Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
This is interesting and it adds to Mchungaji curiosity of the real relatioship between Lowassa and Kikwete.
In the past 6 months, the two have had their differences on issues being subject of my scrutiny.
First it was Arusha MP elections, then Arusha Municipality saga, then Education fund and most suprising the Dowans saga.
Now Lowassa is stating that Wananchi should be at fore front of uwekezaji.
Lowassa anahimiza wawekezaji wa ndani na wazalishaji wasimame mstari wa mbele na kuwapa motivation kuwa wana uwezo kama hao wa nje.
Kikwete anasisitiza wawekezaji kutoka nje ya nchi waje na kuwa ndio njia pekee ya kuinua uchumi wa Tanzania.
Swali, ni nani mzalendo au ni nani kweli kati yao pamoja na madhambi yao anaonekana kujali Watanzania?

Lowassa awafunda wajasiriamali
Imeandikwa na John Mhala, Monduli; Tarehe: 13th May 2011 Habari Leo
WAJASIRIAMALI mkoani Arusha wametakiwa kutogeuka soko la watu wengine hivyo wabuni bidhaa wanazoweza kuziuza ndani ya Afrika ya Mashariki na hata masoko makubwa ya nchi za Kusini mwa Afrika kama SADC,SACU na COMESA.
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa ametoa changamoto hiyo leo katika semina ya siku mbili inayofanyika mjini Monduli ambayo iliandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Lowassa amesema, Tanzania hususani mkoani Arusha kuna ardhi nzuri inayostawisha mazao yote na kutoa mfano kuwa kilimo cha mbogamboga kuwa ni biashara ambayo inaweza kuwafanya wakazi wa Arusha kutisha kwenye soko la Afrika Mashariki.
Amewataka wajasiriamali mkaoni Arusha kutumia semina hiyo ya TIC kujinufaisha kibiashara na kuacha kuwasindikiza wawekezaji kutoka nje ya nchi kuja nchini kuwekeza shughuli zote wakati shughuli zingine zinaweza kufanywa na wajasiliamali na hapa mkoani Arusha.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha amesema na kusisitiza kuwa, biashara ya mboga mboga na mifugo ina soko nje ya masoko haya ya Afrika pia soko la AGOA la nchi za Marekani, Ulaya, Arabuni na Asia.
Amesema, wajasiriamali wengi mkoani Arusha na hata mikoa mingine hawana ufahamu na nguvu kubwa ya kiuwekezaji na wachache sana wanaifahamu TIC na vivutio wanaopewa wawekezaji na kama wapo ni wachache sana hivyo kupitia mafunzo haya baadhi yao watakwenda TIC ili muweze kusajili biashara na uwekezaji.
"Tumieni semina hii ya TIC kujiendeleza na musiache watu kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchi biashara ambazo hata nyie munaweza kuzifanya hiyo ni aibuamesema
Mratibu Mkuu wa semina hiyo, Mbunge wa viti maalumu mkoani Arusha, Namelok Sokoine amewataka akina mama wa mkoa wa Arusha watumie fursa ya semina hiyo kujikwamua kiuchumi ili waweze kujiongezea kipato.
Sokoine amewataka akina mama waliokuja hapo kuwa mabalozi wazuri kwa wale wasiofanikiwa kuja katika semina hiyo kuwaelimisha na kuwa chachu mpya ya kuleta maendeleo katika maeneo yao.
Mkurugenzi Uhamasishaji na uwekezaji wa TIC,Raymond Mbilinyi, alisema mkoa wa Arusha unashika nafasi ya pili ya uwekezaji ukiachia mkoa wa Dar es salaam hivyo jitihada za ziada zinahitajika kutaka wajasiliamali kujitokeza kuwekeza katika biashara mbalimbali zilizopo mkoani hapa.