The Citizen: JK alilishinikiza Bunge kumpa Zitto ulaji

nimeitafuta hii habari kwenye Tanzania News - International News, Tanzania Local News, All Tanzania News, News for Tanzania, News from Tanzania, Tanzania, News! sijaipata!! au kuna gazeti la citizens la kiswahili? maana mada ya citizens lakini imeletwa kwa kiswahili au ndio fruits za shule ya kata...

USIPATE SHIDA HABARI NI HII HAPO CHINI- COPY AND PASTE.

How Kikwete saved the day for Chadema


Sunday, 20 March 2011 13:27
By Tom Mosoba and Florence Mugarula
Dar es Salaam. President Jakaya Kikwete personally intervened to help Chadema secure the chairmanship of at least one of the 17 parliamentary committees and avoid a whitewash, as newfound allies CCM and CUF had teamed up in the National Assembly to lock out the vocal opposition party.

President Kikwete, sources told The Citizen on Sunday, influenced the re-election of Kigoma North MP Zitto Kabwe, as chairman of the Public Corporations Accounts Committee (POAC), despite the raging hostility between his own Chama Cha Mapinduzi (CCM) and Chadema.

Sources in Chadema and within the National Assembly confirmed that Mr Kabwe, a rabid critic of the government in the last Parliament, telephoned President Kikwete to seek his help in his last-ditch efforts to hold onto the position. He was then facing stiff opposition from hostile CCM lawmakers supported by the opposition Civic United Front (CUF), Tanzania Labour Party (TLP) and NCCR-Mageuzi MPs.

After speaking to Mr Kabwe, the President, who is also the CCM national chairman, reportedly directed Prime Minister Mizengo Pinda to rally support for the Chadema MP to head the POAC.

“Mr Pinda told the CCM lawmakers that the President wanted them to vote for Mr Kabwe,” a Chadema MP, who asked not to be named, as he is not the party’s spokesman, told The Citizen on Sunday this week.

However, the State House in Dar es Salaam, denied that President Kikwete had exerted pressure on the MPs or directed them on how to vote for the heads of the parliamentary committees that monitor and audit the Executive’s performance.

Assistant Press Secretary to the President Premi Kibanga said he was not involved in choosing or endorsing the heads of the parliamentary committees. She said that was the MPs’ role, in accordance with the parliamentary Standing Orders.

“The President is not involved in such business. Everything is done by the MPs themselves,” said Ms Kibanga in a telephone interview this week, when asked about Mr Kabwe’s alleged SoS phone call to the Head of State.

The Kigoma MP would himself not give anything away on his supposed lobbying of President Kikwete to personally intervene to secure him a second term as chairman of the POAC. Formed by the last Parliament, it has oversight over more than 100 public organisations and agencies that spend billions of taxpayers’ funds every year.

“What I know is that the CCM had agreed to endorse the Wawi MP, Mr Hamad Rashid Mohammed, in their midnight meeting instead of me, but later in the morning, things changed and I was endorsed with 13 out of 15 votes,” he said.
But reached for comment, Mr Mohammed dismissed the claim, saying he had no intention of challenging Mr Kabwe.
“I know nothing about that matter. I had wanted to vie for the Public Accounts Committee (PAC) chairmanship, but dropped the idea after Bariadi East MP John Cheyo said he would defend it,” he said.

Speaking on the sidelines of the recent MPs’ seminar at Ubungo Plaza in Dar es Salaam, Mr Kabwe could not confirm whether he spoke to President Kikwete on the issue. “I was sure of winning the post because I had already secured eight votes, which is the threshold, but I ended up getting 13, which was good,” said Mr Kabwe.

He defeated CUF Nominated MP Amina Mwidau Mohammed. According to the parliamentary Standing Orders, MPs, who are members of a given parliamentary committee, elect one of them to chair the committee. With 10 seats, CCM has a majority of members of the POAC. Chadema and CUF have three and two, respectively.

It was not immediately clear if Mr Kabwe called the President in his personal capacity or as his party’s deputy secretary general.

Chadema national chairman Freeman Mbowe, and the secretary-general, Dr Willibrod Slaa, could not be reached for comment.

The Kigoma North MP has in the past rubbed his party the wrong way, with critics alleging covert links with some top CCM bigwigs, an accusation he has vehemently denied.

Before the February Bunge committee elections, Mr Kabwe had been taken to task by his party for staying away, when they resolved to stage a walkout during President Kikwete’s State address to open the 10th Parliament. The MP would later be quoted by a section of the media, as saying that he held the President in high esteem and could not show disrespect by boycotting his address to Parliament.

Emerging details show that CCM had, in reaction to the walkout, planned to use its numerical strength in the House to block Chadema, which succeeded CUF as the official opposition in Parliament after the 2010 General Election, from heading the committees. The ruling party was also ready to support MPs from other opposition parties other than Chadema, to win those positions.

An MP said the Speaker of the National Assembly, Ms Anne Makinda, had rooted for Ms Mohammed for the post, after her own efforts to persuade the MPs to back Mr Kabwe had failed.

“Ms Makinda had also warned that removing the Chadema MP would be unwise because he had shown credible performance in the 9th Parliament,” said the MP, who requested for anonymity.

The MP, who comes from the Lake Zone, said a meeting in the night preceding the election had settled on the former leader of the Official Opposition, but the situation changed dramatically in the morning after the PM’s word went around. We could not reach Mr Pinda or his aides for comment


 
Unatafuta ngamia wa kupita kwenye tundu la sindano? Zito is a loser kwa kweli hawezi kujitokeza maana anajua anamtumikia nani. Niliwahi kusema kwenye hii forum kwamba huyu kijana bado hana uwezo wa kuwa kiongozi. Alitishwa na mafisadi na amenywea kama kuku aliyenyeshewa na mvua.
Zitto hakutishiwa alinaswa katika mtego wa pesa. Kiurahisi mno. Alipelekewa pesa na ...... Akapokea, that was the beginning of his end before he ends his beginning.
 
Tunamwomba Zitto aingie humu JF na atujibu masuala haya:

1. Je ni kweli aliwasiliana na JK kuomba ulaji katika POC?

2. Kwa nini alifanya hivyo?

3. Je hakuona kwambakwa yeye kupewa Uwenyekiti wa POC na JK kunamaananisha kwamba atakuwa anafanya majukumu yake kwa masilahi ya JK (aliyefanikisha kuipata nafasi hiyo) na serikali ya CCM kwa ujumla -- na siyo kwa masilahi ya umma wa Watanzania kwa ujumla?


zitto hana majibu ya maswali hayo kaka......san sana akingia humu atatoka povu jingi lililoambatana na matusi.........namjua yule jamaa kwa kutukana......
 
Tunamwomba Zitto aingie humu JF na atujibu masuala haya:

1. Je ni kweli aliwasiliana na JK kuomba ulaji katika POC?

2. Kwa nini alifanya hivyo?

3. Je hakuona kwambakwa yeye kupewa Uwenyekiti wa POC na JK kunamaananisha kwamba atakuwa anafanya majukumu yake kwa masilahi ya JK (aliyefanikisha kuipata nafasi hiyo) na serikali ya CCM kwa ujumla -- na siyo kwa masilahi ya umma wa Watanzania kwa ujumla?

Maswali yako yote yanaweza kupata majibu katika thread ya "Kamati ya Zito ya Mshambulia MMKJJ", Thread ya "MMKJJ juu ya CTI, Dowans na Issue ya NSSF" na "Tamko la Kamati hiyo kwa vyombo vya Habari"
 
nimeisoma habari ile........inaonyesha zitto alipia simu kwa jk kuomba hiyo post...na jk alivyo akamdairekti pinda kuhakikisha dogo anapata hiyo kiti....hapa najiuliza kuna nini nyuma ya pazia kati ya kikwete na zitto?....kwa nini jk atoe maelekezo hayo kwa pinda?
 
1. Zito alikuwa mtu pekee kuzungumzia swala la Dowans nyakati zile ambazo hakuna aliyeweza kusema chochote kile mpaka kiongozi wa nchi! aliyosema wote tuliyasikia, dowans ile , leo tunajua status, na hakuna siri! Kwangu mimi Zito is an hero...Yes
the other day same person

Mimi nimekuwa nikimfuatilia mheshimiwa Zitto, tangu alipoongoza mapinduzi ya kupindua serikali ya DARUSO mwaka 2002/2003 wakisaidiana na Ridhwan Kikwete na Omar Ilyas. Find out please. However, we all know JK ni mdini, maana alianza harakati za udini tangu akiwa UDSM miaka hiyo….na hili fuatilieni.

Nani anayejua Zitto ana mtambo wa kusaga kokoto na alipata tender ya barabara ku-supply kokoto? Is he defending his interest indirectly

I mean we should be careful na watu kama Zitto yes they are bright, mmh! But they might be dangerous for the opposition existence. But we should examine him carefully and not judge him. Nimegusia tu swala la uislam maana mpaka leo kuna baadhi ya waislamu wanaofikiri kuwa wanaiweza kuigawa nchi hii kidini, na kuna wakristo wanaofikiri wanaweza kuigawa nchi hii kidini
Kwa kweli huwa nabaki mdomo wazi nikisoma post za huyu jamaa.
 
Nyie watu kosa la zitto na cdm liko wapi? Mmeshaambiwa kulikuwa na njama ili cdm isipate kamati mojawapo. Jk kaokoa jahazi. Tatizo liko wapi?
Raia Fulani...
si kila kupata ni kuzuri. Wakati mwingine unafikiria kuwa 'umepata' kumbe umepatikana.
 
nimeisoma habari ile........inaonyesha zitto alipia simu kwa jk kuomba hiyo post...na jk alivyo akamdairekti pinda kuhakikisha dogo anapata hiyo kiti....hapa najiuliza kuna nini nyuma ya pazia kati ya kikwete na zitto?....kwa nini jk atoe maelekezo hayo kwa pinda?

Baba mkwe?????
 
weberoya mtu wa ajbu kweli...kuna siku kaja hapa na htread ya kumponda zitto wakiwa huko udsm....aliponda kweli.....leo anakuja na post yake kuwa kwake yeye zito ni Hero.......huwa sikuelewi....usifikiri watu huwa tunasahau
 
Zitto na JK wanacheza mchezo unaoitwa 'Game of Chicken' ukishaingia kwenye huu mchezo kwa waliosoma Game Theory, principle zake ni kwamba lazima mmoja akubali kushindwa, the worst possible outcome occurs when both players do not yield. Hapa kati ya Zitto na JK sioni kama kuna mtu anamwelekeo wa kutaka kushindwa katika eneo lake na matokeo yake yatakuwa mabaya kwa wote, huu ni utabiri wa kisayansi.
 
Kumbe JK ana power ya kulishinikiza Bunge lifanye atakavyo? Ha ha haaaaaa ha.
Mie nilifikiri Zitto yuko pale kwa nguvu ya CHADEMA kumbe chadema si lolote si chochote.
 
Umeiweka vizuri hii. Ajitokeze atueleze kwa nini amtegemee JK kwa ulaji. Kwa nini Wabunge wengine wa Chadema hakakufanya kama yeye. Ni dhahiri JK na CCM yake walikuwa wakiogopa wabunge makini wa CDM kama Tundu Lissu, Mnyika na Halima Mdee kuingia katika kamati hizo kwani caama hicho tawala ingekuwa ni kamasi tu zinawadondoka hadi mwisho wa uhai wa Bunge hili. Kwa Zitto wamepata ulaini kweli kweli.

Ulaini indeed.

Ukiangalia huyu dogo atakuja kuichuuza cdm. Kamati kama hizi na uozo wake zitakuja kuleta shida.

"Ukiamua kuishi maeneo ya dampo usilalamike harufu".
 
Salaam,
Naomba nitumie nafasi hii kufafanua kuhusu habari ya gazeti la The Citizen.
Nyote mnafahamu kwamba mkutano wa pili wa Bunge la kumi ulikutana kwa ajili ya kuchagua wenyeviti wa Kamati za Bunge ili kupata Kamati ya Uongozi ya Bunge. Mimi niligombea uenyekiti wa kamati ya POAC kamati niliyokuwa nikiongoza toka Bunge la kumi.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kamati za oversight ni kamati za Kambi rasmi ya upinzani Bungeni ambapo CHADEMA ilitimiza masharti yote ya kuwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.
Wabunge wa CCM kwa kushirikiana na CUF, NCCR na UDP waliamua kuikomoa chadema kwa kuinyima kamati hizi na hivyo kufanya tafsiri ya kanuni. Habari ambazo tulizipata ni kwamba kamati ya PAC ingekwenda kwa Cheyo, LAAC kwa Mrema na POAC kwa Hamad Rashid na hivyo chadema kutopata nafasi yeyote na kupunguza nguvu yake kwenye kamati ya uongozi ya Bunge ambayo hupanga ajenda za Bunge.
Mara baada ya kupata majina ya wajumbe 15 wa kamati ya POAC nilianza kampeni na msaidizi wangu kwenye kampeni alikuwa ni Mhe. Regia Mtema. Tuligawana wabunge ili kupata kura 8 ambazo zingehakikisha ushindi. Kati ya kura hizo nane, tatu ni zetu sisi wabunge wa CHADEMA-mimi, mhe Matiko na mhe Mtinda. Kwa hiyo nilikuwa natafuta kura 5 kutoka CCM.
Spika alipotangaza majina ya wajumbe jina la Hamad Rashid halikuwemo. CCM wakaitisha kikao cha caucus yao ili kufanya maamuzi juu wenyeviti wa kamati (walifanya hivyo hivyo wakati mimi na dokta Slaa tulipochaguliwa kuwa wenyeviti mwaka 2008).
Kikao chao kikaamua kwamba mwenyekiti awe Hamad Rashid, na kwa kuwa yeye sio mjumbe basi Spika amteue kuwa mjumbe. Kama Spika hatamteua basi mhe Amina Mwidau wa CUF achaguliwe. Wajumbe wa kamati ya POAC kutoka CCM wakapinga ndani ya kikao chao kwamba mimi ninafaa zaidi kuliko huyu mama wa CUF (ambaye mie wakati huu nilikuwa simfahamu kabisa). Wajumbe wote waliopinga uamuzi wa chama ninaambiwa walizomewa na hatimaye kuitwa jina mmoja kutamka kuwa watafuata uamuzi wa chama. Pinda ndiye aliongoza kikao hicho.Spika alipoambiwa abadili orodha yake na kumweka mhe Hamad Rashid, alikataa kwa hoja kwamba orodha imeshakuwa public na hawezi kuibadili. Akabakia mhe Mwidau kama mgombea ambaye CCM wanamtaka.
Wajumbe watano ambao walikuwa wamenihakikishia kura walimfuata Waziri Mkuu kumwambia kuwa wao wataenda kinyume na maamuzi ya chama na watanipigia kura. Usiku kucha wa siku ya kuamkia kupiga kura mimi na Regia tulizunguka kuhakikisha kura zetu zinabakia intact na hata kumshawishi Mbunge wa CUF Mwidau ajitoe.
Tukiwa tunajiandaa kwenda kwenye kupiga kura CCM wakaitwa kwa dharura na kuambiwa na Pinda kuwa uamuzi wa jana usiku umefutwa na Rais ameagiza achaguliwe Zitto.
Tukaenda kwenye uchaguzi, nikagombea na mhe Mwidau na nikapata kura 13 dhidi ya 2 za Mwidau.
Hiyo ndio background kwa ufupi.
Kwa hiyo, sikumpigia simu Rais kutaka anisaidie. Nimekaa bungeni miaka mitano na nazijua siasa za Bunge. Nilikuwa nimejipanga kiasi ambacho kushindwa kungetokea iwapo tu Chief Whip wa CCM angekuja kusimamia mwenyewe uchaguzi. Ikumbukwe pia mie nimekuwa student leader, najua siasa za kipiganaji. Inawezekana hata huyo mgombea angekuja kwenye mkutano baada ya kura kupigwa!
CCM walibadili msimamo baada ya kutishiwa strong rebellion from their own ranks that they will vote for me. Wabunge 5 wa CCM kati ya 11 kumwambia Pinda kuwa watanipa mimi kura ilikuwa ni ishara tosha kwamba wanaweza kuaoibika.
Pia inawezekana kabisa CCM walibadili msimamo asubuhi ili kutaka kudhoofisha hoja ya chadema kwamba mabadiliko ya kanuni yaliwalenga kwa kusema 'mbona Zitto kashinda'
Hayo ndio maelezo ninayoweza kuwapa ndugu zangu kuhusiana na suala hili. Kama kuna maswali zaidi nitawajibu kwa kadiri ya uwezo wangu.
 
Ulaini indeed.

Ukiangalia huyu dogo atakuja kuichuuza cdm. Kamati kama hizi na uozo wake zitakuja kuleta shida.

"Ukiamua kuishi maeneo ya dampo usilalamike harufu".
Kama analengo hilo amechelewa angefanya wakati ule, leo amebaki peupe kila mtu anaangalia matendo yake.
 
Back
Top Bottom