The battalions of idiocy are on the march in Tanzania, old haven of global intellectuals

Ukisoma au kuambiwa kitu, kucheka lazima uilewe lugha sawasawa. Ulimwengu katumia rhetoric language kutusifia huku akitukana
They are legion in our midst, since we diluted our education by building brick and mortar structures without trained teachers or proper books. These anti-knowledge militants have effectively banished books from their lives, having discovered, no doubt, that books have the nasty habit of depriving us of ur boeloved ignorance.
 
Haijanishekesha hata kidogo, Nimeendelea kuumia moyo, nimepata uchungu sana. Wakati Mtoto anajaribu ku- PROVE kile alichokuwa anabishana na mtoto mwenzake, GHAFLA ANAONA KUNDI LINALOTAKA KUMWANGAMIZA, Kwa hali hii tuweza vipi kukuza UDADISI hapa nchini?

ANY WAY, HATA IVO, TRUTH HAS BEEN REVEALED. No one will entrust rumors anymore!!



Kinachovunja mbavu hapa nadhani ni taarifa yote, kwamba wakati dunia ipo kwenye high level ya technology, bado kuna watu wanakwenda kwenye ndumba na vikombe??? wakati taifa liliandikwa sifa nzuri kwenye ngazi za kimataifa sasa CNN inatuandika misurur mirefu kule samunge, wakati wenzetu wanajenga flyovers kukubaliana na hali ya maendeleo ya wanadamu sisi tunazungumzia utaalamu wa misukule wa kufufua wafu.
hii kweli ni kichekesho na ni kichekesho cha uchungu si cha furaha.
kinachotuponza ni pilau, kofia na elfu kidogo wakati wa kampeni za uchaguzi.
 
mkuu english yako nayo imekaa Ki-Mlugo Mlugo vile. Hebu isome vizuri post yako

Jomba hii jamaa usiilinganishe na Mlugaluga aisee! Kiko njema ila ulimi umeteleza tu kwenye "a big words" vinginevyo jamaa anaweza! Mimi namwunga mkono kwenye hiyo hoja yake. Uli katumia maneno magumu mno mpaka unahisi ukakasi!
 
MUME ANAMPIGA MKEWE, AKATOKEA JIRANI....

JIRANI: "Aaaah, mke hapigwi bwana...."
MKE..."Tafadhali mume wangu msikilize jirani anachosema..."

MUME: "Kwanini nisimpige?!?!?!"
JIRANI..."Usimpige, we muolee mke wa pili....."

MKE: "Aaaaa mume wangu we nipige 2, achana na huyo chizi...."
 
Kwa nini waliokwenda Samunge kule kwa babu bado ni VIONGOZI wakubwa tu katika jamii yetu? Kwa nini watoto wetu kwa maelfu wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika lakini wanafaulu kwenda kidato cha kwanza? Kwa nini CCM wanauza na kununua kura na Mwenyekiti wao anakosa la kufanya? Kwa nini mtoto anakojolea Quran wakubwa wanaingia mabarabarani na kuchoma makanisa?

Tanzania ushirikina unafanya kazi!
 
Tanzania haijawahi kupewa sifa nzuri popote pale duniani!! wanasiasa uchwara wa Tanzania ndo huja kutudanganya kuwa Mataifa mbalimbali yanatusifu!! LIIAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAR!!
Sifa zote tunazopewa huko nje tangu enzi za nyerere ni zile zinazofanana na hiyo ya CNN!
Hebu jamani ondokeni kwenye hiyo nusu kaputi ya kuvishwa ukoka kuwa mna amani; wenye upendo, wakarimu and all those bullshits siadi by our politicians!!
Mtampinga Julius mpaka povu liwatoke, ukweli unabaki kuwa enzi zile Tanzania ilikuwa na binadamu wenye thamani kuwavuta kina Che, siku hizi TZ ni mbuga kubwa ya kuvuna wanyama na maliasiri.
 
Nakubaliana na wanaosema hapana pa kuvunja MBAVU kwenye makala ya Jenerali. Anaonesha wapi tunatoka (enzi hizo) kwenye utukufu wa fikra, na chemchemi ya mawazo na tafakari za kina, kwenye utukufu, sifa na heshima ya Taifa lililosimamia na kupigania haki utu, usawa na haki. Tulikuwa Taifa kiongozi (pamoja na umaskini wetu) kwenye masuala ya kisomi na kitaaluma (walau Barani Afrika), tulikuwa Taifa kiongozi katika siasa za kimataifa zilizowahusu wanyonge. Tulikuwa Taifa la watu wanaojiamini, wenye dira inayoeleweka na kuelezeka. Tulikuwa Mboni na Taifa la kupigiwa mfano. Anachosema, haya hayakujileta, yalijengwa na kutengenezwa. Na Ndipo UONGOZI wa kisiasa unapoingia - katika kuweka misingi ya haya yaliyopita. Ya leo ni kinyume cha ya jana - tu kinyume cha tumaini lililojengeka miongoni mwetu na watu wengine waliotutazama na kutamani wawe kama sisi. Imekuwaje tumefika hapa - Jenerali anasema - tunajenga majengo ya elimu pasi kutoa elimu - shule na vyuo vikuu visivyo na vitabu na waalimu walioandaliwa kwa kazi husika. Tunawekeza kwenye majengo (yanayong'ara na kumeta meta kama pale UDOM - jengo zuri la Maktaba lakini halina vitabu). Tumekuwa taifa la kibabaishaji, tunajidanganya. Zamani tukisifiwa na wengine, siku hizi tunajisifu wenyewe kwa sababu hatuna cha kusifiwa... Tunatokaje hapo ... Nahnai ni swali muhimu na la msingi ... ni dhahiri hatuwezi kuendekeza kinachotokea sasa.
 
What makes the situation hopeless is that political leaders, both ruling and aspiring for ruling, are not pointing out these issues as vividly as Generali, and none of them is even trying to give strategies for reconstruction of a better Tanzania.

We must make our presidential aspirants speak on what exactly they will do to reconstruct our education system, reconstruct taxation system and what they will do to fight corruption and injustice. We should not fall for promises that have no explanation on how they will be achieved.
 
zaidi ya kuelezea ukweli, sijapaona panapovunja mbavu. Tusaidiane kupatafuta

panapovunja mbavu nafikiri ni pale anaposema elimu watu wanayopewa ni ya kijinga yenye kupotosha ukweli ndiyo maana baadhi ya watu wameamua kuacha vitabu na kuanza kuvijaribu kama wanayoambiwa ni kweli. kwa mfano kijana aliambiwa amefundishwa yeye atakayekojolea Qoran atageuka kuwa nyoka kijana mwenzake akakojolea kujaribu kuthibitisha endapo mananeo hayo ni kweli na kugundua kuwa ni uongo? teh teh teh

kingine anasema kuna majeshi ya miungu ambayo yanafanya lolote kwa madai ya kumtetea mungu wao
 
there is no way out to look for an enemy but we have to turn back and starts rather than go to know where,let us begining to cuer primary problem and that is culture accompanied by relevant education and also faith(with the exception of christianity and muslims) once we reach there,the secondary problem will be cured automatically from secondary.from there on our mind set would be bright,right?
 
Muonekano wa taifa ni matokeo ya falsafa inayoliongoza taifa husika. Hii ni kwa sababu elimu,biashara na mambo ya kijamii huongozwa na falsafa ya Taifa. mfano ujamaa. Katika uongozi wa mwalimu J.K Nyerere tuliweza kupata sifa nzuri kama alivyoainisha Jenerali kwa sababu Mwalimu mwenyewe alikuwa muumini haswa wa falsafa aliyotumia kuiongoza nchi (ujamaa) na alifanikiwa pia kuwafanya wananchi wote wawe waumini wa falsafa hiyo kwa kiwango kikubwa. kwa msingi huo kila kilichofanyika katika taifa kiliakisi falsafa ya taifa letu.labda nionyeshe namna ambavyo falsafa ya taifa inaathiri/ inaongoza elimu ya taifa husika.kutoka kwenye falsafa ya taifa ndiko ambapo sera ya taifa ya elimu inachukuliwa,kutoka kwenye sera tunatengeneza mitaala, kutoka kwenye mitaala tunatengeneza scheme of work kutoka hapo mwalimu anatengeneza andalio la somo na kwenda kulifundisha darasani. Ni kwa maana hii kwamba lazima anachofunzwa mwanafunzi darasani kitabeba malengo yaliyopo ndani ya falsafa ya taifa. Falsafa iliyotumika kipindi cha nyerere (ujamaa) ndiyo inayotumika hadi leo kwenye elimu ambapo tayari taifa halipo tena kwenye ujamaa.hii ni sababu kuu ya wahitimu wa kitanzania kushindwa kwenda sawa na wahitmu wa nchi nyingine ( mfano mzuri ni kwenye hili soko la ajira la jumuiya ya afrika mashariki) kwa sababu wameandaliwa kupitia falsafa isiyotumika popote kwa sasa na wangefaa zaidi kwenye ulimwengu ule wa ujamaa lakini huu siyo wa ujamaa lazima washindwe. Tatizo ninaamini lipo kwa viongozi wetu, hawajaona kwamba tunahitaji kwa hakika falsafa ya kutuongoza kama taifa ili tuweze kuenenda sawa na mabadiliko ya dunia yanavyokwenda. Sadly enough we are prepared to consume what we don't produce and produce what we don't consume. kwenye technolojia tuna mafundi wa kurekebisha vifaa vilivyokwisha kuharibika lakini hatuna wa kubuni na kutengeneza vifaa vipya vitaavyouzwa ndani na nje ya nchi yetu. naamini uongozi kwa sasa ni ajira ya kumwezesha mtu na familia yake kuongeza kipato na siyo kufikiri kuhusu kesho bora ya Tanzania..mpaka lini tutaendelea kuwa omba omba? mpaka lini nchi hii itabaki kwenye giza la ujinga, umaskini na maradhi? kiongozi ambaye hajui kwa nini leo nchi hii ni maskini pamoja na kuwa na utitiri wa raslimali hawezi kujibu haya maswali kwa vitendo, hawezi pia kututoa hapa na kutupa japo hatua moja toka kwenye umaskini. Ee Mungu inua maono katika kizazi hiki tuzijue kwa hakika sababu za wewe kuweka raslimali hizi hapa kwetu na wala siyo kwa hao wanaozifaidi sasa,tuinulie viongozi wenye kuwa na maono ya kututoa hapa...so sad we real need a way out of this.
 
Ukweli mchungu. Kama Taifa, we need a fresh start. We need to redefine our direction and how to get there. Sijaona uongozi na systems tulizo nazo zikiweza kutupeleka tunakotakiwa kwenda. Taifa letu limekuwa kama mtu asiyejua anapokwenda.
 
Shakespeare again, what kind of english is this? who does use this obscurantism in regular convarsation? Good writter never use a big words to confuse his readers
Nothing fan at all, tired with dictionary language
Ooh poor guy, even the word obscure sends you to a lexicon. We have a big problem.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom