Tetesi: Nape na Mwigulu Waandaa Mkutano Igunga

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Kuna tetesi Nape na Mwigulu wameandaa mkutano Igunga ambao utahutubiwa na vijana hao siku ya Jumapili 09/09/2012.
Cha muhimu wananchi wa huko wategemee nini kipya kutoka kwa hawa jamaa kama sio matusi stori za mauaji ya Moro na Iringa na kingine labda watatoa tamko la Chama kukata rufaa juu ya kupinga kwa kafumu kutenguliwa ubunge wake.
lakini cha kushangaza Mwigulu baada ya Ushindi alitoa kauli chafu kwa wanchi wa Igunga kwa kusema WAMEPIGA MBWA NA MWENYE MBWA sasa sijui ataitengua vipi kauli hii ambayo wananchi wengi bado ipo mioyoni mwao
 
Kwa nini ccm inaendelea kujipaka masizi? hivi hawana watu, hawajui kwamba mwigulu ni miongoni mwa waliosababisha ccm kukosa majimbo-Arumeru&Igunga?
 
Kafumu mwenyewe keshajikatia tamaa zamani, hao wanakumbuka shuka wakati kumekucha,

wameshajua hawawezi kushinda rufaa wala kushinda uchaguzi kama ukirudiwa, hapo ni mpango wa Nape kuendelea kula posho tu.
 
Yaani hao wawili na ule mtambo wa matusi made in mtera ndio wanatusaidia kukiua hicho chama
 
jaman naomba kuuliza!!
unatakiwa kukata rufaa baada ya muda gani hukumu ikishatolewa?
 
Mwigulu anaenda kwa ajili ya kiburudisho cha kada wa magamba alichokuwa akijinoma kipindi kafumu anafumuliwa,amekimiss kweli kiburudisho hicho
 
CCM kwishney habari yake huko Igunga. Bila shaka Rostam anashangilia moyoni. Hao waganga njaa wa CCM wanajipatia per diem zao warudi mjini kutumia.
 
CCM kwishney habari yake huko Igunga. Bila shaka Rostam anashangilia moyoni. Hao waganga njaa wa CCM wanajipatia per diem zao warudi mjini kutumia.

kumbe uko zamu wewe,naogopa kuendelea kuusoma uzi huu ngoja niwe guest kwanza
 
Tutasikia mengi safar hii. Yote hii kulazimisha watu waamini mwangosi kauliwa na cdm. Sasa kwa taarifa yako nape watu wameshtuka. Kama unabisha nenda kahutubie uone aibu yako.
 
Kuna tetesi Nape na Mwigulu wameandaa mkutano Igunga ambao utahutubiwa na vijana hao siku ya Jumapili 09/09/2012.
Cha muhimu wananchi wa huko wategemee nini kipya kutoka kwa hawa jamaa kama sio matusi stori za mauaji ya Moro na Iringa na kingine labda watatoa tamko la Chama kukata rufaa juu ya kupinga kwa kafumu kutenguliwa ubunge wake.
lakini cha kushangaza Mwigulu baada ya Ushindi alitoa kauli chafu kwa wanchi wa Igunga kwa kusema WAMEPIGA MBWA NA MWENYE MBWA sasa sijui ataitengua vipi kauli hii ambayo wananchi wengi bado ipo mioyoni mwao

Nini mikutano waambatane na fiesta nchi nzima kama wanahisi ni suluhisho.
 
wote hao ndio wanaokigawa chama cha mapinduzi kwa propaganda mgando
 
Back
Top Bottom