The best Antivirus this 2010: What's yours?



Wewe hiyo Norton Anti-Virus unaitumia wapi?Nyumbani au offisini?jaribu kutoeleweshe Vizuri mimi nilipoinunuwa Computer yangu hiyo niliikuta ndani ya Computer yangu Norton Anti-Virus ndiyo iliyokuwa Anti-Virus yangu ya kwanza kuitumia nikaitumia Takriban mwaka mzima. Matokeo yake nikagunduwa inaifanya Computer yangu kuenda Taratibu nikaitowa na kuiweka AVG.

AVG nayo nikaitumia karibu miaka 3 Matokeo yake yakawa kama hiyo Norton Anti-Virus. AVG inalinda vizuri lakini nayo inakwenda taratibu kama kinyonga AVG Nikaitowa pia. Nikaweka Kaspersky Anti-Virus nikatumia hiyo Kaspersky Anti-Virus karibu mwaka mzima ikawa inafanya vizuri na wakati Mwengine inakuwa inafanya manyago hailindi vizuri haswa Trojans.

Nikaitowa hiyo Kasepersky Anti-Virus nikaweka NOD 32 Anti-Virus, nayo NOD 32 Anti-Virus nikaitumia karibu miaka 2 na nusu bila matatizo ila baada ya hapo ikawa inaharibu Computer yangu ikawa inaharibika hiyo NOD32 Anti-Virus kwa hili tatizo (NOD32 kernel problem). NOD32 Anti-Virus nikaitowa na kuiweka hiyo Avira Anti-Virus na mpaka hii leo huu sasa unafika mwaka 2 sina matatizo na mambo ya Virus nashukuru Avira anti-Virus inanisaidia sana kulinda Computer yangu.

Sasa wewe unayeisifia Norton Anti-Virus je umeshaifanyia Uchunguzi? Je hiyo NortonAnti-Virus inakulinda kweli? Soma hapa kuhusu Norton 2010 is it a Memory Hog? bonyeza hapa utapata jibu it is that Norton AntiVirus hog memory - Google Search

Kama unajuwa kiingereza utapata jibu kuhusu hiyo Anti-Virus yako Norton inavyokula Memory ndani ya Computer yako.

Chanzo http://answers.yahoo.com/question/in...7181458AAAuMll

Mkuu nadhani ujanielewa,sijakubishia maelezo yako kwamba Norton haifai,ndio maana nikasema siku nitakapohitaji kununua anti virus tena nitachukua the best iliokuwa suggested hapa.

Na kitu kingine ndio natumia niko ok nayo,sasa naona mkuu umepata jazba kama sales person wa kampuni fulani unajaribu kuuza product yako.

Maelezo yako ya uhakika mkuu yamekwenda shule asante tena kwa kutuelewesha hipi inafaa.
 
bit-defender.jpg
 
Mkuu ni jina kubwa lakini haina Mpango wowote ule nakushauri tumia avira Antivir Personal au Avira Premium Security Suite Kiboko ya anti-Virus zote.

Si kweli mkuu. Nimetumia zote hizo unasema. Kwa sasa natumia KIS 2010 lakini bado bitdefender 2010 ni kiboko. Haiachi kitu nyuma ya pazia
 
Kwa mtazamo wangu katika IT hakuna product specific unayweza kusema ni best solution. Inategemea na specific funactional requirement unazotaka, Uwezo/capacity (RAM, CPU, etc) ya mashine husika , competency ya muhusika , User Interface, etc

Mifano Michache ni
Macfeee, Norton ni brand zimekuwepo muda mrefu na zimejijenga jina. lakini tatizo zinaweza kuonekana ni heavyweight hasa ukiweka kwenye pc yenye capacity ndogo au au ukifanya tunning vibaya Mfano umetune antivirus ifanye scanning ya ports za internt 24 hrs a day hata muda amabao mashine yako haiko conneted na internet. Hizi ni nzuri zinahitaji right tunnning. Vile vile soma maelekezo sababu kuna Norton na MAcfee na Av nyingine wana product specif kwa enterprise watu wanafanya kosa kuweka producy hizi kwenye just single pc

Tatizo la Norton hata kapersky inaweza kuwa User interface yake haiko friendly inaweza kuonekana haiko friendly hasa kwa mtumiaji ambayye sio advanced user.

Kama pc yako itakuwa connected na internet mara nyingi utakuta AV fulani infaa zaidi na kama sio kila mara pc iko kenye internete itakuwa ni AV nyingine. Kingine ni mtumiaji kujua REALISTIC THREAT kubwa inaona inatoka wapi.kwenye flush disk, external drive, internet.

Kitu kingine ambaho wataalamu wanasema ni weakness hasa ya kapersky ni kuwa na FALSE POSITIVE nyingi. Hii nimeona pia sababu ilikuwa ina detect key generator ya kama virus. So kwa mtumiaji asiye zoefu anaweza kudhani kapersky ni bora sana just becuse imdetect kitu ambacho si kweli ni virus.

Jibu Langu ni kuwa kabla ya kujua AV gani inakufaa au ni bomba kwako identify Threat kutokana na matumizi yako. dont be general. user tofauti tunakuwa na threat tofauti na hivyo kuhitaji AV tofauti .

Binafsi natumia Avast

Mi ndiyo maana huwa nakukubali mtazamaji, sema tu unapenda sana kiingereza,jitahidi kiingereza uwe unaweka kwenye mabano. hata mimi nimewahi kupata taabu sana mambo haya. Mara ya mwisho nilijaribu mse, lakini ilishindwa kabisa kutoa virus 6, nilifunga avast, cha ajabu wakanaswa bila kucheleweshwa. najua avast ni yebo yebo sana na weakness kadhaa ingawa mwisho wa siku tatizo lipo kwa sisi watumiaji kutokujua ''virus management''.

lakini jibu lako ndilo sahihi, mtu anaweza kukupiga maswali akitaka ufafanuzi.

Main | maajabu ya maji
 
mi natumia Rising kwa miaka 2 mfululizo sasa, nimeipenda sana. Awali nilitumia Kaspersky na Norton ziliifanya computer slow. Rising virus havipenji kabisa ilimradi una firewall yake.

da umenikumbusha haka kadude nilikuwa nikikatumia kabla cjaahamia Linux rasmi na kalikuwa kananisaidia enzi hizo
 
Back
Top Bottom