Jinsi sakata la mchezaji wa zamani wa Simba Hassan Ramadhan Kessy kujiunga na Yanga lilivyoshughulikiwa na inayoitwa Kamati ya Sheria na Haki za wachezaji inaonyesha ni namna gani safari ya Tanzania kuondoa ubabaishaji michezoni ilivyo ngumu na hivyo kutishia mustakabali wa maendeleo ya mchezo kwa ujumla. Hata watu wataalamu na wabobezi katika sheria na uongozi wanaotazamiwa kusaidia kuondoa migogoro na ujanja ujanja kwenye michezo, bado wao wanakuwa sehemu ya tatizo.
Suala la Kessy kwa mfano badala ya kumalizwa limeachwa tena pending bila sababu za msingi. Huu ni mlango wa mgogoro na kelele wakati ligi inaendelea. Sehemu ya taarifa ya Kamati inanukuliwa ikisema eti;
"TFF inafuatilia na kuangalia haki ya Simba namna ya kupata haki yake baada ya kuwasilisha madai kuhusu kuvunja mkataba na mwajiri wake wa zamani.
Kanuni hazimzuii mchezaji kuendelea kucheza kwa hoja ya madai badala yake suala hilo linaweza kumalizwa wakati mashindano yanaendelea"
Badala ya watu kufuatilia matokeo na ufundi wa timu ktk ligi, bado kuna nafasi ya kuendelea kufuatilia issue ya Kessy, kwamba leo hivi, kesho vile. Haya ndio mambo ambayo hayana maana sana kwenye mpira. Kamati ilipaswa kufanya yafuatayo tu na kufunga mjadala kabisa;
1. Kujiridhisha kama Kessy alisajiliwa na Yanga huku akiwa bado na mkataba na Simba au la
2. Kama jibu ni ndiyo sheria na kanuni zinasemaje? Alipaswa kulipa fidia? Kiwango cha fidia
wanayodai Simba ni sahihi. Kama sivyo, kipi ni kiwango sahihi?
3. Kuamua kuwa kama madai ya Simba ni kweli, Kessy na mwajiri wake wanapewa muda gani
kulipa kiwango hiki?
4. Kama sivyo, kutupilia mbali madai ya Simba na kumwidhinisha Yanga bila sharti lolote.
Hii ya kuachia vitu nusu-nusu, inatafsirika kama ni kupima upepo, kuona hukumu itapokelewaje. Kama nilisema hapo juu, ni mlango wa kutengeneza zengwe lisilo na sababu wala tija yoyote.
Tujifunze kuongoza vitu kwa utaratibu na kutoa hukumu stahili badala ya kutengeneza mazingira ya kuridhisha kila upande ktk shauri.