The Article of Union between the Republic of Tanganyika and the Peoples Republic of Zanzibar

Tunaomba Judgment ya Mahakama ya Zanzibar kuhusu ombi la kuwasilishwa kwa hati za Muungano mahakamani. Junius tubandikie hapa tafadhali.
 
Mwanakijiji swala langu kubwa ni kuwa kwanini unajadiliwa? je ni watu wachache au wengi wanaoleta haya mazungumzo wakiwa na nia zao binafsi au ni majority?

Juzi wawakilishi wetu, wabunge, walizima kabisa issue za Richmond. Mimi na wewe leo ni mashahidi kuwa kuna mambo mengi sana ndani ya bunge hatukubaliani nayo.Kwa hiyo kwa nchi zetu hizi kusema kuwa kuna wawakilishi hakuufanyi muungano kuwa halali. wawakilishi is just a paint kusema wananchi wote walihusika.

kama wawakilishi hao wakitunga sheria (pamoja na ufisadi au madhaifu yao) sheria hizo zinakuwa halali na tunatakiwa kuzitii kwanini basi linapokuja suala la muungano tusione kuwa ni halali? As a matter of fact, it can easily be argued kwamba bunge la wakati ule lilikuwa na uhalali zaidi na uzalendo zaidi kuliko hawa wenzetu wa sasa.

Swala la pili ni kuwa lets say nikakubaliana na wewe kuwa wawakilishi wanafanya kitu kuwa halali, then, swali la pili je waliwasiliana na wananchi kwa kiasi gani?

kwa kiasi chochote kile wao ni wawakilishi; hakuna ulazima wa kuhamisha magoli kwa wakati huu. Kwamba Muungano ni halali kisheria hilo sina shaka nalo. Kwamba baadhi ya vitu vingefanywa tofauti hilo linaweza kujadilika lakini haliondoi uhalali wa muungano. Kwa mfano watu wawili wanapofunga ndoa kwa hiari yao uhalali wa ndoa yao haufutiki ati kwa sababu wazazi hawajaulizwa au kutoa baraka zao! Lakini vile vile tunajua ni vizuri kama pande mbili za familia zinahusishwa katika harusi n.k Hata hivyo, uhalali wa ndoa upo.
Umeona Obama aklivyohangaika kutoka meeting moja kwenda nyingine, kutoka chuo hiki kwenda kile kuinadi policy yake ya health care. Je wawakilishi walifanya hivyo waliwaelimisha wananchi kiasi cha kutosha na hata kupata maoni yao? If not so then wananchi walifanywa wanyama wasio na value yoyote??, na serikali za kiafrika nyingi kiwamo ya Nyerere ambaye unajaribu kutaka kumtetea walitufanya hivi ni bahati mbaya sana kuwa wengine hawajaliona hili

Jamani kuna mambo ni lazima tuyaangalia in historical context; hivi wakoloni walipokuja kututawala walijipitisha kwa kiasi gani kwa wananchi ili tuwaelewe na kuwakubalia? Waliomba maoni ya nani juu ya kuundwa kwa nchi ya Tanganyika? Wajerumaini walipofanya Berlin Conference na kuigawa Afrika kama kugawana pizza ni mwafrika gani aliulizwa? Lakini tumekubali kuwa mipaka waliyoiweka na miundo mbinu yake ilikuwa halali na hatuihoji? Gavana wa Mwingireza alipoigawa Tanganyika au Wajerumani walipoinunua Mafia au Bagamoyo toka kwa Sultani tunasema ni halali.. Nyerere kukaa na Karume na kuamua kuunganisha wananchi wao, tunasema "it was wrong!!"..

Kama nchi yetu sote kwanini maamuzi hayawi ya sisi wote? na kama kuna wawakilishi then kwanini hawawasiliani na wapiga kura wao? najua unaweza kusema wawakilishi "si mliwachagua wenyewe" no matter mlimchagua au hamkumchagua swala ni kuwa wananchi wengi hawakujua kuhusu hii issue, that alone is a big mistake, swala la kwa kwanini mliwachagua is another long agenda yenye sababu nyingi, moja wapo kubwa ni nini nguvu ya wawakilishi? akina Kilango bungeni yes wanasema kwa nguvu; kiasi gani as individual ana nguvu kufanya vitu viende au visiende?

Demokrasia ni pamoja na kuamini kuwa wawakilishi wamechaguliwa na wananchi kuwakilisha wananchi. Kama wananchi wanaona wawakilishi wao wanafanya kitu ambacho hawakubaliani nacho demokrasia inawaita wananchi kuwaondoa wawakilishi hao kwenye sanduku la kura. Lakini, haiwezekani kila jambo moja basi wabunge waende kuuliza. Jambo moja tunalosahau ni kuwa TAnganyika na suala la Muungano lilikuwa halina utata. Tanganyika na hata Zanzibar (ASP na TANU) viliamini katika Umoja wa Afrika.

Sisi Tanganyika hatukuwa na tatizo lolote katika masuala ya Muungano tuliamini katika Muungano, itikadi yetu ilijengwa katika kuunganisha bara la Afrika. Hata kama wangewauliza watu, wakati ule kura nyingi ingekubaliana na sentiments za wakati ule. Kilichofanyika kilikuwa ni natural progression of an ideological trajectory of pan-africanism.
Hoja yangu ni kuwa Up to this point (kwa Imani) muungano ni halali, ninachofanya ni kupata nguvu na supportive argument ya kujiaminisha ninachokiamini, na ninashtuka ninapoona watanzania wenzangu tulioungana nao wanasema kuwa muungano si halali, lazima nishtuke, nini kinaendelea , kama sote tu family, why on earth other people questioning our union? mpaka sasa hizi bado sijapata strong reasons za kufanya imani yangu iwe thabiti.

Waberoya, tatizo hapa kuna hoja mbili ambazo wengi wetu hawajakaa chini kuzifikiria kwa makini. Kuna suala la uhalali wa Muungano, na kuna suala la utekelezaji wa Muungano. Umetolea mfano Obama; Juzi Gavana wa Arizona ametia sahihi sheria ya kuharamisha uwepo wa wahamiaji haramu na kuruhusu polisi wa Arizona kuweza kuwakatia mbaroni wahamiaji haramu. Hata hivyo suala la uhamiaji ni suala la Federal Gvt; Obama ameagiza Justice dept kupitia sheria hiyo na nina uhakika itapelekwa kwenye mahakama kuu (supreme court) na kuonekana ni kinyume cha Katiba na kufutwa! Baada ya kupitisha sheria ya mambo ya afya, serikali zaidi ya 30 za majimbo zimeamua kushtaki sheria hiyo kuwa inaingilia haki za Majimbo. Yote hayo yataamuliwa mahakamani lakini hayahoji uhalali wa Muungano wa Marekani.

Sisi katika ufinyu wetu wa kufikiria tunapokutana na matatizo yautekelezaji wa Muungano tunakimbilia "tuvunje tu yaishe".. tukisema kwanini tunaambiwa " kwa sababu una kero"!! Haya ni majibu ya watu wasiofikiria. Inanisikitisha wakati mwingine kwa sababu our collective reasoning as I've mentioned somewhere else is mediocre and pathetic to say the least. NI lazima kwanza tukubali principle kuwa:

. Muungano ni halali
. Muungano ni wa nchi uliounda taifa moja
. Muungano ni wa kulindwa na kutetewa dhidi ya maadui wa ndani na wa nje (tukumbuke kuwa hakuna kitu kitakachowafurahisha mahasimu wa waafrika kama kuona jaribio pekee la kuunganisha afrika likivunjika wakati wao Europe na kwingine wanajitahidi kuungana zaidi na zaidi)
. Matatizo ya Muungano yanatatulika kirahisi tu (kama tungepata watu wenye akili timamu za kutatua matatizo zaidi ya porojo!)

Note that I do believe our union is genuine,but believing is not necessary the truth!!

The truths stands objectively alone; it doesn't matter whether u believe it or not.

Akija mtu na hoja na kuthibitisha kuwa ni halali, then wanaopiga kelele kuhusu muungano ni wangapi? kama wachache leave them! kama wengi then something must be wrong somewhere?

Labda tatizo haliko "somewhere".. may be what is wrong is with the many people wanaopiga kelele kwa sababu hawajafikiria kiundani na kiakili. Kupiga kelele kwa watu wengi hakufanyi hoja zao kuwa ni halali au zina maslahi ya ukweli. Sometimes the minority hold the key to the defense of truth. I'm not a follower of many who shouts but the silent majority who think before they speak.
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________

Jina kamili la
Katiba tarehe ya
kuanza kutumika
na matumizi ya
Katiba hii.
Sheria ya 1985
Na.15 ib.52
152.-(1) Jina kamili la Katiba ya Jamhuri ya Muugano wa
Tanzania, ya mwaka 1977.
(2) Katiba hii itaanza kutumika tarehe 26 Aprili, 1977.
(3) Katiba hii itatumika Tanzania Bara na vile vile
Tanzania Visiwani.
_________

(Imetajwa katika ibara ya 4)
Mambo ya Muungano
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo.

NYONGEZA YA PILI
___________
ORODHA YA KWANZA
(Imetajwa katika ibara ya 98 (1)(a))
(Sheria ambazo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na
heluthi mbili ya Wabunge wote).
Sura ya 500,
Sheria ya
kluthibitisha
Tanganyika
kuwa Jamhuri
ya mwaka 1962
Ibara ya 3, 17,18, 23 na 26
Sura ya 508,
Sheria ya
Utumishi katika
Idara ya
Mahakama ya
mwaka 1962
Ibara ya 22, 23, na 24
Sura ya 509,
Sheria ya
Utumishi
Serikalini ya
mwaka 1962
Ibara ya 22, 23, na 24.
Sura ya 512,
Sheria ya Uraia,
ya mwaka 1961
Sheria yote
Sura ya 557,
Sheria ya
Kuthibitisha
Mapatano ya
Muungano wa
Tanganyika na
Zanzibar ya
mwaka 1964
Sheria yote.
ORODHA YA PILI
(Imetajwa katika ibara 98 (1) (b))
Mambo ambayo mabadiliko yake yahitaji kuungwa mkono na
theluthi mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Bara na theluthi
mbili ya Wabunge wote kutoka Tanzania Visiwani.
1. Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano.
2. Kuwapo kwa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano.
3. Madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
4. Kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.
5. Madaraka ya Serikali ya Zanzibar.
6. Mahakama Kuu ya Zanzibar.
7. Orodha ya Mambo ya Muungano.
 
kama wawakilishi hao wakitunga sheria (pamoja na ufisadi au madhaifu yao) sheria hizo zinakuwa halali na tunatakiwa kuzitii kwanini basi linapokuja suala la muungano tusione kuwa ni halali? As a matter of fact, it can easily be argued kwamba bunge la wakati ule lilikuwa na uhalali zaidi na uzalendo zaidi kuliko hawa wenzetu wa sasa.

kwa kiasi chochote kile wao ni wawakilishi; hakuna ulazima wa kuhamisha magoli kwa wakati huu. Kwamba Muungano ni halali kisheria hilo sina shaka nalo. Kwamba baadhi ya vitu vingefanywa tofauti hilo linaweza kujadilika lakini haliondoi uhalali wa muungano. Kwa mfano watu wawili wanapofunga ndoa kwa hiari yao uhalali wa ndoa yao haufutiki ati kwa sababu wazazi hawajaulizwa au kutoa baraka zao! Lakini vile vile tunajua ni vizuri kama pande mbili za familia zinahusishwa katika harusi n.k Hata hivyo, uhalali wa ndoa upo.

Jamani kuna mambo ni lazima tuyaangalia in historical context; hivi wakoloni walipokuja kututawala walijipitisha kwa kiasi gani kwa wananchi ili tuwaelewe na kuwakubalia? Waliomba maoni ya nani juu ya kuundwa kwa nchi ya Tanganyika? Wajerumaini walipofanya Berlin Conference na kuigawa Afrika kama kugawana pizza ni mwafrika gani aliulizwa? Lakini tumekubali kuwa mipaka waliyoiweka na miundo mbinu yake ilikuwa halali na hatuihoji? Gavana wa Mwingireza alipoigawa Tanganyika au Wajerumani walipoinunua Mafia au Bagamoyo toka kwa Sultani tunasema ni halali.. Nyerere kukaa na Karume na kuamua kuunganisha wananchi wao, tunasema "it was wrong!!"..

Demokrasia ni pamoja na kuamini kuwa wawakilishi wamechaguliwa na wananchi kuwakilisha wananchi. Kama wananchi wanaona wawakilishi wao wanafanya kitu ambacho hawakubaliani nacho demokrasia inawaita wananchi kuwaondoa wawakilishi hao kwenye sanduku la kura. Lakini, haiwezekani kila jambo moja basi wabunge waende kuuliza. Jambo moja tunalosahau ni kuwa TAnganyika na suala la Muungano lilikuwa halina utata. Tanganyika na hata Zanzibar (ASP na TANU) viliamini katika Umoja wa Afrika.

Sisi Tanganyika hatukuwa na tatizo lolote katika masuala ya Muungano tuliamini katika Muungano, itikadi yetu ilijengwa katika kuunganisha bara la Afrika. Hata kama wangewauliza watu, wakati ule kura nyingi ingekubaliana na sentiments za wakati ule. Kilichofanyika kilikuwa ni natural progression of an ideological trajectory of pan-africanism.

Waberoya, tatizo hapa kuna hoja mbili ambazo wengi wetu hawajakaa chini kuzifikiria kwa makini. Kuna suala la uhalali wa Muungano, na kuna suala la utekelezaji wa Muungano. Umetolea mfano Obama; Juzi Gavana wa Arizona ametia sahihi sheria ya kuharamisha uwepo wa wahamiaji haramu na kuruhusu polisi wa Arizona kuweza kuwakatia mbaroni wahamiaji haramu. Hata hivyo suala la uhamiaji ni suala la Federal Gvt; Obama ameagiza Justice dept kupitia sheria hiyo na nina uhakika itapelekwa kwenye mahakama kuu (supreme court) na kuonekana ni kinyume cha Katiba na kufutwa! Baada ya kupitisha sheria ya mambo ya afya, serikali zaidi ya 30 za majimbo zimeamua kushtaki sheria hiyo kuwa inaingilia haki za Majimbo. Yote hayo yataamuliwa mahakamani lakini hayahoji uhalali wa Muungano wa Marekani.

Sisi katika ufinyu wetu wa kufikiria tunapokutana na matatizo yautekelezaji wa Muungano tunakimbilia "tuvunje tu yaishe".. tukisema kwanini tunaambiwa " kwa sababu una kero"!! Haya ni majibu ya watu wasiofikiria. Inanisikitisha wakati mwingine kwa sababu our collective reasoning as I've mentioned somewhere else is mediocre and pathetic to say the least. NI lazima kwanza tukubali principle kuwa:

. Muungano ni halali
. Muungano ni wa nchi uliounda taifa moja
. Muungano ni wa kulindwa na kutetewa dhidi ya maadui wa ndani na wa nje (tukumbuke kuwa hakuna kitu kitakachowafurahisha mahasimu wa waafrika kama kuona jaribio pekee la kuunganisha afrika likivunjika wakati wao Europe na kwingine wanajitahidi kuungana zaidi na zaidi)
. Matatizo ya Muungano yanatatulika kirahisi tu (kama tungepata watu wenye akili timamu za kutatua matatizo zaidi ya porojo!)

The truths stands objectively alone; it doesn't matter whether u believe it or not.

Labda tatizo haliko "somewhere".. may be what is wrong is with the many people wanaopiga kelele kwa sababu hawajafikiria kiundani na kiakili. Kupiga kelele kwa watu wengi hakufanyi hoja zao kuwa ni halali au zina maslahi ya ukweli. Sometimes the minority hold the key to the defense of truth. I'm not a follower of many who shouts but the silent majority who think before they speak.

Thanks, now as the heat is high,

unasemaje wazanzibar wakisema wajiondoe kwenye muungano?
 
SURA YA PILI
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
RAIS
33.Rais wa Jamhuri ya Muungano.
34.Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.
35.Utekelezaji wa shughuli za Serikali.
36.Mamlaka ya kuanzisha na kuwateua watu wa kushika nafasi za madaraka.
37.Utekelezaji wa kazi na shughuli za Rais n.k.
38.Uchaguzi wa Rais.
39.Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais.
40.Haki ya kuchaguliwa tena.
41.Utaratibu wa uchaguzi wa Rais.
42.Wakati na muda wa kushika madaraka ya Rais.
43.Masharti ya kazi ya Rais.

44.Madaraka ya kutangaza vita.
45.Uwezo wa kutoa msamaha.
46.Kinga dhidi ya mashtaka na madai.
46A. Bunge laweza kumshtaki Rais.
46B. Wajibu wa viongozi Wakuu wa vyombo vya Mamlaka ya Utendaji
kudumisha Muungano.
SEHEMU YA PILI
MAKAMU WA RAIS
47.Makamu mmoja wa Rais, kazi na Mamlaka yake.
48.Wakati wa Makamu wa Rais kushika madaraka.
49.Kiapo cha Makamu wa Rais.
50.Muda wa Makamu wa Rais kushika Madaraka.
SEHEMU YA TATU
WAZIRI MKUU, BARAZA LA
MAWAZIRI NA SERIKALI
51.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
52.Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu.
53.Uwajibikaji wa serikali.
Baraza la Mawaziri na Serikali
53A. Kura ya kutokuwa na imani.
54.Baraza la Mawaziri.
55.Uteuzi wa Mawaziri.
56.Kiapo cha Mawaziri na Naibu Mawaziri.
57. Wakati na muda wa Mawaziri kushika madaraka.
58.Masharti ya kazi ya Mawaziri.
59.Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
60.Katibu wa Baraza la Mawa ziri.
61.Wakuu wa Mikoa.

SURA YA TATU
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA

BUNGE
62.Bunge.
63.Madaraka ya Bunge.
64.Madaraka ya kutunga Sheria.
65.Muda wa Bunge.

SEHEMU YA PILI
WABUNGE, WILAYA ZA UCHAGUZI NA UCHAGUZI
WA WABUNGE
66.Wabunge.
67.Sifa za mtu kuwa Mbunge.
68.Kiapo cha Wabunge.
69.Tamko rasmi la Wabunge kuhusu maadili ya Viongozi.
70.Wabunge kutoa taarifa ya mali.
71.Muda wa Wabunge kushika madaraka kama Wabunge.
72.Watu wenye madaraka Serikalini kukoma utumishi wanapochaguliwa.
73.Masharti ya kazi ya Wabunge
74.Tume ya Uchaguzi
75.Majimbo ya Uchaguzi.
Uchaguzi na Uteuzi wa Wabunge
76.Uchaguzi katika Majimbo ya Uchaguzi.
77.Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge wa Majimbo ya Uchaguzi.
78.Utaratibu wa Uchaguzi wa Wabunge Wanawake wa kuchaguliwa na Bunge.
79.Utaratibu wa uchaguzi wa Wabunge wa kuchaguliwa na Baraza la
Wawakilishi.
80.[Imefutwa na Sheria Na.4 ya 1992 - ib.27].
81.Utaratibu wa kupendekeza majina ya wagombea uchaguzi wa Wabunge
Wanawake.
82.[Imefutwa na Sheria Na.4 ya 1992 - ib.29].
83.Uamuzi wa suala kama mtu ni Mbunge au sivyo.
SEHEMU YA TATU
UTARATIBU, MADARAKA NA HAKI ZA BUNGE

Spika na Naibu wa spika
84.Spika na Mamlaka yake.
85.Naibu wa Spika.
86.Utaratibu wa kumchagu Spika na Naibu wa Spika.
Ofisi ya Bunge
87.Katibu wa Bunge.
88.Sekretariati ya Bunge.
Utaratibu wa shughuli Bungeni
89.Kanuni za Kudumu za Bunge.
90.Kuitishwa kwa mikutano ya Bunge na kuvunjwa kwa Bunge

91.Rais aweza kulihutubia Bunge.
92.Mikutano ya Bunge.
93.Uongozi wa vikao vya Bunge.
94.Kiwango cha vikao vya Bunge
95.Viti vilivyo wazi katika Bunge.
96.Kamati za Kudumu za Bunge.
Utaratibu wa Kutunga Sheria
97.Namna ya kutumia madaraka ya kutunga sheria.
98.Utaratibu wa kubadilisha Katiba hii na baadhi ya sheria.
99.Utaratibu wa kutunga Sheria kuhusu mambo ya fedha.
Madaraka na Haki za Bunge
100. Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli.
101. Kuhifadhi na kutilia ng uvu uhuru wa majadiliano na wa shughuli.
SURA YA NNE
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR,
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR NA
BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
SEHEMU YA KWANZA
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
NA RAIS WA ZANZIBAR
102. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka yake.
103. Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na madaraka yake.
104. Uchaguzi wa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

SEHEMU YA PILI
BARAZA LA MAPINDUZI LA ZANZIBAR
105. Baraza la Mapinduzi la Zanzibar na Kazi zake.
SEHEMU YA TATU
BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZANZIBAR
106. Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na madaraka ya kutunga Sheria za
Zanzibar.
107. Madaraka ya Baraza la Wawakilishi.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
7
SURA YA TANO
UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO,
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO, TUME
YA KUAJIRI YA MAHAKAMA YA TANZANIA BARA,
MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR, MAHAKAMA
YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO NA
MAHAKAMA MAALUM YA KATIBA YA
JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
UTOAJI HAKI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO
107A. Mamlaka ya Utoaji Haki.
107B. Uhuru wa Mahakama.
SEHEMU YA PILI
MAHAKAMA KUU YA JAMHURI YA MUUNGANO
108. Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano na Mamlaka yake.
109. Majaji wa Mahakama Kuu na uteuzi wao.
110. Muda wa Majaji wa Mahakama Kuu kushika madaraka.
111. Kiapo cha Majaji.
SEHEMU YA TATU
MADARAKA YA KUAJIRI MAHAKIMU NA WATUMISHI
WENGINE WA MAHAKAMA ZA TANZANIA BARA NA TUME YA
KUAJIRI YA MAHAKAMA
112. Tume ya Kuajiri ya Mahakama.
113. Madaraka ya kuajiri Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama.
113A. Uanachama katika Vyama vya Siasa.
SEHEMU YA NNE
MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR
114. Mahakama Kuu ya Zanzibar.
115. Mamlaka ya Mahakama Kuu ya Zanzibar.
SEHEMU YA TANO
MAHAKAMA YA RUFANI YA JAMHURI YA MUUNGANO
116. Tafsiri.
117. Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano na Madaraka yake.
118. Majaji wa Mahakama ya Rufani na uteuzi wao.
119. Mamlaka ya Majaji wa Mahakama ya Rufani.
 
Thanks, now as the heat is high,

unasemaje wazanzibar wakisema wajiondoe kwenye muungano?

hawawezi!! kwa sababu tukikubali wanaweza itakuwaje kama Kilimanjaro nao wanataka watoke kwenye Muungano (kumbuka kabla ya Tanganyika Kilimanjaro ilikuwa tayari kuwa taifa peke yake!); nini kitazuia haki ya wananchi wa Kagera kujitenga au Mtwara na Lini? Wawaulize wenzao wa Marekani ya kusini ambao walitaka kuvunja muungano wa US!!
 
aha! ha! Mwanakijiji ukiingia kwenye ndoa hamna talaka ? au union ya tanganyika na zanzibar ilibarikiwa " aliyekiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe"? Give me clear logic hapa, kama tulikubali kwa hiyari tuungane, na wananchi wote wakaridhia, na leo wananchi wanaridhia kuwa tujitoe kwenye muungano tatizo ni nini? Kilimanjaro haikuaangana na mikoa mingine kwa mikataba! maana ulishasema mikataba halali, vikao halali viliamua, Kilimanjaro is certainly not fits as example for this. Umetoa mifano kuhusu kusini ya america, hujasema jamhuri ya Soviet!

Imeandikwa wapi na nani kuwa nchi zikiungana kamwe haziwezi kutengana?
 
MMJJ,
Iddi Pandu Hassan, mwanasheria mkuu wa serikali ya mapinduzi zanzibar hakutafuna maneno, aliulizwa mkataba wa muungano akajibu "...hajuwi ulipo...", kwa wa sisi Wazanzibar tunaofahamu siasa za kikwetu huku tumemuelewa. "hajuwi" maana yake "haupo". Itawezekanaje document muhimu kama hiyo Serikali isema haijuwi ilipo, nikukumbushe tu maana ya maneno hayo, wakati muungano huu unaaasisiwa na Nyerere na Karume tu, Wofgang Dourado ndo alikuwa dhamana wa sheria Zanzibar ie AG, aliondoshwa kwa kuonekana "mkorofi", kwa maana hiyo hakuna kumbukumbu yoyote katika ofisi ya mwanasheria mkuu zanzibar, Vuga pale , ambapo mi binafsi nimeshafanya kazi pale, na ni wazi kuwa afisi ile haitajwi kwa chochote cha maana katika mchakato wa muungano huu batili, Afisi ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar ilihusika na masuala ya muungano wakati yalipohojiwa na Mzee Jumbe, na wakati huo Nyerere alimweka Kibaraka wake Jaji Damian Lubuva awe mwanasheria mkuu wa zanzibar(tazama ufisadi wa Nyerere na dhamira yake chafu kwa zanzibar), Mzee Jumbe alipogutuka kuwa Lubuva aliletwa kwa u "shu shu shu" na si mwanasheria, alimfukuza na akamleta mwanasheria wake kutoka Ghana Bashiri Swanzy, ambaye ndiye alieandika petition ya kuundwa kwa serikali tatu zilizom cost Jumbe wadhifa wake. Ni sahihi kabisa kuwa "sijuwi" ya Idd Pandu Hassan kuwa sawa na " hakuna".

Mwanafalsafa1,
Upo bookish sana na hu argue kwa mujibu wa hali halisi ya mambo ilivyo, hakuna aliye against na muungano huu, Wazanzibar sisi hatutimii hata milioni moja, tunajuwana shida zetu na tunajuwa kwa wakati mmoja nini kinatukwaza kwa maendeleo yetu, hii kwasababu tuwachache sana, linaweza kutolewa tangazo la kifo redioni mtu kafa kaskazini Unguja, lakini taarifa zikatakiwa ziwafikie jamaa zake kusini, Mjini Magh, kaskazini na kusini Pemba. Huenda usishangae ikawa tumehusiana sote kwa udugu wa damu hasa na si kwa maeneo. Wala huhitaji kufanya utafiti wa kuzamia saaana kujuwa nini hasa mtazamo wa pamoja wa wazanzibari, nini wanakitaka na nini hawakitaki ni rahisi sana kujuwa mda mfupi tu ukikaa nao pamoja. Hawataki Muundo wa Muungano huu kama ulivyo na si kwamba hawataki kuungana, wamechoshwa na uonevu wa muungano huu, wamechoshwa na utumwa na unyanyasaji wa muungano huu, wamechoshwa na dharau na kejeli na bezo la muungano, huu mpka wanahoji kwani ulikujaje?
Unahoji kura ya maoni, kuwa huna hakika kama ni ya kuamua tunataka au hatutaki muungano, mimi sipo huko na Wazanzibar hawapo huko kabisa. Wanachotaka wapewe fursa ya kuamua kama ni muungano basi wa aina ipi, katika maeneo yepi na pande zote zitafaidika vipi? si uhuni huu uliofanywa na Nyerere na Karume! hawataki hata kuuusikia,basi tu!
Wakati fulani tuliletewa,igizo moja kama la ze comdey, liliitwa "white paper", tukaulizwa masuala kama hayo, ajabu(labda sifahamu utaratibu wa vitu kama vile kwa usahihi) ni kuwa tume ile imeundwa huko huko bara kukusanya maoni ya pande zote mbili kama vile matakwa na mahitaji yao yanafanana. Haikuwa na fursa ya kuwafikia wananchi walengwa hasa na maoni yaliyokusanywa kutoka Zanzibar ni makaratasi yaliyochapwa na usalama wa taifa pale kiswandui eti ndo maoni ya wazanzibar kuwa wanataka muundo wa serikali mbili uendelee, rubbish!
Bado ninaimani na kura ya maoni ya kupima uhalali wa muungano kama vile "ule upuuuzi wa Butiama" mliotuamulia kama tunataka amani au hatutaki, utafikiri ni sisi wenyewe tunaovunja hiyo amani na si watawala wanaolindwa na majeshi ya SMT wanaoleta vurugu hizo kwa kukataa kuheshimu demokrasia ya uchaguzi isichukuwe nafasi yake, haya yote yasingelikuwa kama si SMT kulazimisha kuibakisha CCM madarakani kwa kisingizio cha kulinda muungano ambao hauna mpya kwa zanzibar kwa miaka yote tokea kulazimishwa kwake.

Buchanan,
Nipo katika harakati za kupata kopi ya mwenendo wa kesi na hukumu, nikiipata nitaileta inshalllah.
 
Kwani sultan aliwauliza wazenj kabla ya kuweka mipaka? Kabla ya mapinduz ya Jan 12, 1964i wazenj walipiga kura za maoni?[/QUOTE

Kwani ufisadi unaofanywa sasa uliwahi kuibiwa kutoka nyumbani mwako, mbona unaulani? Si uwache tu?]
 
hawawezi!! kwa sababu tukikubali wanaweza itakuwaje kama Kilimanjaro nao wanataka watoke kwenye Muungano (kumbuka kabla ya Tanganyika Kilimanjaro ilikuwa tayari kuwa taifa peke yake!); nini kitazuia haki ya wananchi wa Kagera kujitenga au Mtwara na Lini? Wawaulize wenzao wa Marekani ya kusini ambao walitaka kuvunja muungano wa US!!

Karume Mkubwa aliwahi kuulizwa swali kama hilo alijibu kwa mkato tu "...Yagujuu..". Pole MMJJ, si wewe ni siasa za ujamaa na kujitegemea hizo zinafanya kazi yake, jibu lako ni sawa na la Nyerere, "...kama hawataki siwalazimishi..", tuliposema hatutaki, mizuka ya kizanaki ikampanda babu wa watu, akasahau kama ulivyosahau wewe kuwa "ni khiyari ivyo.." na "...si lazima..."!, kumbe kwake yeye na kwako wewe "khiyari maana yake lazima".
 
hawawezi!! kwa sababu tukikubali wanaweza itakuwaje kama Kilimanjaro nao wanataka watoke kwenye Muungano (kumbuka kabla ya Tanganyika Kilimanjaro ilikuwa tayari kuwa taifa peke yake!); nini kitazuia haki ya wananchi wa Kagera kujitenga au Mtwara na Lini? Wawaulize wenzao wa Marekani ya kusini ambao walitaka kuvunja muungano wa US!!

Najuwa Mzee Mwanakijiji unatania, au vipi? Naamini hu duni wa mawazo kiasi cha kuwa unachoongelea ni serious. Kufananinisha Kilimanjaro na Zanzibar au kufananisha Muungano wa Marekani na Tanganyika na Zanzibar nchi zilizokuwa Jamuhuri na uanachama wa Umoja wa Mataifa ziwe sawa na States za Marekani. Be Seriuos Man, una watu wengi wanakuaminia usije wapoteza!
 
"WALE WOTE WANAOPIGANIA HAKI WANAPIGANIA VITA VYA HAKI NA WALE WANAOPIGANA VITA KWA LENGO LA KUKANDAMIZA WENZAO,KUWANYANYASA NA KUWATAWALA HAWAPIGANI VITA VYA HAKI" DR Kikwete (tAREHE 25/04/2010)
 
"WALE WOTE WANAOPIGANIA HAKI WANAPIGANIA VITA VYA HAKI NA WALE WANAOPIGANA VITA KWA LENGO LA KUKANDAMIZA WENZAO,KUWANYANYASA NA KUWATAWALA HAWAPIGANI VITA VYA HAKI" DR Kikwete (tAREHE 25/04/2010)

Your quote is absolutely right. But remember that problem is not identifying what is right and what is wrong, it's identifying who stands for what is right and who stands for what is wrong. Also remember the saying "One man's terrorist is another man's freedom fighter" and vise versa. Kwa hiyo hao unao ona wana pigania haki wengine ndiyo wanawaona ndiyo wakadamizaji.
 
Si wanasema kuwa hizi articles hazipo? Mwiba alizipata wapi?

wala siyo siri kama watu wengi wanavyoamini... hivi kuna mtu kawahi kuuliza kama makubaliano hayo hayapo Ikulu ya Dar na Zanzibar? kuna mtu kauliza kama mkataba huo haupo Umoja wa Mataifa? tunaambiwa kuwa mwanasheria mkuu alipoulizwa alisema kuwa yeye hana.. lakini kuna mtu kauliza kama Mwanasheria Mkuu wa Tanzania anao - clue.. na yeye hana!! Mtu mwingine atasema kwa vile wamesema hawana ina maana "haupo"; lakini swali sahihi ni je walitakiwa kuwa navyo!!!?
 
Back
Top Bottom