The flamboyant Lowassa

Geza,
Lisilowezekana kwa mwanadamu, kwa Mungu linawezekana!.

Mwana wa Adamu Alikuja kwa ajili ya waliopotea na sio kwa ajili ya watakatifu!.
Tena akahimiza "wote wenye mizigo waje kwangu nitawapumzisha!"

Wakuu wa kanisa wanapaswa kutenda kama mkuu wao kuwakumbatia wasio wakamilifu ili kuwatakasa!.

Na mwisho nasisitiza, " JIWE WALILOLIKATAA WAASHI LITAFANYWA KUWA JIWE KUU LA PEMBENI!".
Mkuu wangu mimi pia Mkatoliki lakini nakiri hakuna justification juu ya hili! Tuache kupotosha kwa kutumia maneno Matakatifu ili kujiridhisha.pale Lowasa hakuitwa kuinjilisha! Hata Alhaji Mzee Mwinyi alikuwepo! EL amealikwa na Kanisa kutoa mchango (huku wakijua wananchi wako gizani juu ya tuhuma zake!).Huwezi kumuhukumu mtu kwani mwamuzi ni mwenyezi Mungu lakini kinachoshangaza na kutia wasiwasi ni kauli ya Askofu wa Mwanza na EL kuruhusiwa kutumia madhabahu kujisafisha! Kanisa letu limetughafilisha sana tunaofikiri nje ya box! Ingekuwa wanatangaza kama mkutano wa injili then yeyote anakwenda(akiwemo EL) ingekuwa sawa tu lakini huku wanatoa kauli hatujamwalika huku kahudhuria! kweli Kanisa limefikia hapo? EL ni Mtanzania mwenzetu,kiongozi wetu lakini Kanisa kwa hili HALIELEWEKI!
 
Hela tamu hata kama ya wizi
Kama Yuda alimtosa Yesu kwa vipande 30 vya fedha kwa nini Pengo ashindwe?!
Kwanza nimekumbuka mapadri ni mafisadi wakubwa (wanalamba sana wake za watu huku wakijifanya waseja, hongera Slaa kwa kujitoa na kuonyesha unavyojua kulamba..) kwa hiyo sio ajabu fisadi EL kuambatana na fisadi Pengo
Namna ya EL kutubu: kukiri dhambi zake ZOTE na kuziacha then kurudisha serikalini mali ZOTE alizoiba (kumbuka Zakayo na BWANA Yesu) - hapo ndio atakuwa ametubu, sio kwa kugawa fedha haramu kwenye makanisa ya kifisadi
 
shida iko wapi? Lowasa ni mchapakazi hyo inajulikana mafisadi walimchafua ili kumharibia, ninachoamini kwenye ukweli uongo hujitenga. Ipo siku wa tz tutafuoguka macho na kuona.
 
mzee acha kukurupuka,Yesu alipokuja duniani hakuja kwaajili ya watu wema,bali kwa wenye dhambi ili wapate kutubu.Pia kwa yeyote anayejiona kua hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia Lowasa mawe.Pia kipimo cha dhambi ni Mungua anayejua.Mungu ndiye anayejua kua Lowasa ana dhambi au la.Pia leo hii ukiambiwa Lowasa ana utajiri wa kiasi gani na uko wapi utasemaje?

Mungu ndo yuajua dhambi za mtu lakini athari za ufisad wa EL zinaonekana!
na kama Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi Askofu analijua hilo ndo maana amemwalika EL.
 
Inanikumbusha yule Mnyama kwenye Ufunuo wa Yohana ambaye alipotokea tu, Binadamu wote WAKAMSUJUDIA.

Ila Panga la Mungu liliposhuka............. hivi inaishiaje vile?
 
Huyu mmasai akishika nchi hakika wewe hukosi ukuu wa wilaya take it from me
Mkuu Mende, mimi ni maskini jeuri, Kama nimekataa ajira ya £.4,000 FCO, what for niutafute ud DC wa TZS 2,400,000/= ?!.

Hivi u DC mnauona dili?!. I had a good decent job nikaacha sasa naendelea kuchakura kitaa=. Kuku wa kienyeji hafugiki!. Money is not everything!. Money can't buy happiness and satisfaction. I'm happy with whatever I do japo in stinking poverty!.
 
Huyu mmasai akishika nchi hakika wewe hukosi ukuu wa wilaya take it from me

Kwa kawaida ufikapo msimu wa masika mvua ni lazima inyeshe hata kama wachawi watatia fitna zao. Lowasa ni kama mvua, utake usitake itanyesha tu!
 
kaa kimya!unakaa nchi gani kwanza na una umri gani na akili yako ikoje?kama hujui makosa ya huyu mwizi!

Kwahiyo ushauri wako ni mimi kukaa kimya?? Soma signature yangu hapa chini utaujua msimamo wangu kuhusu watu wanaokaa kimya huku wakiujua ukweli... Pili Tujadili hoja iliyopo jukwaani, nina umri gani na ninakaa nchi gani it is absolutely none tena narudia IT IS NONE OF YOUR BUSINESS.

Kama wewe unakaa Tanzania una umri unaodhani unafaa na akili yako ni nzuri AUNAJIAMINI KUWA GREAT THINKER, well and good mimi sijayataka hayo yote bali nahitaji kujua kosa la lowasa ninini lakini with evidence..... otherwise kilichobakia ni majungu na hatuwezi kufika popote kwa kuendekeza majungu matokeo yake nchi inakaa bila viongozi.

Tangu amejiuzulu unaweza kusema tuna Prime Minister?? Anaweza kurejister nini alichokisimamia kikafanikiwa? Msimamo wa Lowsa na Uchapa kazi wake bado unahitajika vinginevyo toa uthibitisho na acha kufuata mkumbo kwakuwa wengi wanasema alihusika na richmond na wewe unashabikia bila hata kusoma ripoti yenyewe na kuona uhusika wake.

 
Kama Edo ni msafi ana haja gani ya kutumia nguvu nyingi anazotumia kujinadi? Kama yeye kidume atuachie wananchi tumtathimini maovu yake,mema yake,longolongo zake,ujeuri wake,fitina zake,mipango miovu yake,utendaji wa kiimla wake,nk na mwisho tulinganishe mzani unalala wapi! Edo pole sana urais 2015 utahitaji kuuangalia kwa kutumia darubini is tok far beyond your reach,sio Tanzania hii.
 
Back
Top Bottom