Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #61
Nadhani haya yanayotokea Tanzania ni laana ya aina fulani. Tulilaaniwa na kwa sababu gani, siwezi kuelewa.
Tunalea ujinga sana. zamani sana niliwahi kupost hapa kuwa nadhani tuna ugonjwa wa "Addiction to Mediocrity" Nchi imegubikwa na na watu mediocre sana katika ngazi mbalimbali za muhimmu. Kuanzia wanasiasa (ambao ndio wanaoongoza), wanahabari (ambao ndio wanatakiwa waelimishe umma) na hata wasomi wetu kama REDET, ambao nao wanatakiwa wauelimisha umma; wote wamekuwa na hilo hilo gonjwa la MEDIOCRITY. Sasa kam hao wanasiasa, wanahabari na wasomi wetu wanaimarisha ugonjwa mkubwa katika jamii yetu yaani ujinga, basi Tanzania tutaendelea kuendesha kwenye one way tukielekea upande opposite wa barabara.
Mwalimu, kitu kinachosumbua ni kuwa hawa ndio wasomi wenyewe; ukiuliza CVs zao utakimbia. Ndio maana huwa nawashangaa sana watu ambao huwa wanasema "serikali haisikilizi wasomi" au waliowekwa ni "vilaza" lakini these are the educated ruling elite. Kama hiki kilichoandikwa kimetoka Ikulu, kwanini hakuna mtu anayeweza kuhoji kwanini Ikulu kwa makusudi kabisa inawaongopea wananchi? Kwanini Mhariri wa gazeti huru anapublish uongo akijua ni uongo (au alipaswa kujua ni uongo kwa sababu ukweli ulikuwa uko nje tayari)?