TFDA yakamata dawa aina 319 zisizofaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekamata jumla ya aina 319 za dawa bandia na zilizokwisha muda wake zenye thamani ya sh 9,538,970 katika mikoa mbalimbali nchini.

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Kamishna wa Polisi, Robert Manumba, alisema juzi kuwa dawa hizo zilikamatwa katika operesheni maalum ‘Operesheni Mamba II’ iliyohusisha mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Shinyanga, Arusha na Mwanza.

Alizitaja dawa zilizokamatwa kuwa ni dawa za kutibu fangasi aina ya Sofadrex, dawa ya kuongeza nguvu za kiume aina ya Cialis, dawa za viuavijasumu (antibiotics) aina ya Ciprofloxacillin, dawa za kurekebisha homoni aina ya Postinor-2, dawa ya pumu aina ya Aminophylline, mifuko 13 yenye vidonge 1,000 kila kimoja ambavyo havikujulikana ni aina gani kutokana na kukosa nembo.

‘Pamoja na dawa hizo, pia tumefanikiwa kukamata aina 238 za vipodozi vilivyopigwa marufuku, vyenye thamani ya sh 12,555,700, ambapo aina nne kati ya hizo ni ile inayosadikiwa kubadilisha na kuongeza maumbile ya binadamu, ambavyo ni sabuni ya Ivan Mwali, Herbal Skin Doctor, Hip Up Cream na Ardiour sex enhancing medicines.

‘Operesheni hii ilifanyika sanjari katika nchi za Kenya na Uganda kwa kuzingatia makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa kwenye mkutano wa maandalizi uliofanyika Juni 27, mwaka huu jijini Nairobi kwa lengo la kufanikisha operesheni hii kwa nchi za Afrika Mashariki, kutokana na ukweli kwamba biashara ya dawa bandia ni biashara haramu inayovuka mipaka, hivyo inahitaji kukabiliana nayo kwa kushirikiana na nchi tunazopakana nazo,” alisema Manumba.

Alisema operesheni hiyo ni mwendelezo wa Operesheni Mamba ya kwanza iliyofanyika katika nchi za Uganda na Tanzania Septemba mwaka jana na kuhusisha mikoa ya Dar es Salaam, Arusha mjini, Namanga, Mbeya mjini, Tunduma, Shinyanga mjini, Kahama, Mwanza mjini na Geita.

Aidha, Manumba alisema kutokana na matokeo ya operesheni hiyo hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa, ambapo jumla ya majalada 38 ya kesi yamefunguliwa katika vituo mbalimbali.

Awali, Mkurugenzi wa TFDA, Magreth Ndomondo, alisema jukumu la mamlaka hiyo ni kulinda afya za wananchi kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya bidhaa wanazodhibiti, ambazo ni vyakula, dawa, vipodozi na vifaatiba.

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=8445
 
thumbs up TFDA! NI KAZI NGUMU SANA KATIKA KUDHIBITI WA HIZI BIDHAA lakini ukiwepo ushirikiano wa kutosha baina ya regulatory bodies zote za east africa bila shaka tutafanikiwa. ushirikiano wa wananchi nao ni jambo la maana sana kwani wao ndio watumiaji wa bidhaa hizo hivyo iwapo elimu ya kutosha juu ya madhara ya bidhaa hizo ikitolewa bila shaka lengo la TFDA la kuwa the best regulatory body on drugs,food and cosmetics by 2015 will be achieved
keep up the work!!!!!!!
 
Ni kweli kabisa.
Hawa jamaa angalau tunasikia baadhi ya yale wanayoyafanyia kazi. Mko wapi Sumatra? Gari imeandikwa Kkoo - Masaki, inaishia Msasani. Nauli kutoka keko kwenda njia [anda ya kigogo ni 350 bila kujali umbali. Amkeni mmezidi kulala. Hongera sana TFDA
 
TFDA ni kama zima moto, wameshindwa kudhibiti bidhaa zinapoingia nchini na mara zote wamekuwa wakikamata wafanya biashara wadogo wadogo wale wanao agiza bidhaa kwa wingi wahakamatwi.
 
TFDA ni kama zima moto, wameshindwa kudhibiti bidhaa zinapoingia nchini na mara zote wamekuwa wakikamata wafanya biashara wadogo wadogo wale wanao agiza bidhaa kwa wingi wahakamatwi.

Patrick,

Binafsi naona kama huwatendei haki TFDA; you have just swept them aside bila kuwapa nafasi ya kujitetea... kudhibiti bidhaa ziingiazo kupitia borders zetu [air, bandari, borders za magari nk.] kunahitaji jitihada za jumla kutoka vitengo mbalimbali maalum kama vile badhari wenyewe, wakaguzi, TRA, TFDA wenyewe, polisi, FCC n.k.

Matatizo yaliopo ya udhibiti kumbuka yanaathiri mpaka baiskeli, magari, vipuri, toys etc... Yote haya yanareflect systems failure na si TFDA pekee.

Matatizo hayo yanaweza kuchangiwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na pesa, human resources, tools, infrastructure, relationship with other government units pamoja na modalities za kufanya kazi bila muingiliano au mgongano wa kiutendaji

Lets congratulate them for at least kufanya jambo, halafu then tuangalie capacity ya staff wao, na pia capacity ya organization kwa tools, watendaji na infrastructure kuboresha kazi zao
 
Back
Top Bottom