TETESI: Pendekezo la Maalim Seif kuhudhuria vikao vya NEC na CC laleta mgawanyiko CCM

Jamani wana JF tulikwisha sema kwamba CUF siyo wapinzani ni chama tawala ndiyo maana tukawafukuza kwenye kambi rasmi ya upinzani Bungeni. Japokuwa walilazimisha kubadili na kutengua kanuni za Bunge lakini haikusaidia. Mwancheni audhulie vikao vya CCM ili kwenye uchaguzi tuwagalagaze wote.
 
Tatizo liko wapi mke anapotaka kuingia chumbani kwa mumewe? Muacheni aende ili ndoa ikamilike vizuri!
 
CUF ni sehemu ya chama cha wakoloni weusi,wanaongozwa na sera za CCM kwa hiyo sishangai hata kidogo mana ni part and parcel ya CCM.
 
Mwee, yaani mmeacha kazi mnajadili Maalim Seif ?Yule mtu mwengine, achanane nae kabisa ni mkombozi wetu huku Zanzibar.Safari hii hatukupigwa hata makofi na jwtz, wakati miaka yote tunakula kichapo halafu mnakaa mkitucheka....Aaagh wahenga wamesema pilipili usoila, yakuwashia nini!

Duuh kweli! Zanzibar sasa ni wilaya!
 
Hizi siyo tetesi huu ni uwongo, unafiki, uzandiki na upotoshaji !!!
 
Ni sawa na mwanamke aliyeolewa halafu anakataa kuitwa kwa surname ya mumewe..CCM+CUF=GAMBA LILELILE.
 
Jamani eeh- hii nimepata kali sana. Kuna habari zinasema kwamba lipo pendekezo katika kamati kuu za CCM, yaani NEC na CC yake kwamba Maalim Seif awe anahudhuria baadhi ya vikao hivyo kama observer (mtamazaji).

Wazo hili limepingwa na wengi ndani ya vikao hivyo. Na katika CUf kwenyewe kuna mgawanyiko katiko hilo, Profesa akilipinga sana ingawa kina hamad Rashid na Jussa wanaliafiki.

Msianze kuniuliza source, source ni 'mndani' wangu aliye ndani ya both NEC na CC ambaye kanidolezea.

Kama hii source yako ina ukweli basi mimi sioni tatizo kwa hilo pendekezo la Maalim Seif. Kumbuka kuwa Maalimu Seif ni makamu wa kwanza wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar ambapo CCM Zanzibar na CUF wanashirikiana kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM inayotungwa na kusimamiwa na CC na NEC ya CCM. Sasa kuna ubaya gani kumualika Makamu wa raisi wa Zanzibar ili apate maelekezo sahihi ya utekelezaji wa ilani ya CCM toka kwa watunzi wenyewe?
 
Jamani eeh- hii nimepata kali sana. Kuna habari zinasema kwamba lipo pendekezo katika kamati kuu za CCM, yaani NEC na CC yake kwamba Maalim Seif awe anahudhuria baadhi ya vikao hivyo kama observer (mtamazaji).

Wazo hili limepingwa na wengi ndani ya vikao hivyo. Na katika CUf kwenyewe kuna mgawanyiko katiko hilo, Profesa akilipinga sana ingawa kina hamad Rashid na Jussa wanaliafiki.

Msianze kuniuliza source, source ni 'mndani' wangu aliye ndani ya both NEC na CC ambaye kanidolezea.

Kama kweli una source ndani ya CC na NEC si ungeshamaliza kitendawili alichotuletea William Malecela kuhusu Chenge. So far habari tulizoletewa za CC bado zina utata halafu weww unakuja na habari mpya na kudai source yako ya ndani. Mimi naona unatuingiza mjini tu kama William.

Halafu hili ya sorce iko ndani ya both NEC na CC sijui una maana gani?? Wote tunajuwa kuwa mjumbe wa CC ni automatic mjumbe wa NEC but not the other way around. sasa hapo ulikuwa unajaribu ku-underline ili kuonyesha umuhimu wa hiyo source au??
 
Back
Top Bottom