TFF: Timu za Ligi Kuu zaambulia $42 tu kwenye mechi ya ligi - Sasa Tuanzishe Private League

kichwat

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
1,819
587
Taarifa za leo kutoka TFF zimethibitisha kwamba katika mechi moja iliyochezwa tarehe wikiendi iliyopita, timu zilizocheza ziliambulia TZS 68,000/= kila moja (USD 42), kati ya TZS 460,000+ zilizopatikana siku hiyo.

Trend inaonesha mfumo uliopo wa mpira wa Tanzania HAUNA FUTURE kwa timu zinazoshiriki ligi.

Je, kwanini Watanzania wapenda soka tusianzishe ligi kama ya EPL au KPL? - tutaiita Tanzania Premier League (TPL)

Katika TPL:
1. Idadi ya kuanzia ya timu katika TPL itakuwa ni idadi ya mikoa yote nchini, then timu zitapungua katika msimu unaofuata na kubakiza timu 20 au 18 tu kama ilivyo katika viwango vya kimataifa.

2. Timu za mwanzo zitatokana na mashindano ya 'kombe la mbuzi' yatakayoandaliwa na wadau katika wilaya na mikoa yote nchini. Hii itasaidia kupata timu zenye washabikia wa kweli kutoka maeneo husika.

3. Udhamini wa awali utatokana na kukusanya nguvu za wadau kutoka kila mkoa, ambao watadhamini timu zao.

hii imekaa vipi wadau?

Football is the world's BIGGEST sporting business. It should be the same in Tanzania.
 
Back
Top Bottom