The Citizen: JK alilishinikiza Bunge kumpa Zitto ulaji

Kumbe JK ana power ya kulishinikiza Bunge lifanye atakavyo? Ha ha haaaaaa ha.
Mie nilifikiri Zitto yuko pale kwa nguvu ya CHADEMA kumbe chadema si lolote si chochote.
Majimshindo leo umeuliza swali zuri mno... hongera sana
Jibu ni ndio. Ana power hiyo akitumia wabunge vikaragosi wa CCM wanaoongoza na kibibi jitu.....
Ndio maana tunapigania mabadiliko......
 
Asante Zitto. Kumbe ni kweli kwamba rais alikuwa involved? hapo nimeelewa, mengine wacha waendelee kuuliza wengine! Nimepata ukweli mmoja tu hadi sasa katika story hiyo ya the citizen kwamba rais alikuwa involved katika maamuzi ya kura hizi. Sasa mwenye taarifa tofauti hasa kuhusiana na Zitto kumpigia rais simu aje na kutuhakikishia! tusimsurubu kwanza kabla hatujapata uhakika!:photo:
 
Mr. I always like to think independently,

je asipokuja JF utamfanya nini? n je maswali uliyouliza hatuwezi kupata majibu kwingineko? kama taarifa hii hakuitoa zito, kwa nini tupate majibu mengine kwa zito?

Swala la Zito ni very complicated ndani ya chama chake na nachelea kusema tumelitengeneza wenywewe.

Ukweli unabaki palepale hata kama zito leo hii ataamua kuwa fisadi kama wengine wote, Hakuna mnaloweza kumfanya!!! mtaishia matusi tu na kejeli..hii ndiyo hula yenu

Kwa sisi wengine ambao tunashindwa kuvutwa na upepo naweza kusemakama Zito ana tatizo basi ni tatizo la chama chake choote

Hii habari Citizen wanasema wameitoa ndani ya chadema!! what a shame! ina maana ndani ya chadema kuna vitu viwili

1. Kuna uchafu unaendela kiasi cha kuwa hata zito akiufanya wengine hawawezi kumuadabisha kwani nao wanayoyao
2. Kama CDM haiwezi kumchukulia hatua basi ni dhaifu sana, kama wanaogopa kuwa wakimfukuza Zito watakipasua chama basi ni sawasawa na Pinda alivyosema tukikamata mafisadi nchi itatikisika! I insist there is a problem somewhere!

Haya ni mswali magumu ya kichama, ukija kiserikali

1. Je leo naweza kumpigia simu JK na akanipa cheo ninachokitaka?? Kama Zito aliomba na kukiwa hamna chance ya chadema kupata nachanganyikiwa ,aidha Zito anaihitaji kusifiwa! na kama anahitaji kulaumiwa basi ppoint za hapo juu apply!
2. Kama Zito alimpigia simu JK AIDHA na tunavyojua ni serikali imeshindwa kabisa hivyo Zito anaingia kama expert! serikali imeonyesha udhaifu na bila akili na msaada wa Zito Ngeleja chali!

Au wengine tungeweza ku-view hili swala kuwa SI MARA YA KWANZA KWA ZITO KUJITOKEZA KUONYESHA ASPIRATION FULANI KATIKA VITU FULANI SI MARA YA KWANZA

1. Zito alikuwa mtu pekee kuzungumzia swala la Dowans nyakati zile ambazo hakuna aliyeweza kusema chochote kile mpaka kiongozi wa nchi! aliyosema wote tuliyasikia, dowans ile , leo tunajua status, na hakuna siri! Kwangu mimi Zito is an hero...Yes kama mjasiriamali basi nacheka sana kuwa kumbe JK akipigiwa simu tu anatoa cheo?? This made my day! kesho napiga simu kutaka uwaziri mkuu! Pinda hawezi. Kipindi kile neno la rais lilitakiwa sana na sentensi au tamko la ZITO LILIONEKANA KAMA NDIYE RAIS...historically noted! na wengi mnafanya kosa hili tena na tena!

2. Hata sasa udhaifu wa cabinet na baadhi ya watenda kazi wa serikali hamna kitu ni zero na wakitokea akina Janaury makamba na akina Zito wakaonyesha wanaweza WANAPEWA TU, kwani leo hii JK akamteua say MKJJ kuwa bosi wa NSSF nani atabisha?? au atakuwa kanunuliwa, hatuna tabia ya wakenya ya kujiuza au KUUZA CV na ability zetu, kila siku mtabaki kusema yule analinda mafisadi!

Mwisho though is painfully to say this CHADEMA losed his status

1.Wasingerudi bungeni mpaka leo hii mpaka kieleweke swala la aktiba ambao leo hii ...kimya!
2.wangekomaa kutomtambua JK kuwa rais wa nchi hii

Sasa matumbo ya njaa ya hawa wabunge wa chadema ndiyo yanasababisha haya yoote, ndiyo wale wapi? hamjaona juzi wamepewa mil.90 na wamekaa kimya, mnataka tuwanyoshee vidole wachache tu!!!

Haya endeleeni kumtukana Zito lakini msisahau Hoja, kama hoja ni kupiga simu na kupata cheo...na sio kuwa JK alimbembeleza Zito then we are not judging this fairly!

Please Zito whereever u are if this information is true, receive my warm congrats, Thank God you have exposed JK once again!. Naomba namba ya JK nataka cheo fulani!!

Highlited in red: Majibu katika para hizi mara moja yananilazimu niseme hivi:
Si lazima kitu kitoke kwa Zitto mwenyewe ndiyo akijibu. Je akiambiwa ameuwa mtu, je hawezi pia kujibu?

Lakini kubwa zaidi ni kwamba paragraph hizi zinanizidishia hisia zangu kwamba 'Waberoya' ni alias nyingine yab Zitto. Ukiisoma replu yake yote kwa makini na utulivu utagundua kwamba ni Zitto tu ndiye angeweza kuiandika -- anailaumu CDM na pia anamlaumu JK. Yote ni katika kujipurukusha tu!
 
Mhe. Zitto,

Yani nilikuwa naogopa jinsi ungekuja kwa hasira but Mungu saidia jumapili njema iwe kwako.

Kaswali kadogo; hivi wewe binafsi kwa utashi wako kwa kumjua JK kama angekuwa Tundu Lissu, angempigia chapuo? maoni yako tu.

asante

Alhaj
 
Asante Zitto. Kumbe ni kweli kwamba rais alikuwa involved? hapo nimeelewa, mengine wacha waendelee kuuliza wengine! Nimepata ukweli mmoja tu hadi sasa katika story hiyo ya the citizen kwamba rais alikuwa involved katika maamuzi ya kura hizi. Sasa mwenye taarifa tofauti hasa kuhusiana na Zitto kumpigia rais simu aje na kutuhakikishia! tusimsurubu kwanza kabla hatujapata uhakika!:photo:
Kwamba Rais alikuwa involved or not mimi sijui. Habari zote tunaambiwa na wabunge wa CCM na hatuwezi kuthibitisha. Ninachothibitisha ni kwamba sikuongea na Rais kumtaka anisaidie.
Tunachoambiwa ni kwamba Pinda aliwaambia wabunge wa CCM kwenye kikao chao cha pili kwamba Rais kasema mpeni Zitto.
It was not my interest to find out the truth, my interest was to win the post and I won! All others are CCM problems and they sort out themsleves
 
Mhe. Zitto,

Yani nilikuwa naogopa jinsi ungekuja kwa hasira but Mungu saidia jumapili njema iwe kwako.

Kaswali kadogo; hivi wewe binafsi kwa utashi wako kwa kumjua JK kama angekuwa Tundu Lissu, angempigia chapuo? maoni yako tu.

asante

Alhaj
Siwezi kumjibia Rais
 
Sasa inakuwaje Rais anatoa maamuzi kuwa mbunge huyu apewe nafasi hii? Huku si kuingilia chombo huru kingine...........shii hivi nimesema chombo huru!! sorry.
Bunge si huru, liko kwa ajili ya kundi fulani........hii ni dangerous ya hatari kweli.
 
Wakati mwingine muwe mnapita kwenye blogu yangu Zitto na Demokrasia kwa maelezo ya mambo mengi kabla ya kukimbilia kwenye judgements.

Zitto,

Hii ni nasaha kutoka kwa mtu mzima.

Huwezi kutumikia nchi hii ipasavyo ukiendelea kuwa chadema. Hawana kheri wala hawaioni michango yako. Si uongozi si wapenzi. Sababu, nna uhakika wewe ni mtu mwenye fikra na unaelewa ni nini.

Nakuasa, ondoka Chadema haraka iwezekanavyo, nenda CCM kafanye mabadiliko yanayohitajika huko. Huko una "chance" kubwa ya kufanikisha nia yako ya kuwatumikia waTanzania.

Na kama ni vigumu kwenda CCM, anzisha chama chako na sisi tutakufata na kukuunga mkono.

Ingawa mimi si CHADEMA wala sina mapenzi na chadema lakini ukweli ni kwamba nimekuwa "fan" wako baada ya kukusikiliza na kukuona kuwa ni "kiongozi" na una ari ya kweli ya kuwatumikia wa Tanzania.

Hiyo ni nasaha yenye "options" mbili, ya kwanza ndio the "best option" kwa mtazamo wangu.
 
Kwamba Rais alikuwa involved or not mimi sijui. Habari zote tunaambiwa na wabunge wa CCM na hatuwezi kuthibitisha. Ninachothibitisha ni kwamba sikuongea na Rais kumtaka anisaidie.
Tunachoambiwa ni kwamba Pinda aliwaambia wabunge wa CCM kwenye kikao chao cha pili kwamba Rais kasema mpeni Zitto.
It was not my interest to find out the truth, my interest was to win the post and I won! All others are CCM problems and they sort out themsleves
My interest was to win the post whoever helped me, very interesting.
 
Tatizo ni kwamba JK anaongoza genge la mafisadi katika serikali na Zitto anafahamu hivyo fika. Na kamao wewe huoni hilo tatizo basi ni mmoja wa genge hilo au unanufaika nalo au ni mbumbumbu tu katika jamii.
hehehehehehehehe
watanzania bana wepesi kweli kujaji wenzao,hata hatufahamiani umeanza mbumbu ooo nini,ok labda mwenzangu ambae sio mbumbu ni jambo gani ambalo jamii inajivunia kuwa bwana Marksman amefanya jambo na jamii ikasema yeah jamaa ndio
mimi nasimamia msimamo wangu kuwa sioni tatizo kwa Zito kupewa nafasi na JK kwanza ni mbunge pili ana akili timamu,hivyo wewe kama markman huna la kufanya juu ya ZITO
 
Siwezi kumjibia Rais

Ok, thanks.

Nahisi JK alitumia uanajeshi wake kufifisha hoja ya CDM kuwa wameonewa. Mimi naamini hivyo na ndo maoni yangu.

Kaswali kengine; Naomba ukanushe au ukubali kwa kusema ndio au hapana kuwa "Eti wewe una mahusiano na familia ya JK".

Baada ya hapo, i am out. Jumapili njema huko uliko.
 
hii habari haina any credible source. Watu wote waliotajwa majina wamepinga hii claim. Waliokubali wameficha majina. What does that say?
 
Zitto,

Hii ni nasaha kutoka kwa mtu mzima.

Huwezi kutumikia nchi hii ipasavyo ukiendelea kuwa chadema. Hawana kheri wala hawaioni michango yako. Si uongozi si wapenzi. Sababu, nna uhakika wewe ni mtu mwenye fikra na unaelewa ni nini.

Nakuasa, ondoka Chadema haraka iwezekanavyo, nenda CCM kafanye mabadiliko yanayohitajika huko. Huko una "chance" kubwa ya kufanikisha nia yako ya kuwatumikia waTanzania.

Na kama ni vigumu kwenda CCM, anzisha chama chako na sisi tutakufata na kukuunga mkono.

Ingawa mimi si CHADEMA wala sina mapenzi na chadema lakini ukweli ni kwamba nimekuwa "fan" wako baada ya kukusikiliza na kukuona kuwa ni "kiongozi" na una ari ya kweli ya kuwatumikia wa Tanzania.

Hiyo ni nasaha yenye "options" mbili, ya kwanza ndio the "best option" kwa mtazamo wangu.
Unaonaje ukimtumia nasaha hizi Magufuli nafikiri zitamfaa pia kwa vile na yeye ana chance nzuri ya kuwatumikia watanzania akiwa CCM.
 
Fuatilieni ule mjadala wa kipindi kile alipoteuliwa kuongoza kamati ya madini,na kufungiwa nilifungiwa humu...Hili lilitokana na ukweli kwamba imani na mapenzi yetu kwa Zitto vilikuwa very high!however nilijuwa Zitto tayari keshakuwa neutralised,hata wapiganaji wenzetu humu JF kama vile Mwafrike wa Kike na His honrable Rev Kishoka walinipelekea mashambulizi left right!Nilishangazwa ni mpinzani gani huyu tuliyemwekea imani?Nikaambiwa nataka watu waingie msituni!Kuhani alinipiga tafu sana that time.

Lakini nilikeep on kumwuliza Zitto kwanini kama kauli mbiu yake kule kwenye website ya CDM kuwa ana misimamo isiyoyumba imefutwa na msimamo wake wa kuingia kwenye kamati akiwa na wanakamati wengine ambao nao walikuwa wakituhumiwa kwenye isssue kama EPA nk.

Ilikuwa mshike mshike humu...Lakini imechukua years kwa baadhi yetu kurealize.
 
Unaonaje ukimtumia nasaha hizi Magufuli nafikiri zitamfaa pia kwa vile na yeye ana chance nzuri ya kuwatumikia watanzania akiwa CCM.

Hata na wewe unaweza kufanya hivyo, mimi nimemnasihi Zitto, wewe mnasihi upendae, au kuna tatizo hapo?
 
maelezo yta zitto yameficha mengi.....haiwezekani jk atoke huko aliko avute waya na amwambie pinda ''mpeni zitto''......kwa upepo wa wakati ule ni ngumu sana hii jk kuifanya na ccm wakakubali.......ccm walikuwa radhi kumpigia yeyote wa cuf lakini sio zitto....ndio maana tumeona hata arusha kimetokea nini juu ya umeya........kuna nini kati ya jk na zitto hadi jk amwamuru pinda kufanya juu chini ili zitto apate nafasi hiyo?.....

maelezo yako Mh.zitto yanaacha maswali mengi sana sio bure ......... i always think beyond the next meal
 
Ok, thanks.

Nahisi JK alitumia uanajeshi wake kufifisha hoja ya CDM kuwa wameonewa. Mimi naamini hivyo na ndo maoni yangu.

Kaswali kengine; Naomba ukanushe au ukubali kwa kusema ndio au hapana kuwa "Eti wewe una mahusiano na familia ya JK".

Baada ya hapo, i am out. Jumapili njema huko uliko.
Sina mahusiano yeyote na familia ya Jakaya Mrisho Kikwete.
Hoja hii ndio naisikia kwako. Kuna maneno yeyote kwamba Zitto ana mahusiano na Jakaya Kikwete?
 
Wakati mwingine muwe mnapita kwenye blogu yangu Zitto na Demokrasia kwa maelezo ya mambo mengi kabla ya kukimbilia kwenye judgements.

Sawa mkubwa! Ila huja-update kuhusiana na hii taarifa ya kupewa ulaji,pengine webmaster wako hayuko faster kukuconsult. Wananchi tunakosa uvumilivu kusubiri habari hot kama hizi.

Pia hongera kwa kuja bila jazba yoyote leo,hope weekend imekaa vizuri!
 
the citizen walikuwa right 90+%. thanx kaka zitto kwa maelezo mazuri. Sasa nimejua chadema ina kazi kubwa, hongereni sana dada matiko na regia nipo nyuma yenu
halafu spika analazimisha chadema ifunge ndoa na hawa malaya
 
Back
Top Bottom