Tendwa: Sitashangaa siku wapinzani wakichukua nchi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amesema hatashangaa siku moja vyama vya upinzani vikishinda uchaguzi na kushika madaraka.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuhusu maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini, Tendwa alisema "kushika dola ndilo lengo la kila chama cha siasa".

Alisema yeye akiwa mlezi wa vyama vya saisa nchini angefurahi kuona vyama hivyo vinakua na kutimiza lengo la kutwaa dola au nafasi za uongozi katika mamlaka mbalimbali za nchi.

"Hili haliwezi kuwa ni jambo la kushangaza, sheria iko wazi kabisa kwamba lengo la kila chama cha siasa ni kushika dola au kuongoza mamlaka nyingine za kiserikali kwa mujibu wa sheria za nchi, na mimi nikiwa mlezi wa vyama vya siasa kama mlivyosema ningefurahi wapambane washinde ili wasifanye fujo,"alisema Tendwa.

Kuhusu miaka 20 ya demokrasia ya vyama vingi nchini, Msajili huyo wa Vyama vya Siasa alisema maadhimisho hayo yataanza Julai 1, mwaka huu na kwamba yatatumika kufanya tathmini ya zama na matukio mbalimbali yaliyotokea katika kipindi hicho pia mchango wa vyama vingi katika demokrasia ya nchi.

Tendwa alisema katika uzoefu wake akiwa msajili wa vyama vya siasa amebaini kuwapo kwa umuhimu wa sheria ya vyama kufanyiwa marekebisho makubwa ili kuongeza tija ya uwapo wa ofisi yake na vyama hivyo kwa ujumla wake.

Alisema katika mchakato wa uandishi wa Katiba Mpya, watapendekeza Msajili wa Vyama vya Siasa na naibu wake baada ya kuteuliwa waidhinishwe na mamlaka nyingine kama Bunge ili kuwapa nguvu ya kiutendaji na uwajibikaji.

"Hili litaondoa lawama za mara anafanya hili au lile ili kumridhisha fulani kwani aliteuliwa na Fulani, kwahiyo sisi tunadhani mtu akiidhinishwa na chombo kingine basi anakuwa na uhuru wa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa ufanisi zaidi," alisema.

Kuhusu vyama vya siasa, Tendwa alisema lazima uwapo utaratibu wa vyama visivyo na tija ‘kushuka daraja' kila baada ya uchaguzi kufanyika na kwamba hatua hiyo itavilazimisha vyama vyete kufanya shughuli za kisiasa.


CHANZO: Tendwa: Sitashangaa siku wapinzani wakichukua nchi
 
Ipo siku hata JK atakubali kuwa nchi itaweza kwenda upinzani muda wowote atabakia Nape tu maana anaogopa hata kivuli chake!!Membe,Tendwa wanajua nini kinafuata!Tendwa ameonyesha kuwa baadhi maamuzi yake yanawabeba waliomteua hana jinsi!!anaomba katiba ione hilo!!
 
Maana wapinzani wanaachia mianya ambayo ingewawezesha kuchukua nchi hata kupitia Tahrir.
 
Kasoma upepo nae sasa anajifanya mtabiri kama shekh yahya!ilo lipo peupe hata akiwasaidia vp magamba chadema imeshabeba nchi.
 
huyu mzee bana ananifurahishaga sana...atakanusha tu hii kauli nyie subirini muone
 
JF
kama Tendwa atashikilia uzi wake huu kuwa chama kisicho kuwa na wabunge & madiwani kishushwe daraja baada ya uchaguzi. kwa sasa ni vyama gani vingeshuka daraja ?????
 
Kwa wapenda demockrasia hili ni suala ambalo liko wazi ndiyo maana waanzisha vyama. Hata vile vyama ambavyo havijapata uwakilishi hata wa udiwani au ubunge bado vinaamini siku moja vitaongoza nchi.

Kukaa na kuamini kuwa magamba hawatakaa wakatolewa madarakni ni siasa za njozi na ni kinyume na demockrasia. Lakini cha ziadi dalili za mabadiliko ya utawala zinaonekana wazi hata kama siyo leo kesho inawezekana. Tufunguke na tukubali mabadiliko katika fikra zetu.

Tatizo kubwa kwa Tanzania watu wengine hawana pa kukimbilia pindi chama fulani kitakapoondolewa madarakani kwa kuwa akili na maisha yao wameweka kwenye siasa za chama kimoja, mfumo ambao umepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom