Baba Mtu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2008
- 871
- 168
MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesitisha kwa muda utengenezaji, uingizaji, usambazaji na matumizi ya dawa zenye viwango duni vya ubora, baada ya kubainika kwenye ukaguzi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Dawa, matoleo, mtengenezaji na tatizo la dawa hizo kwa mujibu wa taarifa ya TFDA, ni ya sindano ya Gentamycin Sulphate 80mg/2ml Ampules, iliyotengenezwa na Kampuni ya Leshan Sanjiu-Longmarch Pharmaceuticals ya China ambayo maandishi yake kwenye vichupa yanafutika kirahisi.
Nyingine ni tembe za Coldril iliyotengenezwa na Kampuni ya Shelys Pharmaceuticals ya Tanzania toleo la 9041 ambayo tembe hizo zimegandamana; tembe za Pen-V pia za Shelys toleo la 9027 na 9034 ambazo zimebadilika rangi kutoka nyeupe na kuwa njano isiyokoza.
Dawa zingine ni MES Syrup ya ZENUFA Laboratories ya Tanzania toleo LM0021 ambayo inavuja na vifuniko vyake vina kutu; Methyldopa (Dopamet) - 250 iliyotengenezwa na Kampuni ya Medochemie ya Cyprus toleo A3A002 na A3D018 ambayo lebo zake zinabanduka kirahisi na vidonge vyake vimeota kuvu.
Dawa zingine zisizotakiwa ni Phenoxymethylpenicillin Potassium (Medopen) – 250 pia za Medochemie ya Cyprus toleo la P2K049 ambazo zimebadilika rangi nyeupe kuwa ya njano isiyokoza.
Pia tembe za Amoxicillin zilizotengenezwa na Zheijian Holley Nanhu Pharmaceuticals ya China toleo 090901, ambazo ‘blister' ya ndani haina namba ya toleo, siku ya kutengenezwa wala muda wa kwisha matumizi.
Tembe za Doxycyline Hyclate zilizotengenezwa na Zhejiang toleo la 100705 , kasha lake la hifadhi halina siku ya kutengenezwa wala ya kwisha matumizi na huku pakiti yake ikiwa na tarehe zote hizo na dawa nyingine yenye matatizo hayo ni Dyclomax (Diclofenac) iliyotengenezwa na Kampuni ya Medreich ya India toleo namba 460156 ambayo ‘kasha lake pia lina tatizo kama la dawa ya hapo juu.
Kutokana na upungufu huo, wananchi wameonywa wasitumie kabisa dawa hizo huku wenye maduka ya dawa wakitakiwa wazirudishe walikozinunua mara moja na walioziagiza wazitoe mara moja sokoni na kuwasiliana na TFDA wapewe utaratibu wa kuziharibu.
"Pamoja na maelekezo yaliyotolewa, Mamlaka inafanya uchunguzi wa kina kwenye maabara na itachukua hatua zaidi za kisheria baada ya kukamilisha uchunguzi wa dawa hizo," ilisema taarifa iliyotolewa na ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo.
Mamlaka ilitoa muda wa miezi sita kuanzia Januari mosi kwa wahusika wa utengenezaji, uingizaji na usambazaji wa dawa hizo, kuhakikisha kuwa dawa zao hazina udhaifu kama uliobainika na kuwataka wananchi kutoa taarifa mara moja TFDA wanapogundua upungufu kama huo.
"Taarifa zitolewe ofisi za TFDA barabara ya Mandela, EPI Mabibo External, Dar es Salaam na ofisi za Kanda zilizopo mtaa wa Nkrumah, Mwanza, mtaa wa Sakina – Arusha na jengo la ofisi ya Mifugo Mkoa wa Mbeya.
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=13428