Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Yaani baada ya kuandika kote wiki hii nzima bado kuna watu wanaamua kuwapotosha Watanzania kwa makusudi. Ninaamini imeandikwa na mtu wa Ikulu au Mambo ya Nje.
JK, Waziri Uingereza wajadili chenji ya rada
Na Mwandishi maalum
2nd July 2011
Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Misaada ya Kimataifa ya Maendeleo wa Uingereza, Andrew Mitchel, wamekutana na kuzungumzia kuhusu fedha ambazo Serikali ya Tanzania inadai ilipwe na kampuni ya kuuza silaha ya nchi hiyo ya British Aerospace (BAE).
Katika mazungumzo hayo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendelea na jitihada za kuishawishi BAE kuilipa Tanzania fedha hizo ambazo ni chenji iliyotokana na kuuziwa radi kwa sababu ni haki yake.
Tanzania inadai kulipwa fedha zake kiasi cha paundi za Uingereza milioni 29.5 zinazotokana na Tanzania kutozwa kiasi kikubwa zaidi kuliko kile kilichotakiwa kulipwa wakati inanunua rada kutoka BAE.
Ununuzi wa rada hiyo ulisababisha matatizo makubwa yakiwemo madai ya rushwa na hatimaye kampuni hiyo ya BAE ilifikishwa mahakamani kwa madai hayo ya kutoa rushwa katika ununuzi wa rada hiyo.
Hatimaye mahakama iliamua kuwa BAE haikutoa rushwa isipokuwa ilifanya makosa katika vitabu vyake vya mahesabu, lakini kampuni ikaamuliwa pia kulipa kiasi cha Paundi milioni 29.5 kuirudishia Tanzania ambayo ni fedha yake kihalali kwa sababu ilidhulumiwa fedha zake.
Hata hivyo, kampuni hiyo pamoja na kuamuliwa kuilipa Tanzania moja kwa moja, iliamua kutoa fedha hizo kwa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ambayo ingeleta fedha hizo Tanzania kwa njia ya kutoa huduma.
Tanzania imepiga hatua hiyo na majuzi ilitoa taarifa kali bungeni kupinga hatua hiyo ya BEA, Serikali inataka kuziingiza fedha hizo katika kuboresha elimu ikiwa ni pamoja na kununua vitabu kwa ajili ya wanafunzi na kujenga madarasa na nyumba za walimu.
CHANZO: NIPASHE