The Arab spring... Mageuzi ya utawala nchi za kiarabu

nimejifunza kukuingizien vijit siku tukiwatoa madarakan. Hasa we nape
 
Huyu Nnape ni gamba laini lililojificha lakini lenye sumu kali kuliko ya magamba makubwa yaliyowazi. Kijana ana mawazo mufilisi kabisa. Anatutia aibu sana.
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...
Is the change we are seing for better?
Arab Spring Revolution haikutokea Libya na Misri tu, kuna nchi umeziacha - Tunisia, Algeria, Morocco, Yemen na baadhi ya nchi za ghuba - umeziacha kwa makusudi au kwa bahati mbaya? Lakini hata hizo ulizozitaja, ni kuwa baada ya revolution, lazima nchi ipitie katika evolution na hili si jambo la siku moja au mbili. Ni mpaka pale wananchi wote, taifa zima, liwe limeimarisha misingi ya demokrasia, taasisi za kidemokrasia pamoja na utawala wa sheria. Na tusichanganye demokrasia na domokrasia (blah blah blah tupu bila vitendo na matokeo).

Tunachoweza kujifunza kutoka nchi ulizozitaja pamoja na kinachoendelea sasa Ulaya (fuatilia ukuaji wa vijana wenye siasa kali za mirengo yote kutokana na dhiki za maisha, na kumbuka kuwa hata Hitler aliungqa mkono na watu wengi wakati wake). Kumbuka kuwa walioanzisha na wanaoanzisha harakati hizi ni vijana waliokata tamaa na maisha na ambao wamejitolea kuendeleza mapambano hayo. Wanaweza kuuliwa na kuuana wao kwa wao, na pengine wasione mafanikio ya kile wanachopigania leo lakini iko siku matunda ya mapambano yao ya leo yatakuja kufaidisha vizazi vijavyo.

Tusisahau pia kuwa hata jeshi, pamoja na kuvaa magwanda - sio magwanda ya M4C, nieleweke - na wao ni wananchi, ni raia. Viongozi watawatuma jeshi wakaue kwa kisingizio cha kudumisha amani, lakini wakirejea nyumbani watoto wanawalilia njaa, hawana makazi stahiki yao, ndugu zao hawapati elimu, hawana ajira, matibabu, mfumko wa bei, udikteta wa viongozi wao, wizi wa mali za umma...Haya hayapo Tanzania? Siku watakapojiuliza wanaua kwa ajili ya nani, wataungana na wananchi wenzao.

Tunachoweza kujifunza Watanzania, hasa viongozi, na hapa sikusudii watawala tu bali hata wapinzani, ni kuwa wasidharau nguvu ya umma. Ulimwengu umefika pahali leo vitisho haviogopwi tena, hasa kwa watu ambao wameshakata tamaa na maisha, kwa watu wanaoimbiwa amani isiyokuwepo. Amani si kutokuwa na vita tu, na vita si kuingia msituni tu. Amani ni kwa mtu wa kawaida, mvuja jasho, angalau anajua kesho atakula nini, atasoma wapi, atatibiwa wapi; na vita kukosekana kwa hayo yote.

Mungu Ibariki Tanzania
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Kwani Keil kuna mtu au mahali umekatazwa wewe kuweka hayo ya Senegal na Kwingineko? Ugonjwa wa kutaka niwaze kama unavyowaza umeanza lini? Fungua thread nyingine anzisha hoja yako, kama ina mashiko watachangia, hapa kwa mujibu wako, umesema hatuna tulo jifunza kutoka nchi za kiarabu, period!



Huwezi kujifunza kutoka kwa Libya na Egypt.

Funzo kwa watanzania linatakiwa litoke kwa nchi za Afrika ambako angalau tayari kulikuwa na demokrasia na siyo kutoka kwa total dictatorship ya waarabu ambao walikuwa hawajui hata vyama vingi ni nini. Ni sawa na uanze kutuletea stori za Iraq, Libya na Egypt, halafu useme tunajifunza nini?

Mbona huulizi tunajifunza nini kutoka kwenye uchaguzi wa juzi wa Senegal? Kama una nia njema ya kuuliza swali lako weka kitu ambacho kina mazingira sawa na Tanzania. Nyinyi ndio ambao mnakimbilia kwenda kujifunza mambo ya US wakati mambo ya US na Tanzania, ni sawa na giza na mwanga wala havikaribiani na matokeo yake kuliwa kila kukicha.
 
Vipi mmpona na ule ugonjwa wa "Chadema phobia"?

Tumejifunza kuingoa sisiem abao hawana tofauti na watawala wa kiaarabu, mf nepotism

Changes we are seeing is much better than being parmanently enslaved.

Aaah Deo unaonekana we mwanafunzi mzuri..
 
Mwaka 1995, mliwatisha Watanzania kwa kutumia mifano ya Rwanda na sasa mnapanga kutumia mifano ya Uarabuni! Nape, you are so transparent, cheap and empty that anybody can read you like the back of one's hand, pole sana...you can run but rest assured that people like you wont find a place to hide, no, not in our new Land of hope, Tanzania mpya come 2015!

Mwizi hudhani wote wezi!!! Ndo maana mmekua mkiwatisha wapiga kura na kutukna kila anayeleta ukweli JF kwasababu mnaamini katika kutishana?!! Pole sana mtu mzima hatishiwi nyau asilani.
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?
Mhe utaona jinsi gani Mkulu wa Boma asivyo na huruma na wananchi wake, badala ya kupiga mahesabu ya kupunguza matumizi ya serikali yeye anaongeza gharama!!!! Hata kama si mmtaalamu wa uchumi unapoongeza baraza la mawaziri kutoka 50 hadi kufikia 55 hizo gharama unafikiri anazibeba nani???? Kwa mtu mwenye huruma angefikiria kuwa to inflate the cabinet is to over burden the Tanzania tax payers!!! Ukiangalia matumizi ya serikali ni makubwa kuliko matumizi ya kimaendeleo!!! Wakubwa kulithisha utawala kwa watoto wao!!! HAYO NDIYO YAMELETA SHIDA YA VURUGU ZA KIMAGEUZI MIDLE EAST!!

 
Inaonyesha jinsi ulivyohangaishwa na hesabu za kulinganisha wakati unasoma... Wapi katika maneno yangu au swali langu nimeongea habari ya mlinganisho??!!!! Nimeuliza tunajifunza nini, wewe unakurupuka na mlinganisho!!!!!..?!!
Msingi wa hoja yangu hapa ni KUWA TUNAJIFUNZA NINI KUTOKANA NA KILICHO NA KINACHOENDELEA KATIKA NCHI ZA KIARABU. NIKAONYESHA NJIA KWA KUULIZA JE MABADILIKO YALE YAMEZISAIDIA NCHI HIZO KWA MAANA YA KUBORESHA MAISHA YAO? Kama ndio how? Na kama hapana yamekosewa wapi!
Mbona kuna watu wengi wamekujibu unataka nini zaidi au unataka ujibiwe unavyotaka? binafsi nimekusoma ulitegemea kupata majibu gani ambayo yange kufurahisha lakini elewa tu mabadiriko yanakuja na hakuna wa kuya zuia...
Mbona hutoi mfano rwnda inavyo chanja mbunga kimaendeleo...

CCM tumewachokoa.......................................
 
Mwizi hudhani wote wezi!!! Ndo maana mmekua mkiwatisha wapiga kura na kutukna kila anayeleta ukweli JF kwasababu mnaamini katika kutishana?!! Pole sana mtu mzima hatishiwi nyau asilani.

kumbe na wewe ni kiazi kiasi hiki.
 
Last edited by a moderator:
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?

Changes zilizotokea uarabuni hazikuwa na matayarisho na zilisukumwa zaidi na fujo na vurugu. Pengine kwa mazingira yaliyokuwepo, msukumo wao ulikuwa ni kuondoa sura zile zile walizoziona kwa miaka nenda rudi bila kujiuliza itakuwaje baada ya kuwaondoa. Hapa kwetu mambo ni tofauti. Hizi debate zinazoendelea shape our thinking and approach. Sioni kufanana kwake na uarabuni maana hatusukumi mabadiliko kwa mtutu wa bunduki kwahiyo tuna muda wa kutosha wa kujipanga kuchagua nani anayefaa na atakayekuwa bora. Ntawashangaa sana watanzania kama tutafuata nyayo zile za waarabu za kutumia nguvu na fujo kuleta mabadiliko maana hali yetu itakuwa mbaya kuliko wao.
 
Tunajifunza kuwa si vizuri kung'ang'ania madaraka kama wananchi wametuchoka, jitahidi 2015 kutotumia TISS na vyombo vya dola kujitwalia ushindi kama 2010.
 
Nape anayefikiri amesimama aangalie asianguke...changes zinakuja in a different way which could be difficult to resist with all the machineries that we thought could come to our aid in order to prevent changes from happening. The best way ni kutoka kuwa malecturer wa watanzania na kuamua kuwa karibu nao kuwasikiliza na kutimiza yale mnayopaswa kutimiza. Ilivyo sasa wanasiasa na viongozi wengi wanataka tuwapigie magoti kama wao ni miungu watu, na chochote wanachofanya na kusema tukubaliane nacho kama hatuna tena vichwa vya kufikiri. Times change...and that is the old approach. Approach hiyo iliwaangusha USSR na washirika wake. Kwa mtazamo wa karibu ni kitu ambacho hapa hakitawezekana, but who knows what is in the store for us????
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Siku zote mabadiliko huwa yapo na wakati wa mabadiliko ishara zinakuwepo. ukizuia mabadiliko kwa wakati wake kuna siku yatatafutwa kwa lazima na hapo lazima kutakuwa na uvunjifu wa amani. Ukiyakubali kwa wakati wake hapatakuwa na uvunjifu wa amani. Kwa Nchi ulizozitaja muda wa mabadiliko uliko umewadia lakini viongozi hawakuona ishara hadi machafuko yakatokea. Amani ikishavunjwa huwa hairudi kwa siku moja. Ni wa jibu wa kiongozi kuona ishara za nyakati na kupima upepo. Angalia Nchi zingine pia ambazo zimekubali mabadiliko kwa wakati hakuna uvunjifu wa amani.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?

Ni mapema mnoo kuwaza kujifunza kutoka kwa Arab Spring, hizo nchi (Arabs) sasa zipo kwenye kipindi cha mpito.Ukichukulia kwamba viongozi walio watoa walikuwepo madarakani kwa miaka 30 huku wakiunda serikali za kifamilia (nepotism), mfano Egypt. So hizi changamoto wanazopitia sasa sio kitu kibaya, wananchi wapo kwenye harakati za kuondoa mabaki mabaki ya serikali za zamani na kuunda serikali za ukweli na usawa kwa wote.Fall of Gaddafi regime is a special case ilo nawe unalijua, Arabs Spring ya ukweli ni ile ya EGYP na Tunisia. Usitumie issues za Arabs Spring kuwatisha watanzania. Ili kutunza utu wa vizazi vya leo na vijavyo mabadiliko ya kisiasa kwa Tanzania kwa sasa ni ya lazima.

Ungetuambia tunajifunza nini kutokana na mabadiliko yanayoendelea Zambia ningekuelewa. Nitafurahi kusikia unawahamashisha watanzania wajifunze kutokana na mabadiliko ya kisiasa yanayotokea kwa jirani zetu Zambia.
 
Mwaka 1995, mliwatisha Watanzania kwa kutumia mifano ya Rwanda na sasa mnapanga kutumia mifano ya Uarabuni! Nape, you are so transparent, cheap and empty that anybody can read you like the back of one's hand, pole sana...you can run but rest assured that people like you wont find a place to hide, no, not in our new Land of hope, Tanzania mpya come 2015!
Somo tulilojifunza tutalitumia 2015 Tanzania.

Whether its for better or not, time will tell.

Hakuna mema ya Taifa yaliyowahi kutokea kabla ya wananchi kujitolea.

A true lesson to learn: Listen to the people, period.Kama wako wrong ama right, hilo ni juu yao na Taifa lao.
 
O.K, Nape nafikiri unataka mtu wa kukujibu hivi, "Nimejifunza kuwa mkataa pema pabaya panamwita, Libya walimfukuza Gaddafi aliyewapa 3elimu Bure, maji, umeme, nyumba,gharama za Ndoa, mafuta ya magari gei chini kuliko nchi yeyote duniani, ndoa ya mkee mmoja na rate ya taraka kuwa ndogo sana, lakini wao waka mtoa" ukiukata uongozi wa naman hiyo, wewe unatafuta mabaya, mfano hou upo tofauti sana na CCM, yaani Chukua Chako Mapema, wao kila kitu ni deal, Elimu wameua, maisha magumu zaidi (naomba hapa ifahamike kuwa maisha mgumu kwa Bongo ni ya kutengenezwa na CCM), umeme wa kubahatisha, vyeo ni vya urithi, nchi inajali zaidi wanasiasa na wageni kuliko wataalam na wenyeji, inapapalikia vitu visivyo na mshiko kuliko mambo muhimu (rejea issue ya Gender balance na bajeti ya Afya, yote hayo tumetoa kutoka mashirika ya kimataifa, la gender tumefanya la afya tumekataa)

Kwa ujumla swali lako lingekuwa hivi, "Unajufunza nini kwa nchi zilizofanya uchaguzi wa kidemokrasia na wananchi kubadiri chama kilichopo madarakani?" hapo ungeonekana hauko bias, lakini kwa swali lako hilo nafikiri lipeleke kwa wazee wa Dar es salaam, hapa JF umepotea njia.
 
Kwanza nilichokiuliza hapa hakina uhusiano na hoja zako. NIMEULIZA TUNAJIFUNZA NINI KWA KILICHOTOKEA NA KINACHOENDELEA KUTOKEA KATIKA NCHI ZA KIARABU. Sasa mashairi ya chungwa na chenza hapa yanatoka wapi? Kuna wengine tuko nao humu najiuliza HIVI IMETOKEAJE MIE NA WAO TUKO JF PAMOJA??!!!!!
Wewe Nape propoganda zako ni zile za old stone age. Nimesoma gazeti la mwananchi wakikunukuu ukisema eti Mkapa kupanda kizimbani kutoa ushahidi inaonyesha hakuna aliye juu ya sheria. Hivi ni jambo la kweli hilo? Angekuwa amepandishwa kizimbani kwa zile tuhumu za ufisadi zinazomkabili ndio ungeweza kujitapa, lakini kutoa ushahidi?
 
Nini tunajifunza kutokana na kinachoendelea kwenye baadhi ya nchi za kiarabu hasa, Libya, Misri nk. Kabla ya mabadiliko ya tawala zao eg. Gadafi na kinachoendelea baada ya hayo mabadiliko...

Is the change we are seing for better?

Hapo kwenye red ndiko kwenye somo. Tunajifunza kwamba watu wanataka uongozi na sio utawala.

Gadhafi alikuwa mtawala na aligueza Libya kuwa kama duka la familia. Unachoona kinaendelea sasa hivi Libya is a classic example of a nation which for eternity had no strong & effective institutions! Hakuna mtu mwenye akili timamu aliyetegemea kuwa baada ya Ghadafi kuondoka mambo yatakuwa shwari! Hilo haliwezekani kwa sababu hakukuwepo na institutions za kuongoza nchi. It will take time and certainly there will some painful moments ahead.

In my view Libya wamefanya vizuri if you look at all the key factors. Jeshi la Libya or should I say Jeshi la Ghadafi ni maiyolo afadhali hata mgambo wetu wa jiji. Kale kajitabu kake kijani alikokuwa anakaita 'constitution' ni yeye tu (Gadhafi) ndiye alikuwa anaelewa kumeandikwa nini ndani! Kwa kifupi kuondoka kwa Ghadafi Walibya walijikuta kumbe wanaishi kwenye nyumba iliyojengwa na makuti na sio matofali, na upepo mkali ukipita lazima wadhurike. Hivyo kwa sasa inabidi waijenge nyumba upya na ni juu yao kuamua aina ya ukuta wautakao i.e kama watatumia matofali ya kuchoma ya cement/mchanga hilo ni juu yao, lakini walau wamepata fursa ya kujenga.

About Libya.
Kama ulikuwa unafuatilia kwa karibu the demise of Mubarak utakumbuka kwamba takriban siku 18 kabla hajajizulu, Mubarak with the help of his loyal desciples was busy constructing an exist plan. Alibadilisha certain clauses kwenye katiba ya nchi na baadae akakabidhi mikoba. Tofauti na Libya, jeshi la Misri ni top notch! was ready to 'mind the shop'.

Tanzania
Tuna takriban miaka 2 na nusu sasa hadi uchaguzi mkuu (2015). Nyumba yetu haiko imara kabisa, kuta zina nyufa, paa linavuja. Wananchi wamejaribu kuonesha wasiwasi wa kuendelea kuishi ndani ya nyumba hii mbovu lakini hakuna lililofanyika. Ili kujinusuru toka kwenye hatari inayowanyemelea wananchi wameanza kukusanya zana za ujenzi. Wanataka wabomoe kila kinachofanana na utawala na kujenga uongozi maana ni kupitia uongozi wanaweza kuwa na nyumba bora na imara.

Kwa muda huu wa miaka 2 na nusu uliobakia, CCM wangejikita kwenye jambo moja tu - kuweka mazingira mazuri ili 2015 watakapokuwa upande wa pili wa shilingi wasikose oxygen.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom