TGIF - Je ni neno au msemo gani unaukumbuka?

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
127
Nilipokuwa mdogo kuna maneno au misemo ya “Kiswahili” nilikuwa naisikia na kuitumia sana bila ya kujua kuwa ni ya kingereza

Kwa sababu inglishi haikuwa richabo, sikuweza kung’amua kuwa yale maneno yalikuwa ni ya king'eng'e ambayo yamegeuzwa kuwa ya Kiswahili.

Mfano….

....Bibi yangu alikuwa anapenda kutumia neno "Bilalifulu” akiwa amekasirika. Ilinichukua miaka kadhaa kuja kugundua kuwa kumbe neno lenyewe ni tusi la kiinglishi – “Bloody Fool”

...Neno “kuteta” ………. Kwenye sentensi “njoo TUTETE kidogo.” Je mnajua kuwa hili neno linatokana na neno la kiinglishi – “Tete a tete”....meaning “one to one conversation”

Je ni neno au msemo gani unaukumbuka ambao ulikuja kugundua baadaye kuwa ni wa kiinglishi?
 
:)


  • Enkachif - Handker-chief
  • Ki-sosa - Saucer
  • Keki - Cake
  • Kiplefti - keep-left



Kuna neno/msemo nilisikitika kutopata Kiingereza chake nikiishi ng'ambo.
"Pole" - Mfano Pole na kazi!
Kiswahili is a rich language bwana! (Not very rich)




.
 
:)[*]Ki-sosa - Saucer

Ebwanaee yaani mpaka leo hii nilikuwa sijui kuwa "kisosa" inatokana na "saucer"


Kuna neno/msemo nilisikitika kutopata Kiingereza chake nikiishi ng'ambo.
"Pole" - Mfano Pole na kazi!
Kiswahili is a rich language bwana! (Not very rich)
COLOR="White"].[/COLOR]

Pole na kazi = ?????
 
Kuna mengine kama

Shirt- shati

Ruler - Rula

Gas - gesi

Train- treni au garimoshi

Cents- senti au (kamusi ya Chenge) vijisenti

Shillings- shilingi

Science- sayansi

Nappy- Nepi za watoto

Bus- basi la abiria au kielezi

Dude -Dude au kidude. Hili neno kwa kiingereza linamaanisha mtu mshamba ambae ndio kwanza ametoka kijijini na ameingia mjini na hajui hata kutofautisha mavazi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom