TETESI: Serikali yatishia gazeti la KULIKONI

hii serikali ingelikuwa inawapigania watz kama wanavyopigana na haya magazeti basi leo tusingelikuwa masikini.....wanataka kutuondosha kwenye point ya ufisadi tu basi
 
Nimemtisha nani, wapi? Mbona unaogopa kabla hujatishwa? Nimeseme kama unaleta kitu ulichoambiwa na chanzo chako huwezi kukiita rumor. Kama wewe mwenyewe humuamini chanzo chako kwa nini utuletee rumor hapa?

Ni rumor au ni kweli mna hakika mmeambiwa kwamba serikali imetoa warning?

- Mkuu badili channel basi usiwe kikwazo kwenye habari muhimu kwa wananchi, hii habari ni ya muendelezo sasa unaizuia mkuu kuendelea, vipi ukisogea pembeni ukatuachia mabwege tuendelee kubugia sharubati, I mean genius anatafuta nini huku JF, badala ya kwenda kufundisha Havard?

- Kama habari ya Halisi ni ya uongo, basi tuonyeshe uongo ulipo mkuu halafu utuwekee ukweli zaidi ya uongo wa Halisi, enough na hizi logics hii topic sio mahali pake, hii habari ni one way street, either una ya ukweli zaidi ya hii habari au kaa ule dataz, ikibidi badilisha channel, acha kuzuia habari mkuu,

Mkulu Halisi lete dataz hapa, yaani sina sababu hata ya ku-question habari yako najua ni 100% true, yaani ukweli.

Respect.

FMEs!
 
Well, ni rahisi: Tetesi ni kitu cha kusikia juu juu ambacho hakiaminiki bado. Sasa kama source yako mwenyewe huiamini, kwa nini ulete habari kutoka kwa mdaku ambaye wewe mwenywe wouldn't bet a nickle on them?

Chanzo chako cha ndani mwenyewe unakiiita rumors, mimi recipient wa info huwezi nilaumu nikiwashuku nyote.
 
Nimemtisha nani, wapi? Mbona unaogopa kabla hujatishwa? Nimeseme kama unaleta kitu ulichoambiwa na chanzo chako huwezi kukiita rumor. Kama wewe mwenyewe humuamini chanzo chako kwa nini utuletee rumor hapa?

Ni rumor au ni kweli mna hakika mmeambiwa kwamba serikali imetoa warning?

Do i know you!
 
Well, ni rahisi: Tetesi ni kitu cha kusikia juu juu ambacho hakiaminiki bado. Sasa kama source yako mwenyewe huiamini, kwa nini ulete habari kutoka kwa mdaku ambaye wewe mwenywe wouldn't bet a nickle on them?

Chanzo chako cha ndani mwenyewe unakiiita rumors, mimi recipient wa info huwezi nilaumu nikiwashuku nyote.
tujadili mada na kama huna mbadala tuache wadanganyika, tumkome nyani.
 
JK amejenga maadui wa kutosha ndani ya chama chake mwenyewe, na sasa anajenga wengine nje ya chama waliomwamini kuwa ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi. Sijui atakapomaliza vipindi vyake vya uongozi ataficha wapi sura. Watu watamla nyama. Aamue sasa kuikamata nchi na kuongoza mwenyewe. Sio lazima kuwa dikteta au kuzima mijadala huru inayoendelea, bali he has to be on top of the things!
 
You know ndugu, he wish he could be! Apite wapi while Fisadi papa Rostamu Azizi is always on his neck?
 
Well, ni rahisi: Tetesi ni kitu cha kusikia juu juu ambacho hakiaminiki bado. Sasa kama source yako mwenyewe huiamini, kwa nini ulete habari kutoka kwa mdaku ambaye wewe mwenywe wouldn't bet a nickle on them?

Chanzo chako cha ndani mwenyewe unakiiita rumors, mimi recipient wa info huwezi nilaumu nikiwashuku nyote.
huo ni mtazamo wako
lakini ukweli siku zote husimama.
ilisemwa ktk maandiko kuwa hata shetani ana mashahidi wake
 
Baada ya gazeti la KULIKONI kuandika tahariri yenye kuonyesha kupingana na taarifa ya serikali, serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, imeelezwa kutoa tishio la kulichukulia hatua gazeti hilo ikiwa halitajitetea.

Upo uwezekano wa gazeti hilo kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufungiwa katika siku chache zijazo. Hii ni sehemu ya vitisho ambavyo kuanzia sasa vitavikumba baadhi ya vyombo vya habari ikiwamo Jamiiforums na mitandao mingine ambayo itaendelea kuishambulia na kuishushia hadhi serikali.

Watendaji wa serikali wamesema walikaa kimya kwa muda mrefu na walimshauri JK (na yeye alisema) kuchukua hatua lakini akadharau na sasa nchi imekuwa katika "matatizo" makubwa kwa muda mrefu na hivyo sasa ni wakati mwafaka kuchukua hatua za NGUVU NA HARAKA. "Baadhi ya hatua zimekwisha kuchukuliwa," anasema mtoa habari wa JF ndani ya serikali.

Tahariri iliyoikera serikali ndiyo hii:

Serikali iwe wazi, kuna kesi ngapi za mafisadi kortini?

TAMKO la Serikali lililotolewa jana kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuhusu mjadala ulioibuka hivi karibuni kuhusu tuhuma za ufisadi nchini imeacha maswali mengi kuliko majibu katika muktadha wa utawala wa sheria nchini na mapambano dhidi ya wizi wa mali ya umma. Serikali badala ya kutoa mwongozo, imeonekana kujitoa na zaidi kuwatisha wananchi na wapambanaji kwa kutumia mwanasesere.

Baada ya kutumia muda mwingi kueleza kuwa mjadala unaoendelea sasa ni 'malumbano ya Rostam Aziz na Reginald Mengi,' na yanayohatarisha usalama wa Taifa, Serikali kupitia tamko hilo lililoandikwa na kusainiwa na Waziri George Mkuchika lakini katika mazingira tata likasomwa na Naibu wake, Joel Bendera, ilionekana kushindwa kuonesha hasira zake na kutimiza ahadi zake za kuchukia ufisadi badala yake ikajidhihirisha kuwa imeanza kusita.

Serikali hiyo hiyo kupitia tamko hilo hilo moja baada ya kuutaja mjadala huo kuwa ni 'malumbano' ikaishia kutoa ushauri kuwa wahusika wapeleke hoja zao kwenye vyombo husika vya dola. Tunajiuliza 'malumbano yasiyo na tija' yatapelekwa vipi kwenye vyombo vya sheria?

Lakini katika moja ya mambo ambayo tumelazimika kuyasemea ni kuhusu aya moja katika tamko hilo la Serikali ambayo ukiitazama vyema haiwiani na mfululizo uliokuwa awali kwenye aya nyingine- hii ni kama imeingizwa ghafla ikionekana kumlaumu moja kwa moja Mengi kwa kutaja mafisadi na kumtishia kwa 'kuvunja' sheria huku ikishindwa kutoa tamko lolote kuhusu waliotuhumiwa kwa ufisadi-aliyeibiwa simu ndiye anaitwa mwizi.

Katika aya hiyo tamko hilo linasema: “Serikali imesikitishwa na kitendo cha Reginald Mengi cha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu , watu kuzungumzia ama kujadili suala ambalo tayari liko mahakamani.

“
Kwa kufanya hivyo Bwana Reginald Mengi amewahukumu watuhumiwa hao na kuwatia hatiani bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa (They have been condemned unheard). Kwa mujibu wa sheria za nchi, mahakama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhumiwa.

Kauli hiyo imetushangaza, kutustusha na kutulazimisha kurejea kwenye kile alichokisema Mengi ambacho baada ya waliotuhumiwa kujitahidi kukipotosha sasa, Serikali nayo inayopaswa kuwa kati, nayo inaingia na kuonekana ikishiriki kupotosha zaidi.

Kwanza tuweke wazi jambo moja-Mengi katika taarifa yake ya kuandika orodha ya watuhumiwa aliowaita wa ufisadi papa alikuwa akijua alichokuwa akikisema na pia alijua kwamba ukiacha sheria za daawa (civil law) zitakazowapa watuhumiwa hao haki ya kumshitaki kama wataona amewakashifu, hakuna sheria ya nchi hii na yoyote inayomzuia raia mwema kuwataja watu ambao anaamini wanahusika na makosa ya jinai.

Tofauti na Serikali kujaribu kupotosha kuwa Mengi 'kahukumu,' rejea ya tamko lake inaonesha kuwa alitumia neno “watuhumiwa.” Je, kuna kosa gani hapo kuwataja watuhumiwa tena kwa kujitolea ili wachukuliwe hatua?

Hoja hiyo inatufikisha katika kujadili kauli tata ya “sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama kujadili suala ambalo tayari liko mahakamani....”

Kwanza tungeomba Watanzania waelimishwe ni sheria gani ya nchi hii inayokataza “mtu,watu kuzungumzia suala ambalo liko mahakamani,” kama ilivyodai serikali.

Utafiti wetu umeshindwa kubaini hilo na kwa kuwa limekuwa likitumika kama ngao ya kuwanyima wananchi haki ya kujadili masuala ya msingi kitaifa tunadhani ni vyema hilo likawekwa wazi.

Sisi wa KULIKONI tunafahamu ipo dhana ya kisheria ya uhuru wa mahakama ambayo pia ina kipengele ndani yake cha kutaka mahakama isiingiliwe katika kufikia uamuzi wake. Lakini kwa bahati mbaya, tofauti na inavyoelezwa, dhana hii haikatazi watu “kutaja” suala lililoko mahakamani wala “kujadili.”

Kinachozuiwa kupitia dhana hiyo ni kutoa ushahidi au kutaja masuala ambayo yanaweza kuifanya korti ishawishike kuamua vinginevyo, hakuna mahala panapokataza “kutaja” wala “kujadili.”

Jaji Willem van der Merwe aliyekuwa akisikiliza kesi ya tuhuma za kubaka dhidi ya Rais wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ni mmoja wa majaji waliotoa jibu ambalo Serikali ya Tanzania inapaswa kulitafakari kama kiigizo na msimamo jadidi ambao mahakimu na majaji wote nchini wanaujua kuliko kuwatisha wananchi kwa kuunda makosa ambayo hayapo katika sheria yoyote.

Ikiwa kesi hiyo imejadiliwa sana kwenye vyombo vya habari, mitaani, kwenye tovuti na blogu, Mei 8, 2006 aliposoma hukumu hiyo, Jaji huyo alikiri kuwa yeye akiwa mwanajamii hakusita kuisikiliza mijadala mbalimbali nje ya mahakama wala kukwepa kutazama mijadala kwenye televisheni, lakini mwishowe alihukumu kesi hiyo si kwa kutumia mijadala hiyo bali ushahidi uliowasilishwa kortini na pili sheria za nchi na si vinginevyo.

Mkuchika awaeleze wazi Watanzania ni sheria gani inayounda kosa la “kutaja” au “kujadili” kesi zilizoko mahakamani?

Tamko la serikali pia limesema Mengi amejadili masuala yaliyoko mahakamani, baada ya kuona kuwa hakuna mantiki kusema watu hawana haki ya kujadili masuala yaliyoko mahakamani, pia tuzungumzie sasa kauli hii japo kwa uchache.

Wananchi wengi wanaamini kuwa Serikali ina watu makini na wanaofanya kazi kwa viwango. Tamko la jana limedhihirisha hali ni tofauti.

Wakati Serikali ilitarajiwa ingetoa tamko lililofanyiwa utafiti, jana imeonekana kukariri maneno yale yale yaliyotumiwa na baadhi ya watuhumiwa na mashabiki wao waliochangia mjadala wa ufisadi kwa kutoa madai potofu kuwa Mengi kataja masuala ambayo yako mahakamani. Hebu twende pamoja katika hili.

Watuhumiwa watano waliotajwa kwa ufisadi papa ni Rostam Aziz, Yusuph Manji, Subash Patel, Tanil Somaiya na Jeetu Patel.

Katika watuhumiwa hao ni mmoja tu ambaye kwa sasa walau yuko mahakamani tena kwa kesi ya ufisadi wa EPA, Jeetu Patel, ambaye katika tamko la Mengi hata hivyo hakuna mahali, tuchukulie kuwa ni kosa kutaja suala la mahakamani, alipotajwa au kujadiliwa na Mengi kwa sababu ya kesi yake hiyo iliyoko sasa mahakamani.

Watuhumiwa waliobaki, kwa sasa hawana kesi yoyote mahakamani ya kuhalalisha 'kosa' la Mengi kama lilivyoelekea kufanya tamko la Serikali. Sasa kimetumika kigezo gani kusema kwamba watuhumiwa hao wamehukumiwa kabla mahakama haijafanya hivyo?

Je, huku si kurudisha nyuma kwa dhahiri mapambano dhidi ya ufisadi, mapambano ambayo wananchi wamekuwa wakiambiwa washiriki kwa kuwafichua waovu?

Je, huku sio kulinda mafisadi kwa mlango wa nyuma? Je, huku si kuacha sheria nzuri na dhana nzuri ya utawala wa sheria ambayo haiwapi mafisadi nafasi na kuanza kukumbatia 'sheria za watawala' zinazowapa ahueni mafisadi?

Tunachoweza kuishauri tu kwa sasa Serikali ni kwamba wanafalsafa na wahenga wameshaonya: “Unaweza kuwapumbaza watu wachache tu na kwa muda mchache, lakini huwezi kuwapumbaza watu wote na kwa muda wote.”

Mh!! Ure tryin' 2chase the***?
 
Sawa kabisa, unachunguza, dadisi, swalisha, chambua, hoji, thibitisha every darn thing kinachosemwa na serikali, waleta data, wapinzani, waandishi, wazabuni, prosecutors, waheshimiwa, wanavijiji na wanahalisi.

Tumeshaamka sasa hivi Watanzania. Hatuamini amini tena na kubugia kila tunachopewa kama maji ya sharubati.

Huwezi kuja kusema umeambiwa siri na leak source mmoja huko lakini ni tetesi mpaka serikali itamke. Aidha umeambiwa au hujaambiwa, tetesi.

Unajua maana ya "swalisha" weye?
 
Mbele yangu hapa nina kamusi ya Kiswahili toleo la kwanza 2001, ISBN 9976 911 44 0 iliyotolewa na TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) na neno "swalisha" lina maana moja tu!!
 
Back
Top Bottom