TETESI: Pendekezo la Maalim Seif kuhudhuria vikao vya NEC na CC laleta mgawanyiko CCM

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Jamani eeh- hii nimepata kali sana. Kuna habari zinasema kwamba lipo pendekezo katika kamati kuu za CCM, yaani NEC na CC yake kwamba Maalim Seif awe anahudhuria baadhi ya vikao hivyo kama observer (mtamazaji).

Wazo hili limepingwa na wengi ndani ya vikao hivyo. Na katika CUf kwenyewe kuna mgawanyiko katiko hilo, Profesa akilipinga sana ingawa kina hamad Rashid na Jussa wanaliafiki.

Msianze kuniuliza source, source ni 'mndani' wangu aliye ndani ya both NEC na CC ambaye kanidolezea.
 
Kama wamefikia uko CUF sio wenzetu!
<br />
<br />

Kwani maalimu wangu hukumsikia yule mbunge wa CUF aliyesema bungeni juzi jioni kuwa wao CUF si wapinzani kama CDM?

Hao si wenzetu na kamwe hawawezi kuwa wenzetu kwa kuwa wapiganaji wa kweli hatuna unafiki!
 
aliye toa hilo wazo anaijua vizuri CUF (kuwa ipo chini ya nani) ili kuwaua kabisaaa wamwalike Maalimu apate Posho za vikao na hivi tunaambiwa aliwa na njaa utaona hata bara ambako kunaonekana kuna unafuu kuwa ni wapinzani nako kutakufa Ktk hili Prof ahame Chama tu ila kama kweli yeye ni mpinzani
 
Mwee, yaani mmeacha kazi mnajadili Maalim Seif ?Yule mtu mwengine, achanane nae kabisa ni mkombozi wetu huku Zanzibar.Safari hii hatukupigwa hata makofi na jwtz, wakati miaka yote tunakula kichapo halafu mnakaa mkitucheka....Aaagh wahenga wamesema pilipili usoila, yakuwashia nini!
 
Waliotoa wazo hili wako sahihi kabisa.Kwani CUF si CCM tu kuna tofauti gani.CUF wameshawekwa kwapani na CCM,kwishney.
Jamani eeh- hii nimepata kali sana. Kuna habari zinasema kwamba lipo pendekezo katika kamati kuu za CCM, yaani NEC na CC yake kwamba Maalim Seif awe anahudhuria baadhi ya vikao hivyo kama observer (mtamazaji).

Wazo hili limepingwa na wengi ndani ya vikao hivyo. Na katika CUf kwenyewe kuna mgawanyiko katiko hilo, Profesa akilipinga sana ingawa kina hamad Rashid na Jussa wanaliafiki.

Msianze kuniuliza source, source ni 'mndani' wangu aliye ndani ya both NEC na CC ambaye kanidolezea.
 
sharif ndie mwanasiasa bora kwa sasa kwani hivi sasa hapa Tanzania ni makamu wa kwanza wa urais na 2015 ni Rais wa Zanzibar, hivyo ni vijiba moyo.
 
Hiyo naona kama haiwezekani na kama ni kweli basi siri nyingi za chama zitavuja hivyo kuwaongezea nguvu CUF.
 
Maalim Seif anaielewa vyema CCM alikuwa CCM wakamtosa,wakamkashifu,wakamnyanyasa,wakamtesa, wakamshtaki, wakamweka kizuizini miaka nenda miaka rudi.Yamemkuta mengi, mwaliko hauna maana sana kwake labda CCM wanataka kujikosha kwa yale waliomtendea.
 
Sasa cha ajabu nini ? Ni kawaida ndoa kuishia chumbani, ebo !
 
Tatizo la maalim ni njaa na uchu wa madaraka!!! really the man is not after saving the peple he is after popularity and his stomach...CUF kwishney

Jaman where is julius mtatiro.
 
Back
Top Bottom