Tetemeko la Ardhi Bukoba: Rais aahirisha kwenda Zambia, kuwakilishwa na Makamu wa Rais

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,169
103,628
Habari za hivi punde ni kwamba Rais Magufuli ameahirisha kwenda Zambia badala yake kuungana na watanzania katika kipindi hiki kigumu baada ya mikoa ya Kagera na Mwanza kukumbwa na tetemeko la ardhi lililosababisha vifo na majeruhi pamoja na kuharibu mali.

Rais atawakilishwa na Makamu Samia Suluhu



image.jpeg
 
Rais JPM amefuta safari ya Zambia kwa ajili ya kuapishwa kwa rais mteule Edger Lungu ili kuhudhuria mazishi ya wahanga waliokufa kwa tetemeko.
 
Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ameahirisha safari iliyokuwa imepangwa ya kwenda ziara ya siku tatu nchini Zambia pamoja na kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mteule wa Zambia. Hii ni kutokana na kutokea kwa tetemeko la Ardhi, kwa hiyo Makamu wa Rais ndiyo atahudhuria kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Rais wa Zambia. Chanzo; ITV HABARI.
 
Habari zilizotufikia wanaJF hivi punde ni kwamba Rais Magufuli ameahirisha kwenda Zambia badala yake kuungana na watanzania katika kipindi hiki kigumu baada ya mikoa ya Kagera na Mwanza kukumbwa na tetemeko la ardhi lililosababisha vifo na majeruhi pamoja na kuharibu mali.Rais atawakilishwa na Makamu Samia Suluhu
Wana JF kilio chenu kimesikika labda ataendelia kuwasikia na mengine.
 
Back
Top Bottom