwalimu na Kawawa walipanga na kutekeleza hayo, kwa kushirikiana na majeshi, wakati wenyewe wakikaa na wake zao kwenye nyumba zenye air conditioning!

Huku mwishoni Kingunge kajitafutia kamrija. Kakaweka pale kwenye parking system Dar. Nasikia zaidi ya nusu ya fedha zote za parking Dar anachukua Kingunge. Hawekezi chochote. Anaziweka tu mfukoni. Hakuna cha tenda wala cha nini, lazima kila anayepaki gari Dar ampe Kingunge mshiko. Na hili linalindwa na Chama, kwa hivyo marufuku kulizungumzia serikalini.
 
Legacy ya Kingunge ni kwamba hakuwa fisadi na wala siyo fisadi so far. Kama kuna vijimali ambavyo vinaonekana sasa hivi ni jitihada za mkewe pamoja na mtoto wake katika kuona kwamba hawabaki nyuma kimaendeleo.

Ila kwa itiakadi, Kingunge ni mjamaa, na aliishi kijamaa kama alivyoishi Mwalimu. Hana sifa ya kujilimbikizia mali.
 
hakuna alichofanya zaidi ya kuandika volumes ya vitu visivyotelezeka, hakuwa mjamaa au bapari, bali aliyechanganyikiwa, hadi akamwasi Mungu, akajiweka mahali pa juu sana, kiasi ambacho akadiriki kupuuza misahafu mikuu iliyopo kwa zaidi ya miaka milioni moja.
hana mchango wowote katika taifa hili ambao ni chanya

mchango mkuu aliofanya ni kulea mafisadi na kuwalinda kwa nguvu zote, pia kuiondoa ccm kwen ye dira aliyonayo julius

Msahafu miaka milioni moja. Msahafu gani huo. Upi?
 
Moja ya mafanikio yake ni kusaini kesi zote za vifo ambazo zilipaswa kusainiwa na Mwalimu kama Rais wa nchi.Mwalimu kama raisi alikuwa anatakiwa kisheria kusaini kesi za vifo ili watu wanyongwe! Ila yeye kutokana na imani yake aliamua kutofanya hivyo.Ni Kingunge ndiye aliyetekeleza hayo kutokana na yeye kutokuwa na dini.
Na Kingunge bila ya hiyana alisaini na kuidhinisha unyongwaji wa watanzania kwa muda mrefu sana.

Ya kweli haya jama? Tunamuonea mzee wa watu hapa sasa.
Wakati wa Mwalimu,aliyehukumiwa kunyongwa alikuwa ni mtu mmoja tu,nae alikuwa ni yule Mhehe aliyemuua Kleruu,na mpaka Mwalimu anatoka madarakani nadhani huyo bwana alikuwa hai bado(sina uhakika)
 
Ndani ya chama na serikali, Kingunge is among the best strategist. kazi zake hudfanyika ndani zaidi hivyo ni vigumu kuona wazi wazi legacy yake ni nini. lakini kila linapotokea jambo kubwa la kisera, Kingunge ni kati ya watu ambao hutumika kulishughulikia. Kwa mfano, Ilani nyingi za uchaguzi yeye hushiriki kuanzia evaluation ya utekelezaji wa ilani inayomalizika, kuratibu utafutaji wa maoni ya ilani mpya, kuandika ilani mpya, na kuhakikisha mgombea anaielewa vema.
tatizo ni kuwa anazidiwa sana na nguvu ya pesa na ndio maana siku za hivi karibunio, michango yake inaonekana kutokuwa na mantiki tena.
Tangu walipokutana Zanzibar kubadili Azimio la Arusha, nguvu ya Kingunge imeyeyuka kwa kiasi kikubwa kwa sababu yote anayoyafanya husimama katika ujamaa na 'msahafu' wake mkubwa ulikwua ni azimio la arusha.
Sasa hivi amebakiwa na jukumu kubwa la kuspin mamb
 
Ukiona watu hawawezi kueleza achievements zake mara moja, ujue kuna walakini.

Hata mimi kichwani, hakuna linalonijia la maana kuhusu huyu mzee.

Sana sana ni mtu anayeamini na kutuhubiria juu ya party(political) supremacy (chama kushika hatamu).

Mzee Kingunge ni mwanasiasa mkongwe na atakumbukwa kwa kuwa sehemu ya mhimili wa siasa za Tanzania. Ni bingwa katika Political propaganda na sijawahi kuona mwanasiasa mwingine yeyote wa kiwango chake.

Mwanasiasa ambaye mimi ninamwona anaweza kuchukua nafasi (kiuwezo) ni Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Sumaye. Huyu ni mzuri sana kwenye mikakati na ni mwanasiasa makini kama alivyo Mzee Kingunge.

title ya " kingunge" ambayo imepata umaarufu si Tanzania tu bali hata nchi jirani, ilitokana na nini maana huenda ilikuwa ni matokeo ya harakati za mhusika kwenye suala fulani muhimu.Siamini kama imekuja hivihivi tu na kuingia kwenye msamiati. Naomba wenye kujua asili yake watuelimishe.
 
Legacy ya Kingunge ni kwamba hakuwa fisadi na wala siyo fisadi so far. Kama kuna vijimali ambavyo vinaonekana sasa hivi ni jitihada za mkewe pamoja na mtoto wake katika kuona kwamba hawabaki nyuma kimaendeleo.

Ila kwa itiakadi, Kingunge ni mjamaa, na aliishi kijamaa kama alivyoishi Mwalimu. Hana sifa ya kujilimbikizia mali.

Ufisadi si lazima uibe fedha za umma.

Kutumia madaraka kwa nia ya kudumaza na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi ni Ufisadi mkubwa, pengine ni ufisadi mkubwa kuliko hata ule wa kuiba fedha.

Kingunge ni Fisadi.

Kitu kimoja ambacho Kingunge na waasisi mafisadi wenzie hawakujua ni hii hali ya kuanikwa hadharani na ujuvi wao kuchambuliwa huku wao wakiwa hai.
 
Legacy ya Kingunge ni kwamba hakuwa fisadi na wala siyo fisadi so far. Kama kuna vijimali ambavyo vinaonekana sasa hivi ni jitihada za mkewe pamoja na mtoto wake katika kuona kwamba hawabaki nyuma kimaendeleo.

Ila kwa itiakadi, Kingunge ni mjamaa, na aliishi kijamaa kama alivyoishi Mwalimu. Hana sifa ya kujilimbikizia mali.

Ndugu yangu heshima kwako. Bado sielewi maana ya fisadi, au inawezekena labda wewe ndugu yangu unapunguza maana ya ufisadi. Nakushangaa sana unapomfananisha Kingunge na Mwalimu. Wakati Mwalimu alipoona kuwa umri umekwenda aliamua kujiuzulu uongozi, walipombembeleza aendelee kwenye ngazi ya chama alikubali kwa shingo upande na akaamua hata kuconjure kung'atuka. Lakini Kingunge alikubali uwaziri wakati mwenzie aling,atuka, sijui kwa hili nani better. Kingunge ndiye alikuwa wa kwanza kusema kuwa allegations zilizotolewa kwenye orodha ya mafisadi ni distraction, sijui kama mwalimu angesema hivyo. Kingunge amejiwekea kamrija TPS na Ubungo terminal, bado sijajua mwalimu kamrija kake kako wapi, kingunge amewatetea waziwazi mafisadi na anaendelea kuwakemea wale wanaopinga ufisadi waziwazi na ameunga mkono vitendo vya kuwaadhibu wapigania haki, i wonder kama mwalimu angefanya hivyo.
Namuunga mkono aliyeanzisha nyuzi hii. Inatusaidia kuondoa unafiki wa kuanza kumsifu mtu akifa kwa mengi ya uongo mara pengo lake halitazibika, alikuwa mchapa kazi, mara alikuwa mzalendo, mara hili mara lile. Ni vizuri tukawa wakweli kuwa pamoja na kuwa hakuwa malaika, Mwalimu hawezi kulinganishwa na yeyote, kizuri zaidi ni kuwa hawezi kulinganishwa na Kingunge.
Mtu kama yeye ni watu ambao taifa lingewategemea sana kwenye wakati mguu kama huu, ambao tunaona wazi kuwa kuna leadership vacuum. Lakini ameprove kuongeza hivyo vacuum, mimi naona JK is much much better than him.
 
Kuna point imetolewa kwamba Mwalimu alipoona amezeeka aliamua kung'atuka, lakini Kingunge hajafanya hivyo.

Because of his faith, Mwalimu had something to look forward to. Because of his lack of faith in the after life, Kingunge must be extremely worried that now it is all coming to an end, and it had absolutely no meaning! When you do not believe in God, then towards the end of your stay here you enter into a deep crisis about the meaning of life. Why were you here? What if you were wrong?

You need to be a fool to praise those that have led you astray. Kingunge participated, in a leadership position, in an experiment that inflicted untold harm on Tanzania. His, I submit, was a very nasty contribution. We are still trying to recover from it.
 
Nini tena hiyo kitu mbaya alichotufanyia au alichoshiriki kutufanyia huyu mzee wa watu?
 
Back
Top Bottom