AirTanzania
JF-Expert Member
- Mar 17, 2011
- 1,139
- 1,033
hi ni hatari kwa Taifa kila siku viongozi wanatafuta jinsi ya kuwadanganya wananchi badala ya kuwaletea maendeleo
Msaada Please what U knew about?I knew it!!!
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo wa Uingereza, Andrew Mitchel wamekutana na wamezungumzia kuhusu fedha ambazo Serikali ya Tanzania inadai ilipwe na kampuni ya kuuza silaha ya nchi ya Uingereza ya British Aerospace (BAE).Katika mazungumzo hayo kwenye Ukumbi wa Palace of Conferences katika kijiji cha Sipopo, nje kidogo ya mji mkuu wa Equatorial Guinea uliopo katika Kisiwa cha Bioko, viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea na jitihada za kuishawishi BAE kuilipa Tanzania fedha hizo ambazo ni haki yake.Tanzania inadai kulipwa fedha zake kiasi cha paundi za Uingereza milioni 29.5 zinazotokana na Tanzania kutozwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kile kilichotakiwa kulipwa wakati inanunua rada kutoka BAE.Ununuzi wa rada hiyo ulisababisha matatizo makubwa yakiwemo madai ya rushwa na hatimaye kampuni hiyo ya BAE ilifikishwa mahakamani kwa madai hayo ya kutoa rushwa katika ununuzi wa rada hiyo.Hatimaye mahakama iliamua kuwa BAE haikutoa rushwa isipokuwa kuwa ilifanya makosa katika vitabu vyake vya mahesabu lakini kampuni ikaamuliwa pia kulipa kiasi cha paundi milioni 29.5 kuirudishia Tanzania ambayo ni fedha yake kihalali kwa sababu ilidhulumiwa .Hata hivyo, kampuni hiyo pamoja na kuamuliwa kuilipa Tanzania moja kwa moja, iliamua kutoa fedha hizo kwa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ambayo ndiyo ingeleta fedha hizo Tanzania kwa njia ya kutoa huduma.Tanzania imepinga hatua hiyo na kutoa taarifa kali Bungeni kupinga hatua hiyo ya BEA.Serikali inataka kuziingiza fedha hizo katika kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kununua vitabu kwa ajili ya wanafunzi na kujenga madarasa na nyumba za walimu.Viongozi hao wawili pia wamezungumzia hali iliyopo nchini Libya ambapo Rais Kikwete amemwelezea Bwana Mitchel msimamo wa viongozi wa waafrika ambao unapinga kampeni ya kupiga mabomu inayoendeshwa na majeshi la Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO) dhidi ya Libya.Imetolewa na:Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Safarini,Malabo, Equatorial Guinea01 Julai, 2011
Kaka usisahau wana mpango wa kuimega mbuga ya Selous karibia hecta Elfu 35 kwa ajili ya kuchimba Uranium then hv majuzi wamekataa kujenga bara bara ya lami inayopita mbugani......bado kufa tu.
viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea na jitihada za kuishawishi BAE kuilipa Tanzania fedha hizo ambazo ni haki yake.
nadhani hapa ndio ngoma ilipo. Nashangaa hadi hivi sasa upinzani nchini haujaja na statement ya kueleweka wao wanasimamia wapi au ndio wamelainishwa na maneno ya kizalendo.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo wa Uingereza, Andrew Mitchel wamekutana na wamezungumzia kuhusu fedha ambazo Serikali ya Tanzania inadai ilipwe na kampuni ya kuuza silaha ya nchi ya Uingereza ya British Aerospace (BAE).Katika mazungumzo hayo kwenye Ukumbi wa Palace of Conferences katika kijiji cha Sipopo, nje kidogo ya mji mkuu wa Equatorial Guinea uliopo katika Kisiwa cha Bioko, viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea na jitihada za kuishawishi BAE kuilipa Tanzania fedha hizo ambazo ni haki yake.Tanzania inadai kulipwa fedha zake kiasi cha paundi za Uingereza milioni 29.5 zinazotokana na Tanzania kutozwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kile kilichotakiwa kulipwa wakati inanunua rada kutoka BAE.Ununuzi wa rada hiyo ulisababisha matatizo makubwa yakiwemo madai ya rushwa na hatimaye kampuni hiyo ya BAE ilifikishwa mahakamani kwa madai hayo ya kutoa rushwa katika ununuzi wa rada hiyo.Hatimaye mahakama iliamua kuwa BAE haikutoa rushwa isipokuwa kuwa ilifanya makosa katika vitabu vyake vya mahesabu lakini kampuni ikaamuliwa pia kulipa kiasi cha paundi milioni 29.5 kuirudishia Tanzania ambayo ni fedha yake kihalali kwa sababu ilidhulumiwa .Hata hivyo, kampuni hiyo pamoja na kuamuliwa kuilipa Tanzania moja kwa moja, iliamua kutoa fedha hizo kwa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ambayo ndiyo ingeleta fedha hizo Tanzania kwa njia ya kutoa huduma.Tanzania imepinga hatua hiyo na kutoa taarifa kali Bungeni kupinga hatua hiyo ya BEA.Serikali inataka kuziingiza fedha hizo katika kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kununua vitabu kwa ajili ya wanafunzi na kujenga madarasa na nyumba za walimu.Viongozi hao wawili pia wamezungumzia hali iliyopo nchini Libya ambapo Rais Kikwete amemwelezea Bwana Mitchel msimamo wa viongozi wa waafrika ambao unapinga kampeni ya kupiga mabomu inayoendeshwa na majeshi la Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO) dhidi ya Libya.Imetolewa na:Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Safarini,Malabo, Equatorial Guinea01 Julai, 2011
Author wa hii taarifa ni Salva -- fundi wa kupotosha mambo!
Unajua temeo lilikuwa CDM sasa baada ya kupata ambacho hawakutegemea wamekuwa si wenyekutegemeka katika mambo ya kitaifa wapo busy na matatizo yao ya kichama very hopelessnadhani hapa ndio ngoma ilipo. Nashangaa hadi hivi sasa upinzani nchini haujaja na statement ya kueleweka wao wanasimamia wapi au ndio wamelainishwa na maneno ya kizalendo.
Kumbe kuna WIZARA YA MISAADA,daaaah,yaani hii wizara ni maalumu kwa marais OMBAOMBA kama huyu mdai chenji