Teophil Makunga umejidhalilisha mno kutumiwa na Nchimbi

tuangalie na tuhukumu yaliyomo ktk ripoti. Theophil ni sehemu ya wajumbe na labda alikuwa na msimmamo wake binafsi ila alielemewa na wajumbe wengine
mpeni heshima yake.

.
Paka ana heshima yake ya kuitwa 'paka' vinginevyo ukimwita kuku utakuwa umemvunjia heshima. Msaliti ni jina la sifa stahiki kwa Theo.
.
 
Dr Ulimboka umemuonea, hana bei, bei yake ni damu yake, soon amesema ataongea na kuanika yote anayoyajua kuhusu watesi wake.
Kumbuka waliposhindwa kumnunua, wakamtesa.
Alihitaji kujipanga kwanza, ndipo aseme.

Mkuu hilo hata mimi nimelisikia lakini kwanini anatishia kufanya hivyo?Je akikaa kimya na asitimize ahadi yake, wewe na mimi tutahisi nini lilikuwa lengo la kutishia kufanya hivyo na bila shaka tutajiuliza ni nini kimemfanya asitimize ahadi yake.

Mkuu hili tishio lake mimi nalitizama kwa mtizamo wa mashaka sana.
 
Niliangalia ITV wakati sehemu ya hii ripoti ikisomwa kwenye taarifa ya habari, hata wajumbe walikuwa wanaonekana wazi kuwa na aibu kwa uwongo waliokuwa wamelazimishwa kuusoma. Yule Jaji ndiyo kabisa alionekana kituko. Waandishi walipojaribu kuihoji Nchimbi akaingilia kati kusema eti hawawezi kuweka hadharani mambo yote kwa sababu watakuwa wametoa hukumu wakati jambo liko mahakamani. Sasa kulikuwa na sababu gani kuunda hiyo tume?.
 
Dr Ulimboka umemuonea, hana bei, bei yake ni damu yake, soon amesema ataongea na kuanika yote anayoyajua kuhusu watesi wake.
Kumbuka waliposhindwa kumnunua, wakamtesa.
Alihitaji kujipanga kwanza, ndipo aseme.

...kwa nini asiyeseme hiyo siku aliposema ataanika yote anayojua kuhusu watesi wake? ana haja gani ya kutoa taarifa kwanza? Si akae kimya tu huko alikokuwa na akitoka anatoka kikweli kweli badala ya kutoa taarifa kuhusu kutoa taarifa??????? Unafiki kwa kwenda Mbele!

Simshangai Makunga, kwani Channel ten wenyewe walimkana mwandishi wao baada tu ya kuuawa,

na walishabikia sana uongo uliokuwa umeanza kuenezwa na polisi kwamba mwandishi aliuawa na kitu kilichorusha kutoka kundi la watu na kumlipua Mwangosi
.

So Kama Channel ten walikuwa na bei sembuse Makunga.

....Yaani Mkuu Kapotolo zile Picha zisingekuwepo wote hawa wangekuwa wamekula King. Zile picha zimewaumbua sana na kuuweka hadharani Unafiki Wao!!
 
...kwa nini asiyeseme hiyo siku aliposema ataanika yote anayojua kuhusu watesi wake? ana haja gani ya kutoa taarifa kwanza? Si akae kimya tu huko alikokuwa na akitoka anatoka kikweli kweli badala ya kutoa taarifa kuhusu kutoa taarifa??????? Unafiki kwa kwenda Mbele!

Ametoa taarifa ili kuujuza umma kinachofuata, na kuziba ombwe la ukimya wkt anajipanga.
 
A MAN CAN NOT BE GLAND WITHOUT MONEY BUT MONEY DOES NOT MAKE A MAN TO BE GLAND wewe kula za ncimbi kaka
 
Namheshimu sana Makunga, ni mtu mwema na mwadilifu lakini sio SHUPAVU. Naamini wapo wanahabari wengi wenye uwezo na ushupavu wa hali ya juu waliostahili kuwemo kwenye kamati hii (ingawa tangu mwanzo sikukubaliana na wazo la kuunda kamati).

Tukio la kuuawa kwa Mwangosi kule Nyololo lilirekodiwa vizuri sana kwenye kamera, na kilichotakiwa ni kuwakamata waliomuua na kuwafikisha mahakamani badala ya kutumia pesa za walipa kodi kuwalipa wajumbe feki wa hii kamati.

Lakini pia ndani ya ile kamati alikuwepo mwanahabari mwingine Pili Mtambalike, ambaye ni intelligent na hana tamaa za kijinga za fedha. Sijui ilikuwaje mpaka naye akakubaliana na upuuzi huu.
 
nahisi harufu ya mpasuko wa wanahabari/vyombo vya habari kote nchini, sina tatizo sana na report coz ni kitu ambacho nilikitegemea na ingekuwa bora zaidi kama ingekabidhiwa kimyakimya na nchimbi nae akapiga danadana zake mambo yakaisha kuliko kuipa promo kwenye media, kubwa zaidi ni uwepo wa mtu kama T.Makunga kwenye ile kamati na mwisho wa siku na yeye akahusika kuandaa a useless report kama ile, labda tusubiri reaction ya waandishi/vyombo vya habari, but kwa kifupi wanachojaribu kufanya ni kujisafisha tu[/QUOTE
Nina imani wanahabari hawawezi ku react chochote kwani wote wanafahamiana kuwa wanaishi kwa kutegemea bahasha za khaki, Kama unabisha waite siku moja kwenye issue yako yoyote, utakutana na swalila kwanza. Je, vipi huyu jamaa anaeleweka au ametuleta kwenye blablaa tu?? Fuatilia.
 
Hata mimi nilikuwa namkubali sana mzee huyu ila kwa ripoti hii ya kujipendekeza sina imani nae tena.TUNASUBIRI TAMKO LA WAANDISHI NA VYAMA VYAO KAMA NAO WATAGEUKA KUWA WASALITI.
 
Lakini Tundu Lissu alisema Jaji Ihema hawezi kufanya kazi hii na imejionyesha dhairi katika ripoti hii.
 
Ametoa taarifa ili kuujuza umma kinachofuata, na kuziba ombwe la ukimya wkt anajipanga.

...That is what Hypocrites,Politicians et al always do. Kutoa tu Taarifa with nothing Much being done. :blabla: :blabla:
 
Nilikuwa na imani kidogo baada ya kuona watu kama makunga ktk kamati ile lakini matokeo niliyoyaona nipo mdomo wazi hadi leo.Kwa kweli Tido tunakwamini sana,ebu chukua hatua dhidi ya huyu makunga ameaibisha sana.looooo!!!!!
 
No wonder siku hizi gazeti la mwana wa nchi limepoteza sifa kwa kuandika habari kiutata sana na kupoteza hadhi yake kama chombo huru cha habari. Nikiangalia timu ya mwana wa nchi sasa hivi mkulu T ido, mhariri Mau kunga mwandishi Mee na (mtetezi wa Nchi mbili Jangw ani). Mwanahalisi halipo mitaani yaani tumebakiwa na Raia Mwema tu ambalo linatoka mara moja kwa wiki. Sasa sijui tutapata wapi habari huru za kila siku maana naona kama Mwana wa nchi mafisi adi washafika bei.
 
Ni aibu yaani naona hata waziri alikuwa anajiumauma aliishia kusema kuwa siyo kila kitu kimewekwa wazi baada ya kuona miguno imezidi

  • A%20S%20embarassed.gif
    • A%20S%20embarassed.gif
      • A%20S%20embarassed.gif

Baada ya kusoma ripoti ya kamati ya Kitchen Party ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi nimebadili msimamo wangu wa jinsi nilivyokuwa namkubali sana Mhariri huyu wa gazeti lenye heshima ya mgongo wa chupa la Mwananchi.

Pia mtazamo wangu dhidi ya gazeti hili kuwa ni objective umebadilika pia, Mwanahabari mwandamizi kama Makunga kushiriki kuandika ripoti nyepesi kama ile, yenye kila viashiria vya elimu ya Ngumbalu kwa walioshiriki kuiandika ni kujidhalilisha na kujivunjia heshima. Nchimbi kakutumia kujisafisha na kulisafisha jeshi lake lakini aliyepoteza credibility ni wewe.

Sijui tatizo ilikuwa ni posho ya ushiriki wa kazi za tume lakini hii report ni nyepesi mno, no wonder jaji Ihema alishindwa kuandika hukumu wakati jaji.

Tumekwishapata Salva Rweyemam mwingine
 
Kumbe ni kweli; Never judge a book by its cover, kumbe hata Theophil Makunga ni mchumia tumbo?1 lol salala!
 
Asingekuwa na mwanya wa kuwa tofauti kwani Kamati ilitekwa na watendaji wa Sirikali. The government employees should have been pervasive.
 
Yaani mkuu, nia aibu sana sana, Looo! Afu ITV wamewavua nguo kabisaaa, kwani wakati wanasoma hiyo taarifa yao ya kupika kwamba polisi hawakuhusika, hapo hapo wakawa wanaonyesha ile picha walo mzingira na mmoja akimuonyesha mtutu ulo mmaliza, yaani hata mtoto mdogo wa darasa la nne aloona ameniuliza hivi mbona picha inaonyesha polisi wanaua halafu ripoti inadai hawakuhusika? ... ni aibu aibu na nadhani ni haki yao hata wakipta mtaani tuwazomee!

Mtoto wangu wa miaka 3 na miezi 8 baada ya kuona tukio la polisi kumpiga Daudi akaniambia mbona polisi wamemua mtoto wa Mbowe ? Nikamwambiaa ni mwandishi anauawa na polisi wabaya.
 
Back
Top Bottom