Tendwa sasa atishia kukifuta CHADEMA

Tendwa amekosa jambo la kuwaambia watanzania. Anaona kuisema CCM ni chama chake, atapoteza ajira na mafao yote. Anaamua kuisema CDM ambayo haina nguvu ya Dola lakini ina nguvu ya umma. I tell u, ajaribu aone nguvu ya umma itakavyovamia Ofisi zake na kumtoa kafara yeye kabla hata wabunge wa CDM hawajatoka nje kupisha shughuli za Bunge kwa kukosa uhalali wa kisheria kwa kushiriki Bungeni kwakuwa hawatakuwa wabunge tena!
 
We Tendwa jaribu uone kama nchi itakalika badala ya kulaani policcm we unaimaind cdm au ndio umetumwa kama wenzio policcm
 
Ajaribu kufuta kama anaweza na sio porojo tu,ukilaza wake atajuta kuzaliwa,na by the time akifanya hivyo kuanzia mama yake mpaka babu yake awapeleke nje ya nchi.....viongozi wasiojuwa nini wanakifanya eti simple tu nitafuta chama stupid...

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Mnafiki hajifichi! Huyu babu kada wa CCM ameshindwa kusimamia majukumu yake pale Ofisi ya Msajili wa Vyama kwa kushindwa kukemea vitendo vya kihuni na kijinga wanavyofanya Watawala,sasa eti anatishia nyau kuifuta CDM!
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyajati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.

nilidhani angesema atalifutilia mbali jeshi la polisi kwa kuua raia bila makosa
 
Mungu amewaumbua.Kilichoikoa CDM ni zile picha zilizopigwa na waandishi kuonyesha yule polisi katili alivyofumua utumbo wa mwandishi yule masikini.Kwani siku ile tayari Chagonja alishasema CDM ndiyo walirusha kitu kizito kumuua yule mwandishi,kumbe walishajipanga kupiga propaganda na tayari Tendwa alishaandaliwa kuongea ujinga kama wa leo ili kuhalalisha kufuta CDM.Mungu ni mwema waandishi wamemuumbua Tendwa na wenzie.
Mkuu Molemo vipi wale wachili wa Arumeru bado hawajamuua Lema kama walivyomuahidi huyu anayejiita Mlezi wa Vyama( Tendwa)
 
Anazidi kuhalalisha kile nilichosema ktk ule uzi wangu wa sababu 3 zilizoko nyuma ya vifo ktk mikutano ya Chadema. Vifo hivyo, vinataka kuhalalisha jambo. Kama si kuchafua chadema, basi ni kuifuta chadema. Exactly, kama alivyosema rafiki yangu. Nijuavyo na niaminivyo, hilo halitawezekana.
Pili, kwa kuwa mjadala wote sasa umeelemea polisi kwa kubebeshwa lawama zote, Tendwa anataka kubadili mjadala uwe Chadema na vifo. Watz wa leo siyo wa miaka 50. Hawatafanikiwa.

Huyu jamaa anadhani anaweza kuwatishia chadema kwa kirungu cha usajiri. Anafikiri ukubwa wa chadema ni kuhesabu wanachama kama ccm. wamwambie chadema ni chama cha watanzania wote ukitoa makada wa ccm na mafisadi na familia zao waliobaki wote ni nguvu ya umma. Anaamini katika akili ndogo kuwatawala akili kubwa! kama anajua kupima mwelekeo wa upepo angetulia tu muda wake uishe asepe maana hana ubavu wa kufuta nguvu ya umma. Nguvu ya umma haiwezi kufutwa kama chama cha siasa.

Nadhani huyu mzee bado anadanganyika kuwa anaweza kuwa fool watanzania wa leo! Anasahau kuwa watanzania wa leo wanauelewa wa mambo zaidi kuliko yeye!
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Hivi ni jukumu la vyama kutunza amani!
 
Tatizo moja hawa jamaa akili zao nahisi zimeganda,maana mipango yenyewe wanaipanga ya kitoto
mno,yaani serikali inaagiza polisi waue kila CDM wanapofanya mikutano ili waichafue CDM na wapate
sababu ya kumwambia huyu mzee asiye fikiria mara mbili kuwa aifute CDM.Listern you CCM don't waste
your time kuwaza CDM ikifutwa mtamaliza vuguvugu la mabadiliko! you are wrong,"mnaweza kufuta chama
lakini hamuwezi kufuta vuguvugu la mabadiliko kwenye fikra za watanzania".
 
Atafuta chama lakini hawezi kufuta fikra za kimapundizi zilizopo vichwani mwa watanzania...kufuta chama bila kuja na jibu la uhakika kwa matatizo ya watanzania hakutaisaidia serikali yangu chochote,nawasihi badala ya kukaa chini na kudraft plan za ni namna gani watakifuta chama chochote cha siasa nchini,watumie mda huo na nguvu hizo kujiuliza ni kwa nini wamepoteza mvuto kiasi hicho,pia wakumbuke bila kuja na majibu ya msingi ya matatizo ya nchi hii hata wakifuta vyama vyote vya siasa hakutawasaidia kwani kila unapombana binadamu naye ndivo hivyo hivyo anavyotafuta means nyingine yakusurvive na hiyo ndio hatari zaidi...PIA MABADILIKO HAYAZUILIKI KAMWE.
 
TENDWA futa vyama vyote ibakishe CCM.... ila mwisho wa siku tutapigia kura hata mawe lakini sio CCM.. Shame on you
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.

Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyajati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.

Source:Habari Radio Tumaini.

Nadhani atakuwa anamaanisha kukifuta Chama Cha Mapolisi (CCM) ingawa kimeanza siasa pasipo kuwa na usajili. Kinyume cha hapo yeye mwenyewe ataonekana bw*ge na si watanzania tena.
 
Back
Top Bottom