TGIF: Je unaijua Misingi iliyoliunda Taifa letu?

Mkuu Azimio Jipya,
Katiba ni chombo muhimu sana kwenye Taifa letu; Viongozi wa taifa letu kuanzia Rais mpaka mawaziri wanaapa kuihifadhi na kuilinda katiba, vilevile wanaongoza nchi kwa kufuata katiba. Kwa mantiki hiyo basi kama katiba imeundwa kwa kufuata misingi ya Taifa (rejea posti #57) inamaanisha Serikali yetu inafanya/inatakiwakufanya kazi kwa kuzingatia misingi iliyoainishwa kwenye katiba ambayo ni uhuru, haki, udugu na amani:
Kuna watu wanataka kuingiza kitu ambacho waasisi wa Taifa hili hata hawakukitaja (UTU) kama msingi wa Taifa, hili lilikuja kuingizwa baadae kwenye Azimio la Arusha. Kwangu mimi UTU ni dhana pana sana na kila mtu anaweza kuitafsili atakavyo yeye na ndio mana napata hisia kwamba waasisi wa Taifa hili waliamua kuanisha hayo niliyoyataja hapo juu kwakua yanajieleza yenyewe.

Nyerere kwa maneno yake mwenyewe alidai Azimio la Arusha limeundwa kwa misingi ya UTU, angalia video hii kuanzia dk ya 6:10 Nyerere's Meeting With Tanzania Press Club 1995 Part 5 of 10 - YouTube

Mkuu @ Red. Nafikiri sasa nimekupata.

Wakati wote nilikuwa nawaza Mawazo matatu anapata shida gana na dhana nzima ya UTU! Personaly naona ni dhana nzito na yeneye misingi mizuri kwa ujamla nikiangalia naona misingi ya Taifa ianweza kuanzia hapo.

Hapa nakubalina kuwa ni dhana pana sana na almost very subjective ... kwani inatgemea kuwa ni nanai anataka kusema nini na kwa manufaa ya nani.

Utaona nimekuwa na sisitiz aMjadala wa Kitaifa kwa ajili ya dhana ya UTU. Kwani ni kweli nilikuwa na jua kuwa Fisadi anaweza kuitumia atakavyo na Mzalendo pia anaweza kuitumia atakavyo!!

Na nikweli kuwa katiba ya nchi ndio iwe nguzo kuu ya kufanyia marejeo yote kwa ajili ya nchi. Pamoja na kuwa napendekeza dhana nzima ya UTU iwe ndio tofali la kuijenga katiba yetu ... ni lazima ifantike hivyo very objectively!!
 
Back
Top Bottom