TGIF: Je unaijua Misingi iliyoliunda Taifa letu?

... Je Watanzania tunasimamia vipi kupigania utu wa watu wetu? should we? au nani atatukumbusha kusimamia utu wa watu wetu wakinyanyaswa, wakidhalilishwa na kupata ubutu wa utawala wa kifisadi? Je ufisadi si adui mkubwa wa utu wa mtu? Isn't corruption the greatest enemy of the dignity of man?
It is, for sure; na ndio maana mara zote tumesema tunapambamba kujinasua kutoka katika mikono ya hawa wakoloni weusi.

Mwanakijiji nimekupata, na hapo ndipo baadae palipo zaa siasa ya kutofungamana na upande wowote, maana sisi msingi wetu umejengwa juu ya utu wa mtu na si siasa za magharibi wala mashariki!


Usawa wa Kiutu ambao pia hata wakomunisti walikiri kuwa aina ya ujamaa wa Mwalimu Nyerere ni wa kipekee haufanani na wao, yeye mwenyewe akiupambanuwa kuwa ni ujamaa wenye asili ya ubinadamu unajengwa juu ya utu na misingi ya familia moja. Nadhani familia moja leo aipo na hakuna kiongozi anaye jali shida za wananchni wake kama za familia yake. Mwalimu yeye akisema kama watanzania wanalala njaa basi na watoto wangu watalala njaa, aina ya elimu wanayosoma watanzania ndio pia watoto wangu wataisoma; leo tumeona hawa watawala wetu wakitoa elimu duni hapa ndani ya nchni na watoto wao wakisoma ng'ambo! Leo tumeona watoto wao wanapomaliza shule tu wanakuwa mamilionea na wanamiliki mitaji mikubwa wakati watoto wa wakulima na wafanyakazi wakizeeka bila hata mitaji ya kukaangia vitumbuwa.

Heshima yako Mkuu umenirudishia hisia lakini kila nikikumbuka napata hasira na kulia.
 
Oohh Mwanawasu Mwanakijiji.,nimedondosha chozi kwa tafakuri ya maono,utu., na intellectual ya kambarage. Rip the son of Africa.
 
Wasiwasi wangu ni kwamba utaishia ku-quote speeches na maandiko za mwana jumuia mwenzako (a.k.a. mtakatifu nyerere) kama mising ya taifa...too late no going back..

Taifa letu si yeye na wala yeye siyo authority ya kuunda taifa letu..

Tutaandaa mising yetu yenyewe wala si matokeo ya ccm ya nyerere a.k.a chadema

Daah., wee jamaa nunda sana .. "ccm ya nyerere aka chadema " ...if that's, basi heri ya chadema
 
Daah., wee jamaa nunda sana .. "ccm ya nyerere aka chadema " ...if that's, basi heri ya chadema

Nyerereism is dead and buried long time ago...wamebaki wapigao kelele..sana sana wataishia kumpa utakatifu period..which we don't care
 
Mzee Mwanakijiji,

Katika muktadha wa hoja yako, inaelekea misingi ya taifa unayoizungumzia ni ile inayofahamika kwa wengi katika lugha ya Kingereza kama values (au maadili). Mataifa ambayo yameendelea, yamefanya hivyo kwa kuwa yamejengwa kwenye misingi ya kudumu; misingi ambayo huwa ni injini ya ustawi wa jamii na maendeleo ya raia wa taifa hilo kwa ujumla. Ili umelithibitisha kwa kuvitaja vipengele vya misingi ya taifa la Kimarekani na Magna Carta ya Uingereza.

Mifano hii miwili, inaonyesha azma ya jamii ya kisiasa kutaka kuikumbatia demokrasia, siyo tu kama mfumo wa serikali, bali pia kama njia pekee inayomhakikishia 'mtu uhuru wa kutoa fikra na mawazo yake bila kuingiliwa; kutafuta, kupokea na kusambaza taarifa au mawazo, kupitia chombo chochote cha habari na bila ya kujali mipaka (kifungu cha 19, Tamko la Haki za Binadamu-Universal Declaration of Human Rights)'.

Ulazima wa kulijenga taifa kwa misingi ya kidemokrasia unatokana na ukweli kwamba, madhumuni ya demokrasia ni kuhami utukufu wa mwanadamu na haki zake za msingi. Hata mataifa ya Magharibi yaliyofanikiwa kuzijenga sera za demokrasia ya kiuchumi na haki sawa katika jamii, kama vile mataifa ya Ki-Nordic, yalifanya hivyo kwa kuukumbatia msingi huu.

Haki za msingi za binadamu, zinachukuliwa kuwa ni muhimu sana, kwa kila binadamu, kiasi kwamba utetezi na ulinzi wake ni jukumu la jamii nzima ya kimataifa. Hii inaeleza kwa nini kila taifa-hali hupashwa kuvizingatia vipengele vya Umoja wa Mataifa vinavyolenga kuhami haki hizi; hata pale taifa-hali linapoagiza sheria yake ya manispaa.

Hii ndiyo maana zipo mamlaka kadhaa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa zinazofuatilia na kuweka kumbukumbu za uvunjwaji wa haki hizi. Baadhi ya Mamlaka hizi ni Umoja wa Mataifa kwa Ajili ya Binadamu, Umoja wa Mataifa Juu ya Mateso Mwandishi Maalum, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai n.k.

Unauliza Tanzania ina misingi gani na kama baadhi yetu tumepata kujifunza misingi hiyo shuleni. Ni swali muhimu sana, Mzee Mwanakijiji, lakini mwishoni tunarejea kule kule: chanzo cha maadili hayo na thamani ya elimu yenyewe. Kama sikosei, la mwisho lilijadiliwa wakati wa kipindi cha Weekend World, BBC World, Jumamosi, Mei 7, 2011.

Je! Elimu inaweza kuwa na thamani bila uhuru wa kujieleza? Je! ni katika mazingira yapi elimu inaweza kuwa kikwazo badala ya kuwa chanzo cha mabadiliko katika jamii? Je! upo uwezekano kwamba elimu inaweza kutumika kuendeleza mazingira ya uonevu, ukandamizwaji na umasikini? Ni yapi madhumuni ya elimu:? Kuimba kama kasuku au kutafakari kwa kina bila ya kusubiri mwingine akwambie nini la kufanya? Ni kipi huleta mtaji wa akili katika elimu? Je! Ni misingi ipi (au mazingira yapi) yaliyoyafanya baadhi ya mataifa kuendelea na mengine kukwama katika mzunguko wa umaskini kama vile Haiti, au Colombia na Mexico ambapo vikosi vya kihalifu vina nguvu kuliko dola? Je! ni sahihi kusema kwamba mataifa ya kiafrika, kama vile Botswana na Mauritius, yamepata mafanikio waliyonayo kwa kuwa waliukumbatia msingi wa demokrasia tangu mwanzo? Je! binadamu anaweza, kwa hiyari yake mwenyewe, kuukumbatia uimla kama msingi wa kulijenga taifa lake? Je! ni busara kiongozi wa taifa kujaribu uimla, kama msingi wa taifa lake, kabla ya kuijaribu demokrasia, au, hata, kuipa nafasi ikomae? Je! ni sahihi kusema kwamba uimla, kama mfumo wa serikali, hujengwa kwa misingi ya kibabe na vitisho? Je! hao wanaotishwa baadaye huacha au huendelea kuwatisha wenzao hata maradufu?

Haya ni baadhi ya maswali machache, kati ya mengine mengi, yaliyoingia kichwani mwangu baada ya kuyasoma makala yako fupi, ingawaje kwenye pointi.



Kila taifa lina misingi yake. Misingi ambayo husimama kama maono ya aina ya taifa gani watu wanalitaka kujenga na wananchi wake hujitahidi kuifikia hiyo. Kwa mfano Wamarekani wanachukulia Tangazo la Uhuru na kauli za waasisi wao kuweza kuona misingi yao. Mambo kama Uhuru (liberty) na haki za mtu (individual rights) ni misingi ya Wamarekani.

Je Tanzania ina misingi gani? Je unaifahamu? Je unafahamu Kanuni Nne za mahusiano ya Tanzania? Je unajua ilimaanisha nini kusema wewe ni Mtanganyika au Mtanzania (baada ya Muungano)?

Je umewahi kujifunza misingi hiyo ukiwa shuleni au chuoni?
 
Wasalaam Mkuu Mwijage! Si kwa niaba ya Mzee mwanakijiji bali kwa niaba yangu binafsi naomba kujibu maswali yako kama ifuatavyo: -
  1. Je! Elimu inaweza kuwa na thamani bila uhuru wa kujieleza?
  2. Je! ni katika mazingira yapi elimu inaweza kuwa kikwazo badala ya kuwa chanzo cha mabadiliko katika jamii?
    UKOSEFU WA UHURU, YAANI LACK OF FREEDOM TO ALL, UFISADI, SERIKALI HISIYOWAJIBIKA KWA UMMA, YAANI NON RESPONSIVE TO CITIZEN
  3. Je! upo uwezekano kwamba elimu inaweza kutumika kuendeleza mazingira ya uonevu, ukandamizwaji na umasikini?
    NDIO, HASA UTU UTAKAPO HESABIWA KWA ELIMU YA MTU WAKATI ELIMU INATOLEWA PASIPO HAKI NA USIMAMIZI SAHIHI, YAANI UKOSEFU WA UHURU WA KUAMUA AINA YA ELIMU AMBAYO JAMII INAITAKA
  4. Ni yapi madhumuni ya elimu:?
    NI UKOMBOZI WA KIFIKRA
  5. Ni kipi huleta mtaji wa akili katika elimu?
    UHURU WA KWELI, HASA KATIKA MAAMUZI YA PAMOJA, YAANI 'LEADERS SHOULD BE A LEADING CENTER AT A PARTICIPATOTY LEADERSHIP WHERE ALL PEOPLE ARE EQUAL AND NOT A CENTRAL MANAGERS WHO COMMANDS AND SIPHONING EVERYTHING FOR THEMSELVES
  6. Je! Ni misingi ipi (au mazingira yapi) yaliyoyafanya baadhi ya mataifa kuendelea na mengine kukwama katika mzunguko wa umaskini kama vile Haiti, au Colombia na Mexico ambapo vikosi vya kihalifu vina nguvu kuliko dola?
    UFISADI NA UDHALIMU
  7. Je! ni sahihi kusema kwamba mataifa ya kiafrika, kama vile Botswana na Mauritius, yamepata mafanikio waliyonayo kwa kuwa waliukumbatia msingi wa demokrasia tangu mwanzo?
    NDIO NA HAPANA INATEGEMEA NINI NI DEMOKRASIA KULINGANA NA WAKATI NA UTASHI WA TAIFA HUSIKA
  8. Je! binadamu anaweza, kwa hiyari yake mwenyewe, kuukumbatia uimla kama msingi wa kulijenga taifa lake?
    NDIO, INATEGEMEA NA WAKATI, HATUA, ELIMU NA MALENGO MAHUSUSI YALIYOWEKWA KATIKA HUO UIMLA
  9. Je! ni busara kiongozi wa taifa kujaribu uimla, kama msingi wa taifa lake, kabla ya kuijaribu demokrasia, au, hata, kuipa nafasi ikomae?
    NDIO, KAMA ILIVYO FAFANULIWA KATIKA JIBU LA SWALI NAMBA NANE HAPO JUU
  10. Je! ni sahihi kusema kwamba uimla, kama mfumo wa serikali, hujengwa kwa misingi ya kibabe na vitisho?
    SILAZIMA, KAMA NI MSINGI AMBAO TAIFA LENYEWE LIMEJIAMULIA KULINGANA NA WAKATI HUSIKA NA KIWANGO CHA UIMLA YAANI 'DEGREE OF IT'S CONCENTRATION'
  11. Je! hao wanaotishwa baadaye huacha au huendelea kuwatisha wenzao hata maradufu?
    WANAWEZA KUACHA KAMA NI WATU WALIOELIMIKA NA WALIOPATA UONGOZI KWA MALENGO YA KUJENGA NCHNI YAO NA TAIFA NA WANAELEWA WAPI PA KUANZIA NA NINI CHA KUFANYA, HASA KAMA WALIKUWA SEHEMU YA MPANGO ULIOFAFANULIWA KATIKA JIBU LA SWALI LA NANE NA KUMI NA HIVYO KULETA ADVANTAGE, LAKINI PIA WANAWEZA WASIACHE KAMA NI WAPUUZI WACHACHE AMBAO HAWAJAELIMIKA, HAWANA SERA WALA MALENGO MAHUSUSI YA KUJENGA TAIFA LAO BALI NI MAFISADI NA MADHALIMU TU, MFANO NI FROM THE COLLEGE OF AFRICAN LEADERSHIP EVIDENCES.


Mwisho!
 
Nitarudi kujibu baadhi ya maswali ya Mwijage hapo juu.

Kuhusu swali la msingi kwa ufupi jibu ni kuwa Tanzania imejengwa katika msingi wa UTU wa MWANADAMU (THE DIGNIqTY OF MAN). Hii ni falsafa ya juu kidogo kuliko wale waliopigania tu "USAWA NA HAKI ZA WATU". Fikiria kidogo; mtu anaweza kukubali kuwa uko sawa naye mbele ya haki (equality in justice) lakini asikuthamini kama mtu mwenzie. Kwa mfano, mtu anaweza akasema "binadamu wote ni sawa" lakini inapokuja swali la kukuozesha binti yake au binti yako kuolewa kwao anakuona hauko sawa kwa sababu ya rangi, dini, hadhi, cheo n.k Kimsingi anakubali mko sawa kisheria lakini hamna utu sawa!

Mtu anaweza akasema "sisi sote ni sawa" kwa maana ya kuwa sheria inatulinda sote sawawsawa lakini yeye katika nafasi yake akaona anastahili zaidi; hivyo atajihakikishia umeme, maji, afya bora, usafiri salama n.k lakini hatopigania kuona watu wengine wasio na nafasi kama ya kwake wanapata vitu anavyopata yeye na hivyo kulingana naye kwa namna fulani.

Hapa ndio utaona tofauti ya watu kama Nyerere, Gandhi, Mother Theresa, MLK Jr, Mandela, Tutu n.k Hawa hawakuongozwa na kutaka kutambuliwa kwa usawa wa wanadamu kwa misingi ya kisheria - kitu ambacho kimefikiwa katika nchi nyingi sana - bali usawa unaotokana na utu.

Nitoe mfano mwingine wa karibu sana. Mkristu anaposimama na kutetea haki za wakristu tu kwa maana ni wakristu wenzake na hivyo anaona ni wajibu wake yawezekana kabisa akawa anatenda haki kwa nafsi yake na imani yake. Yeye akiona Waislamu wanahoji kuhusu utendaji wa mtendaji Mkristu atakuja juu na kuona kuwa Mkristu "mwenzake" anashambuliwa. Kwa huyu usawa ni usawa kwa "wakristu" tu lakini watu wengine wote wenye dini nyingine hawako sawa naye. Hivyo huyu atatoa ajira kwa misingi ya dini, atapigana vita dhidi ya ufisadi kwa misingi ya dini, na atajaribu kutafuta namna ya kumezea mate ubovu kwa misingi ya dini. Haongozwi na misingi ya utu.

Lakini akija kupata mwanga ataona kuwa Waislamu na Wapagani na wale wasio na imani kabisa wote ni binadamu wenye utu sawa na yeye! hili ni wazo tofauti.

Sasa taifa letu lilijengwa katika msingi huo angalau kama 'FOUNDING PRINCIPLE'. Jana nimebahatika kuangalia picha mbalimbali za Igunga (ambazo wengi nadhani hamtapata nafasi ya kuziona - msiniuilze kwanini) nikajikuta nashangaa utofauti uliopo kati ya Binadamu wa Dar-es-Salaam na binadamu wa 'sehemu nyingine'. Nimeona nyumba, mavazi, maisha ya wananchi wetu huko na kuyaona kwa asilimia 100 hayajabadilika sehemu nyingine kuliko ilivyokuwa kabla ya uhuru. Kwa watu hawa neno "uhuru" halina maana yoyote.

Siasa zetu na sera zetu za uchumi na mikakati mbalimbali imelenga kuleta "maendeleo" ya vitu. Hivyo Mkapa anaenda Igundu na kuwaonesha wananchi "barabara" na "hospitali" kama "maendeleo". Leo hii watu wanalazimishwa kuona "mengi" ambayo "serikali imefanya". Ukiangalia utaona yote ambayo yanaoneshwa yanahusiana moja kwa moja 'kuongezeka vitu". Lakini vipi kuhusu utu? Iweje leo wapo watu Igunda wanapewa msaada wa chakula, watu wanakufa Zanzibar kwa meli pasipo ulazima wowote au ajali za mabasi ambazo kiakili tu unaweza kujua zisingepaswa kutokea? Iweje kwa mfano watu wanalalamikia mashindano ya Vodacom kuendelea badala ya kulalamikia ajali kuendelea?

Kuungua kwa soko la Mwanjelwa kwa mara nyingine kwanini hakuwaudhi watu zaidi? Hivi kweli watu wanafikiri kuna tofauti kubwa kati ya ajali ya meli, basi na kuungua kwa soko la Mwanjelwa? Well.. utaona tofauti tu kama utaangalia ni "nani amedhurika"! Kwa sisi wengine hivi vyote vinahusiana na utu. Sijasikia wanasiasa wakilalamikia tukio hilo na kuonesha hasira! Ajali nyingine ya basi imetokea juzi tu hapa lakini hatujasikia watu wakiona kama ni tukio baya!.

Athari kubwa kabisa ya ukoloni na utumwa katika fikra zetu ni kupoteza utu wetu. Leo utu unahusishwa na vitu, wenye vitu zaidi ndio watu zaidi.

Sasa.. ile dola 100 yetu. Ni nani hapa amegusia karibu zaidi swala hili la "utu" kama founding principle ya Tanzania? tukubaliane japo tufikiria kapata kama asilimia 80-90!!!
 
Mwanakijij, mada yako inatugusa watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa. Taifa letu lilijengwa na misingi imara hakuna anayeweza kubisha kwa hilo, Arafat na Mwijage wamejaribu kulifafanua na nadhani wanastahili ahadi yako ya tuzo la $100. Swali la msingi tunalopaswa kujiuliza watanzania Je Taifa letu bado limesimama kwenye misingi yake? Inasikitisha sana kuona Tanzania tumepata utitiri wa viongozi wasio na maadili na hili ndilo linalotishia utaifa wetu. Tukianzia na Raisi wa CCM mpaka viongozi wa upinzani ni vurugu tupu! Yapo mambo mengi sana ambayo yanahatarisha misingi ya Taifa hili. Kitendo cha Raisi kuwakumbatia wala rushwa na wezi wa rasilimali za Taifa na kitendo cha kiongozi wa upinzani kujipangia mshahara wa mil.7 kwa mwezi ni moja tu ya kero zinazotishia misingi ya Taifa hili. Mwalimu Nyerere (RIP) aliweza kusimamia misingi ya Taifa letu kwasababu alikubali kuishi kama mtanzania wa kawaida. Inasikitisha sana kuona Taifa lilokuwa imara kama Tanzania linasheherekea miaka 50 ya uhuru likiwa kwenye mapasuko (Fallen state). Labda kwa kumalizia ungejaribu kuwauliza watawala wetu kama wanaijua misingi ya Taifa hili.

Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Mzee Mwanakijiji,
Hakika mada hii inatugusa wengi na pengine ni muhimu pia tuwe waangalifu ktk kashfa na yale tunayoyaombea kwa sababu hata iwe vipi Tanzania ni nchi inayokua kiumri tu na sii kimaendeleo. Kama nilivyowahi kusema mtoto anapozaliwa huvaa nepi na kila anavyokuwa ndivyo mavazi yake hubadilika kulingana naye. Haya tunayoyaita leo manendeleo ni makuzi ya miji yetu kiasi kwamba Dar population imefikia millioni 5 toka millioni 1.5 na ukubwa waardhi au sehemu haujaongezeka hivyo kinachofuatia ni kujenga maghorofa sawa na mtoto anayeacha nepi na kuvaa kaptula.. Kiafya tanzania bado ni masikini kama ile ya mwaka 1960 na pengine maskini zaidi kwa sababu ukitazama index ya nchi zote duniani, Tanzania imeshuka daraja. Makuzi ya mwili haina maana tuna Afya bora zaidi.

Turudi ktk UTU, mkuu nakukubali...kwanza kabisa ni lazima tufahamu ya kwamba waasisi wa Uhuru wetu walipigania Uhuru wetu siii kwa sababu ya kumweka mtu mweusi Ikulu ATUTAWALE isipokuwa ilitokana na kuona watu wachache wana dectate Uhuru wetu na wanamiliki uchumi wetu hali wananchi walio wengi hawana Uhuru huo na wanaendelea kudhoofika kiuchumi. UTU wetu uliondolewa na tukawa watumwa nguvu kazi watawaliwa ndani ya nchi yetu wenyewe kwa maslahi ya kundi la watu waliojiita Elites (Malkia, Kings na Sultan).

Kwa hiyo UTU ndio uliwasha cheche na harakati za Uhuru na ili UTU huu upate kusimama fikra pevu dhidi ya kutawaliwa na utumwa zilijengeka through a Golden rule isemayo - Usimtendee mtu vile hutapenda wewe utendewe! (Don't treat others the way you don't want to be treated!). Hivyo equality in Justice was meaned to discepline us lakini maajabu ya Mungu dunia nzima bado tumeendelea na KUTAWALIWA. Na pengine yawezekana hii ni failed phylosophical ethic tradition kama tunavyouzungumzia Ujamaa (socialism) kwa sababu UTU umezungumzwa toka Taurat - Wapende jirani zako kama nafsi yako (Love your neighbors as yourself: I am the LORD.) yet maneno haya yamekuwa mtihani mkubwa kwa binadamu pamoja na kujaliwa akili ya kutopenda kutendewa mabaya, hatuna mapenzi ya kweli na bado tunawatendea wengine mabaya - we can't flip a coin tujitazame sisi kama tutapenda tutendewe hivyo.

Hivi leo baada ya miaka 50 ya Uhuru, we still watumwa kifikra, kuna watu wanataka sana tuamini kwamba wakati wa mkoloni babu zetu waliteseka sana, walinyanyaswa na kadhalika lakini ukweli ni kwamba tumebadilisha vichwa vya watawala. Leo hii hatuna viongozi kama tulivyodhamiria na ndio maana bado tunatumia neno WATAWALA WETU. Twende mbele turudi nyuma utaona ya kwamba hao babu na baba zetu ingawa hawakuwa na elimu ya kushika madaraka ya juu wote waliweza kujenga nyumba zao na kufikia Uhuru aghalab kuikuta familia haina hata nyumba. Hadi tunapata Uhuru ilikuwa vigumu sana kuona homeless na binafsi ktk maisha ya ujana wangu sikumbuki kuona homeless, sikumbuki lakini leo hii mkuu Mwanakijiji kama ulivyosema hapo juu ukienda Igunga na vijijini utashindwa kuamini kama hizi ni sehemu za nchi yetu huru. Tushukuru Mungu Mitumba imeficha aibu kubwa sana!

Na inasikitisha zaidi kuona kwamba tunaendelea kuuza UTU wetu kwa fedha. Demokrasia has done nothing other than intergrate marketing the two! Tunarudisha Ukoloni bila kupoteza fikra za kuthamini UTU. At the back of our head tunaamini kabisa Ukoloni mamboleo kama njia pekee ya kuboresha Uchumi wetu ili hali uchumi huo hauna manufaa kwa wananchi hata kidogo. na maadam tumeshindwa kuelewa mahusiano baina ya UTU na UCHUMI itakuwa sii rahisi kusimamisha justice hata kidogo..Why in the hell wazee wetu walipigania Uhuru (sio kwa vita bali through dialogue) ikiwa leo Mtanzania hana amani wala tumaini na maisha bora zaidi?. Still mzee wangu naomba darasa zaidi ili nipate kumsoma vizuri Mwalimu maanake huwa sichoki kusikia vision yake kwa Tanzania huru - Mwenyezi Mungu amweke mahala pema peponi!
 
This is interest discussion na cha kuongeza tu. There are failures every corners of our country na ccm siku zote wanataka wananchi wasijue malengo ya kuchagua viongozi, demokrasia ni nini, what's role of the gov and who's gov?

Hizi discussions na cdm nchini vimesaidia kufungua macho wananchi juu ya haki zao na jinsi ya kuzipigania. We are getting somewhere!
 
A) Kwa hakika utu wa binadamu ndio msingi uliowekwa na watangulizi wa taifa hili kuanzia watemi na machifu kabla ya uhuru. Wakoloni walipofika Lushoto walimkuta mtemi kimweri akiwa mahakamani kwake akitoa haki ili kuhakikisha utu wa mwanadamu unatimizwa kwa thamani na haki.
Baada ya kuondoka watangulizi waliokuwa wanajenga msingi huo sasa tuna taifa lenye ukosefu wa misingi (values).

B)Labda nigusie majibu kidogo kutokana na maswali ya Mwijage.

1. Je elimu inaweza kuwa na thamani bila uhuru wa kujieleza?
Jibu langu ni ndiyo. Elimu peke yake inaweza kujieleza hata bila ya uhuru wa kujieleza endapo itatumika kielimu.
Elimu ni kichochoe kizuri cha kujieleza, nitoe mfano, miaka 50 hayajatufikisha pale tulipotarajia. Kutokana na ukosefu wa elimu miongoni mwa wengi wetu, viongozi wanawaimbia mafanikio machache ambayo ni haki ya wananchi.
Kama elimu ingetumika vema wananchi wangewajibu kwa vitendo. Fikiria tungesusia sherehe za miaka 50 bila maneno hiyo tu ingekuwa sehemu ya kujieleza kwa elimu hata kama uhuru wa kujieleza haupo.

2. Je, Mazingira gani elimu inaweza kuwa kikwazo badala ya kuwa chanzo cha maendeleo ya jamii?
Elimu ni msumeno unaokata mbele na nyuma. Inategemea mtumiaji na matumizi yake.Kwa maendeleo ya kijamii elimu imetumika vizuri na vibaya kama tunavyoshuhudia.
China wameitumia vema sasa wanakaribia kuongoza dunia. Sisi tunaitumia vibaya kuliangamiza taifa, mikataba feki, posho, ufahari na ufujaji n.k

3.Je, elimu inaweza kutumika kuendeleza uonevu na ukandamizaji?
Ndiyo, pale unapomuondoa mwananchi kwenye ardhi yake na kumkabidhi mwekezaji kwa kisingizio cha uwekezaji ni ukandamizaji. Wananchi wanapoondolewa maeneo ya kwa 'study fake' au visingizio vya environment impact au kutowarudishia mapato yatokanayo na sacrifice yao ni ukandamizaji wa kutumia elimu.

Pale unapokusanya kodi na kupanga matumizi ya kikundi cha watu wachache wanaoishi Dar kununua VX na si Asprin ni uonevu, na ukandamizaji ni pale matumizi ya FFU yanapokuja baada ya mlipa kodi kusema kodi yangu iko wapi. Ni elimu inayotumika kutafuta vifungu vya sheria asiyoijua mwananchi ili kumnyanyasa kwa lugha za amani na utulivu n.k.

4. Je nini madhumuni ya elimu?
Madhumuni ya elimu ni kumwandaa mwanadamu kukabiliana na mazingira yake.

5. Kwanini mataifa flani yaendelee na mengine yakwame kimaendeleo?
Ni kutokana na kuthamini au kutothamini msingi ya jamii inayoiweka jamii pamoja kwa lengo moja. (Values and social fabrics).
Walioendelea wana values zao kama kuthamini haki ya mtu, uhuru wake na haki za binadamu wa taifa hilo.
Mataifa hayo yana kitu ' moral authority' iliyowekwa na wananchi wanaothamini values za society, ethics na principle zake, zote zikihanikizwa akilini mwao na elimu bora.

Mtaifa masikini si masikini, bali yana upungufu wa viongozi wenye elimu wanaoitumia elimu hiyo vibaya'libertine' kwasababu ya egoism, selfishness na kutojali utu wa mtu.

6. Je mataifa kama Botswana na Mauritius yamepata maendeleo kwa kukumbatia demokrasi mapema?
Kuna ndiyo na hapana
Hapana kwa sababu demokrasia ni kama soksi usiyoweza kuivaa peke yake bila viatu.
Ndiyo kwasababu walijenga misingi ya uadilifu na uzalendo kwa nchi zao kwanza kabla hawajakumbatia demokrasia.

Angalia mataifa yote mashariki hadi magharibu yaliyopiga hatua utagundua kuwa hakuna kitu zaidi ya misingi ya uadilifu wa viongozi wao.
Katika miaka 6 Japan imekuwa na mawaziri wakuu 5 bila taifa kupoteza mwelekeo kwasababu taifa limeandikwa katika misingi inayothaminiwa na wote na isiyo na shaka katika uadilifu.

Malaysia tulikuwa sawa katika miaka ya 50, sasa wametuzidi si kwasababu nyingine bali misingi imara ya taifa lao inayolinda masilahi ya umma kuliko mtu mmoja au kikundi cha watu.

Taifa kama letu limeoza kimaadili, uadilifu, ubunifu na hamasa. Kiongozi hawazi anataka kulipeleka wapi taifa siku inayofuata, wote akili zao ni dili gani itakayo mnufaisha yeye na kizazi chake. Ni wapi anaweza kununua VX ya serikali kwa milioni 2 bila kujali mita chache kuna hospitali haina ambulance.Ubinafsi na uozo wa maadili ndio umetufkisha hapa.

Ubinafsi wa kulipana posho na kukosa utu wa kununua kitanda cha mzazi. Utovu wa maadili wa kusikiliza marafiki na si wananchi, yote hayo yakifanywa vema kwa kutumia vibaya elimu kama ilivyotumika kutengeneza atomic bomb.

Tatizo letu sio demokrasi, utawala wa kiimla au wa sheria! ni ukosefu wa uzalendo kwa wananchi, ubinafsi na uchoyo kwa viongozi, kupoteza thamani inayolijenga taifa, kutofuata misingi tuliyojiwekea na kutoheshimu utu wa mtu.

Kwa hali ilivyo sasa tofauti ya ukoloni na kujitawala inaelezeka kwa page 1000. Kama mkoloni hakuwa na utu,je uliopo sasa ni upi?
 
Kila taifa lina misingi yake. Misingi ambayo husimama kama maono ya aina ya taifa gani watu wanalitaka kujenga na wananchi wake hujitahidi kuifikia hiyo. Kwa mfano Wamarekani wanachukulia Tangazo la Uhuru na kauli za waasisi wao kuweza kuona misingi yao. Mambo kama Uhuru (liberty) na haki za mtu (individual rights) ni misingi ya Wamarekani.

Je Tanzania ina misingi gani? Je unaifahamu? Je unafahamu Kanuni Nne za mahusiano ya Tanzania? Je unajua ilimaanisha nini kusema wewe ni Mtanganyika au Mtanzania (baada ya Muungano)?

Je umewahi kujifunza misingi hiyo ukiwa shuleni au chuoni?

PICHA ZA IGUNGA

View attachment 37470View attachment 37471View attachment 37472View attachment 37473

Mwanakijiji, unatakiwa kukumbuka kuwa wakati tunapigania uhuru tulikuwa tuna malengo. La kwanza ilikuwa nikuondoa dhuluma- Tuliyokuwa tunafanyiwa na wakoloni.Kulikuwa na dhuluma kwa upande wa haki,hali na mali (kipindi kile tulikuwa tunasema kunyanayswa, kupuuzwa, kudharauliwa etc). Kwa sasa ni kama vyote vimerudi, japo si kwa kiwango sawa na cha wakoloni.

Tulipowaondoa wakoloni tulianza kujenga taifa letu kwa misingi ya kurudisha heshima ya mtanganyika, na tukaendelea hadi kufikia kulinda heshi ya mtanzania.

Misingi rasmi iliwekwa kwenye azimio la arusha, na kanuni za chama za wakati ule.

heshima kwa binadamu, Umoja, undugu, vita dhidi ya rushwa etc etc lakini kwa sasa ukiangalia yote yako kinyume.

Misingi yetu haifanani na ile ya Marekani, hata matofali yanayojenga msingi wetu hayafanani na yale ya Marekani.
 
Mojawapo ya maneno mazito kabisa katika historia ya Tanzania ni yale yaliyotolewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye makala ambayo kwa kiasi kikubwa inaaminiwa ilichangia sana kubadilisha mtazamo wa Wazungu kuhusu Afrika ya Kusini chini ya ubaguzi wa rangi. Makala hiyo ilitoka kwenye gazeti la The Observer la London Machi 7, 1961. Ilikuwa ni wakati wa mkutano wa nchi za jumuiya ya madola na ni wakati huo swali la "JE AFRIKA YA KUSINI IENDELEE KUWA MWANACHAMA WA MADOLA BAADA YA KUWA JAMHURI?".

Makal hii ilianza kwa kusema hivi (msisitizo wowote wangu):
The people of Tanganyika are working to build a non racial democratic society. We fought successfully against our classification as multi racial state because what we want is a society where the individual matters, and not the color of his skin, or the shape of his nose. Racial group privileges or discrimination are incompatible with this.

Mwalimu akaenda mbele zaidi baada ya kusifia kidogo mafanikio yetu ya kwanza ambayo yaliwashangaza wageni wengi wa wakati huo ambao wakilinganisha Tanganyika ya wakati ule na nchi jirani suala la rangi lilikuwa si issue ya kuwagawa wananchi - wanaokumbuka uchaguzi wa 1965 baadhi ya wasio weusi walichaguliwa na wananchi! Wakati Nyerere anayesema haya ya kutokuangalia rangi ya mtu Martin Luther alikuwa hajasema ile hotuba yake maarufu ya "I have a dream".

Nyerere akasema hivi:
We have of decided on this policy because we expect to gain economically if we do so. On the contrary, if it becomes necessary, we shall accept economic loss.

And in fact we did! Kuchukua uamuzi mzito kama ule dhidi ya taifa lenye nguvu na washirika wa karibu kama Afrika ya Kusini ilikuwa ni kitendo cha ujasiri. Tulijali jinsi wanavyotendewa watu weusi kiasi kwamba hatukuwa tayari kujifanya hatuoni. Leo hii watawala wetu wamekuwa na urafiki wa karibu na watu wenye kuvunja hii "dignity of man" principle bila kujua THAT IS IN CONTRADICTION TO BEING TANZANIAN.

Ni katika hili Nyerere akasema kitu ambacho wengi walikiona matokeo yake lakini bila ya shaka hawakujua the founding principle:
The Tanganyika Government cannot afford to have any relations with the South African Government, and it must, within the bounds of international law, lend support to those who struggle against the system of apartheid.

Akasema tena,

we do not see how any country like ourselves , committed to policies based on the dignity of man, can be a member at teh same time as South Africa is one.

na akatangaza kitu kinachoweza kumfanya mtu yeyote vinyweleo visimame!

We believe that the dignity of man is the idea which can defeat racialism!

Na hapa akaelezea kwanini Tanganyika isingeweza kuwa mwanachama wa Madola kama Afrika ya Kusini nayo ingekuwa mwanachama.

By refusing, we would be making clear to all enemies of freedom and dignity of man that we are prepared to do anything which is necessary to protect our society from spiritual as well as material evil.


Ilikuwa ni katika makala hii ndio ile kauli maarufu ambayo ilitolewa na kunukuliwa na vyombo vya habari duniani:

Inevitably, therefore, we are forced to say that to vote South Africa in, is to vote us out

Utaona basi harakati zetu za ukombozi zilihusiana zaidi na utu wa binadamu kuliko kitu kingine chochote. Na ukiangalia hapo unaweza kuyaona maamuzi mbalimbali ya wakati ule yakiwa yanahusiana moja kwa moja na kanuni hii ya "utu wa mwanadamu".
 
Mwanakijiji, unatakiwa kukumbuka kuwa wakati tunapigania uhuru tulikuwa tuna malengo. La kwanza ilikuwa nikuondoa dhuluma- Tuliyokuwa tunafanyiwa na wakoloni.Kulikuwa na dhuluma kwa upande wa haki,hali na mali (kipindi kile tulikuwa tunasema kunyanayswa, kupuuzwa, kudharauliwa etc). Kwa sasa ni kama vyote vimerudi, japo si kwa kiwango sawa na cha wakoloni.

Tulipowaondoa wakoloni tulianza kujenga taifa letu kwa misingi ya kurudisha heshima ya mtanganyika, na tukaendelea hadi kufikia kulinda heshi ya mtanzania.

Misingi rasmi iliwekwa kwenye azimio la arusha, na kanuni za chama za wakati ule.

heshima kwa binadamu, Umoja, undugu, vita dhidi ya rushwa etc etc lakini kwa sasa ukiangalia yote yako kinyume.

Misingi yetu haifanani na ile ya Marekani, hata matofali yanayojenga msingi wetu hayafanani na yale ya Marekani.


Bongolander soma sehemu nyingine katikati kidogo hapa.
 
Msingi wa kutunga Katiba yetu umetokana na Misingi iliyojenga Taifa letu ambayo kwenye Utangulizi wa Katiba yetu imetamkwa kama...... UHURU, HAKI, UDUGU na AMANI. Sasa kama kila mtu atachukua kile anachokipenda na kukifanya ndio Misingi ya Utaifa wetu tutakuwa tunazidi kuwachanganya zaidi Watanzania. Nakuu Utangulizi unasema hivi..

UTANGULIZI
MISINGI YA KATIBA

KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi
yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na
amani:

 
Msingi wa kutunga Katiba yetu umetokana na Misingi iliyojenga Taifa letu ambayo kwenye Utangulizi wa Katiba yetu imetamkwa kama...... UHURU, HAKI, UDUGU na AMANI. Sasa kama kila mtu atachukua kile anachokipenda na kukifanya ndio Misingi ya Utaifa wetu tutakuwa tunazidi kuwachanganya zaidi Watanzania. Nakuu Utangulizi unasema hivi..

UTANGULIZI
MISINGI YA KATIBA

KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi
yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na
amani:


Katiba ya mwaka gani!? kati ya hiyo katiba unayoisema na Taifa la Tanganyika na Tanzania ili ilianza kuwepo kabla ya nyingine?
 
Kila taifa lina misingi yake. Misingi ambayo husimama kama maono ya aina ya taifa gani watu wanalitaka kujenga na wananchi wake hujitahidi kuifikia hiyo. Kwa mfano Wamarekani wanachukulia Tangazo la Uhuru na kauli za waasisi wao kuweza kuona misingi yao. Mambo kama Uhuru (liberty) na haki za mtu (individual rights) ni misingi ya Wamarekani.

Je Tanzania ina misingi gani? Je unaifahamu? Je unafahamu Kanuni Nne za mahusiano ya Tanzania? Je unajua ilimaanisha nini kusema wewe ni Mtanganyika au Mtanzania (baada ya Muungano)?

Je umewahi kujifunza misingi hiyo ukiwa shuleni au chuoni?

PICHA ZA IGUNGA

View attachment 37470View attachment 37471View attachment 37472View attachment 37473

Ni UTU ... Ndio MSINGI wa Uasisi wa Taifa Hili!!!

Ni UTU kutafsiriwa kwenye Kauli, Fikra na Vitendo kwa kila Mwanachi anayeJitaa Mtanzania.

Utanzania sio kuzaliwa tu Tanzania ..Ni uwezo wa Kuutafsri Utu kwa Matendo, Fikra na kauli na hilo linapofanikiwa tunampata MZALENDO.

NI UTU kutafsiriwa kwenye nyanja zote za jamii ..Utu kwenye Elimu, Utu Kwenye Kilimo, UTU kwenye Ulinzi, UTU katika kugawana Rasilimali za TAIFA, UTU kwenye UONGOZI, UTU kwenye KATIBA, UTU kwenye Muungano, UTU kwenye SIASA za ndani na nje, UTU kwenye AFYA(mtu ni afya), UTU kweneye maendeleo na ujenzi wa UCHUMI, UTU kutafsitriwa kwa kila mwanachi, familia, jamii na hatimaye kuupata UTU WA TAIFA.

Maendeleo yoyote hata yawe na mafanikio kiasi gani machoni mwa binadamu nu Bure ..Kama hayakuzingatia UTU kama msingi na muhimili wake. UTU utawale Uchumi UTU utawale Bishara, Kwahiyo tuwe maendelao yanaoendana na kuendelea kwa UTU na Dhana nzima ya UTU.

Kwa kifupi binadamu na utu wake waendelee na maendeleo ya Mazingira yale ... Yaani Binadamu na Maendeleo!

Maendeleo ya Tafa hili yatenganishwe na yawe dhahiri kwa kuona na kwa kupima KUWA:

1. UTU: wa WATANZANIA unakuwa unalindwa na KUENDELEA
2. VITU: Kuendelea kwa vitu kwa maana ya uchumi na mazingira yote yanayomzunguka Mtanzania.

IKIWA NA MAANA KUWA

MAENDELEO YA MTANZANIA = MAENDELEO YA UTU + MAENDELEO YA VITU(mazingira yake)

Kile kilichopandishwa mlimani kilimanjaro siku ile ya uhuru kilamaanisha UHURU WA UTU WA MWANADAMU. Uhuru wa UTU wa mtanzania na mazingira yake.

Kiite mwenge wa uhuru ..ile ilikuwa ni alama kusimamia na kuonyesha alama ya UTU WA TAIFA na hadi kwenye nembo ya nchi kipo. Ni alama ya UTU wa TAIFA...Ingawaje sikuhizi kinafanyiwa mzaha mtupu... Na WAPINGA UTU WA TAIFA ...Watetea UNYAMA NA UFISADI WA TAIFA!!!

Tafiti zinaonyesha kuwa: Alama ya UTU wa TAIFA ... imetapakaaa nchi nzima kwa kila namna. Mtu akiuliza kwanini hiyo alama niliyoiita alama ya UTU WA TAIFA ..iko kila mahali ..Kila kofia ya Mwanajeshi wetu hadi leo iko, nembo ya taifa, alama ya mashirika mengi , alama na ishara karibu kila mko ipo alama ya UTU WA TAIFA ..siwezi kumaliza ....Ukweli anahitimisha kuwa MSINGI WA YA KUUNDA TAIFA HILI NI UTU KUTAFSIRIWA KWENYE KILA NYANJA YA KIJAMII.

TUNACHIHITAJIKA KUFANYA:

Kuanzishwa kwa harakati za dhati za kuufufua UTU wa Mtanzania. Kwa sababu ni swala la kifikra na kisaikolojia ..inaaaminika kuwa MSUKUMO WA UTU WA TAIFA haujapotea (Iko kwenye subconscious ya Jamii) Nasema MSUKUMO UPO UMELALA !! KWA HARAKATI SAHIHI TU ... NI WA KUAMSHWA NA KUFUFULIWA NA MOTO UTAKAO WAKA HAPO ..HAUZUILIKI KWA NAMNA YEYOTE ILE.

NDIO!!

NGUVU YA UTU WA MTU INAWEZA KUZUIA MABOMU YOTE NUKLIA DUNIANI YASILIPUKE !!

HAKUNA HAJA YA KUTILIA SHAKA ..POTENTIAL ENERGY INVOLVED ... HASIMAMISHI MTU UTU WA MTU KUITWAA NCHI HII AMBAYO UTU NDIO CHIMBUKO LAKE!!!

HIVYO UTU SIO JAMBO LA KUFANYIA MZAHA ... ITS AN AUTHORITY!! ...... Anayetaka amatafute JK NYERERE(RIP) atamsimulia!!

NAMNA YA KUUMALIZA USHENZI UNAOENDELA HAPA NCHINI SASA HIVI ..SI NGUVU NYINGINE..

ILA NI NGUVU YA UTU.... na si yakuagiza ulaya au marekani, au kumpigia mwekekezaji magoti ...IPO!!

WANATAKA KUUPANDISHA ULE MWENGE WA UHURU KUSHEHERAKEA MIKA 50 YA UHURU

HUO NI USHENZI... WANAPATA WAPI MAMLAKA YA KUFANYA VILE...

HAPA KUNA JAMBO LA KUFANYA ...TUTAONA.....!!!!!
 
Mzee Mwanakijiji,
Pamoja na yote hayo kwa nini lakini tuli copy na Ku Paste kuundwa kwa katiba yetu toka ile ya mwingereza mtawala wetu!..Hivi naweza kuipata original copy ya katiba ya mwaka 1961kwani tumefanya changes mara 5 zote ktk UTAWALA lakini maajabu ni kwamba sioni sehemu zinazohusu dira yetu kama Taifa huru.
Kuna kipande hiki cha sheria zetu very interesting nawaomba mkitazame kwa makini.

Sources of Law
Tanzania's legal system is based on the English Common Law system. It derived this system from its British colonial legacy, as it does the system of government, which is based to a large degree on the Westminster parliamentary model.

The Constitution
Unlike the unwritten British constitutional system, the first source of law for the United Republic of Tanzania is the 1977 Constitution. The constitutional history of Tanganyika traces its background from the 1961 Independence Constitution, which was adopted at the time of independence. In 1962 Tanganyika adopted the Republican Constitution, which operated from 1962 up to 1965. These two were based on the traditional Lancaster style constitutions negotiated at independence by the British upon handover of state power to newly independent states. In 1965 Tanganyika adopted an Interim Constitution while the country awaited a new constitution to be drafted, after it abolished the multi party political system and adopted a one party state system. The process lingered longer than it was meant to and thus the constitution lasted from 1965 up to 1977 when a new constitution was adopted and it has remained applicable to date, with fourteen subsequent amendments. The Constitution provides for a bill of rights, notwithstanding the fact that it also makes provision for a number of claw-back clauses. In other words the enjoyment of certain rights and freedoms under the constitution is not absolute, but it is subject to legal regulation.The Bill of Rights is found in part three of the first Chapter of the Constitution and the fundamental rights and freedom are stipulated in article 12 to 24, article 25 to 28 imposes duties on every individual to duties and obligations to respect the rights of others and society. Article 29 establishes the obligation of society to every individual.Article 30 of the Constitution limits the application of these rights subject to law and the under the due process of law, as the case may be.The Constitution allows any person to challenge any law or act/omission, which contravenes his or her right, or the Constitution.

Statutes
The second source of law is the Statutes or Acts of Parliament. The Laws Revisions Act of 1994 Chapter Four of the laws of Tanzania [R.E. 2002,] established that all legislations previously known as Ordinances, i.e. those which were enacted by the pre independence colonial administration, as Orders in Council, can now be legally recognized as Acts. These principal legislations, and subsidiary legislations thereto, are published in the Government Gazette and printed by the Tanzania Government Printers.

Case Law
The third source is case law. These are cases from the High Court and Court of Appeal which are either reported or unreported and are be used as precedents, and bind lower courts thereto.Reported Tanzanian cases are found in the Tanzania Law Reports, High Court Digests and East Africa Law Reports.

Received Laws
The fourth source is Received Laws established under Section 2.3 of The Judicature and Application Laws Act, Chapter 358 of the Laws of Tanzania [R.E. 2002] (JALA) these include: Common Law, and Doctrine of Equity, Statutes of General Application of England, applicable before the 22 of July 1920, which is deemed to be the Reception date for English Law in Tanzania.

Customary and Islamic Law
The fifth source is the Customary and Islamic law, which are established under section 9 of JALA. Whereby customary law is in effect only when it does not conflict with statutory law whilst Islamic law is applicable to Muslims under the Judicature and Applications of Laws Act, empowering courts to apply Islamic law to matters of succession in communities that generally follow Islamic law in matters of personal status and inheritance.

International Law (Treaties and Conventions)
International Laws, that is, Treaties and Conventions, are not self-executing. The Act of Parliament can apply treaties and conventions to which Tanzania is a party in the Courts in Tanzania only after ratification
 
Back
Top Bottom