Teuzi vs uwajibishaji wa JK

Posa

Member
Nov 12, 2010
76
79
Kwa muda sasa nimejaribu kujikumbusha hata mtendaji mmoja ambaye rais yeye mwenyewe moja kwa moja amemuwajibisha kwa kipindi chake cha urais nikilinganisha na teuzi alizokwishafanya, sijapata.

Hapa sizungumzii mabadiliko ya jumla kama anapowaacha wakuu wa mikoa/wilaya akifanya mabadiliko, nazungumzia, mfano, wakati wa awamu ya tatu rais wa wakati huo BWM aliwahi kumuwajibisha aliyekuwa mkurugenzi wa PPF kwa manufaa ya umma, nadhani, sina uhakika, kwa sababu ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mfuko.

Naomba tujadili, inaweza ikawa kwa kuorodhesha majina watu waliokwisha wajibishwa vs walioteuliwa au vyovyote mtakavyoona inafafaa. NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom