The future of Cloud computing

Gurta

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
2,234
531
Katika vitu ambavyo vimeshika vichwa vya habari za TEHAMA wiki hii ni pamoja na kuzinduliwa kwa iCloud -- huduma ya cloud computing kutoka Apple.

Najaribu kufikiri ni kwa namna gani nchi zetu za kiAfrika na hasa TZA; tumeweka miundombinu gani katika kuwezesha cloud compuing kufanya kazi? Nifahamuvyo ili hii huduma iweze kufanya kazi kwa ufanisi, miundombinu ya intaneti inabidi kuwepo na sio kuwepo tu bali kuwepo katika hali ya juu, kasi kubwa na reliability.
400px-Cloud_applications.jpg
Kwa mfano, zile notebook za zinazo-run Chrome zilizotangazwa zitakuwa na storage space ya 16GB. Hii ni sawa au pungufu ya storage space inayokuwa offered na smartphone nyingi tu. Kwa nini waweke storage psace ndogo hivyo? Google wanataka watumizi wa kompyuta zao kuhifadhi sio tu mafaili yao bali hata apps zinazo-run kwenye kompyuta zao katika cloud storage.

Sasa ndapo ufanisi wa kuhifadhi katika 'cloud' unategemea fast internet connection, reliable, accessible, affordable; Afrika na TZA specifically, tumejiaandaa vipi? Kuna mikakati gani? Tutaachwa nje au kuna nafasi na sisi kushiriki?

Naomba kuwasilisha. Karibu kwa mjadala
 
With cloud computing u can overcome lots of issues, 1. Infrastructure 2. Software 3. Storage.

Tanzania should consider building data centers, or allow companies to build data centers so that we can have our own cloud.
 
Back
Top Bottom