Tendwa na Wapinzani!

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
42
Wapinzani `wamechacha` -Tendwa
2009-01-04 12:49:22
Na Simon Mhina
Msajili wa vyama vya siasa, John Tendwa, amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani `wamechacha` hudiriki kumuomba nauli ya daladala ili waweze kurudi majumbani mwao.

Tendwa alitoa madai hayo alipozungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya mapato na matumizi ya vyama vya siasa nchini.

Alisema vyama vingi vya siasa vimejitahidi kuleta mahesabu ofisini kwake baada ya kukaguliwa, japokuwa kuna matatizo ya hapa na pale.

Hata hivyo, alisema vyama ambavyo havipati ruzuku ya serikali amevisamehe japokuwa navyo pia sheria inavitaka kukaguliwa na kuwasilisha taarifa ya mapato na matumizi ofisini kwake.

Alipoulizwa ni kwa vipi wao wamesamehewa, msajili huyo alijibu ``Mambo mengine ni kujisumbua tu na kutafuta lawama zisizo na faida, hebu fikiri, kuna wenyeviti wa vyama na makatibu wao wanakuja hapa ofisini, halafu wananiomba nauli, wanasema hawana senti ya kupandia daladala, sasa watu kama hao unawadai mahesabu yepi?``.

Alipoulizwa viongozi hao wakishamuomba nauli hufanyaje, Tendwa alisema hulazimika kuchomoa pochi yake na kuwakatia kitu kidogo.

``Kwa kweli kama kuchacha, kuna viongozi wa vyama vya upinzani wamechacha kwelikweli hadi wananuka, lakini mimi nitafanyaje kwa vile na mimi ni binadamu

SOURCE: Nipashe
 
Tuma Maoni Yako
 
Unapokuwa unaburuzika

Juzi Ijumamosi nilikiona kipindi ambacho Generali Ulimwengu akikiendesha kwenye TBC akiwa Tendwa yupo nilimstajabu mtu kama yeye akiwa anaitwa msomi kwakuwa tu yumo kwenye System anajisahau na anajikuta anazungumza kama wanasiasa waliofilisika.

Anasema "America imewachukua miaka 100 ndio kufika kwenye Democracy walionayo ikiwa ina mapuingufu, verejee leo sisi tulioanza juzi tuwe sawa na wao na wengine"? Haya mie nayaita maneno ya Kibahalula, kwani mbona Internet na mengi tumeyavaa ikiwa ya juzi tu iweje yaliomema tuyawache tuwe tuyaendea kwa mwendo wa Jongoo?
Tendwa lazima ajuwe Africa tunaiweka vibaya kwa hizi chaguzi na kuwa na watu wa Sampuli yake. Africa kila kukicha watu wanakwenda kwenye Uchaguzi vyma vya upinzani vinashindwa kwa hila kisha vinatakiwa na kina Tendwa na Mabwana zao waliowapa ajira watu waufyate wasiseme Kwinii! Wapinzani kama Ghana wasingeonyesha mapema kuwa hawatakubali basi wangeshindwa.

Sote tunajua ya Mugabe mazuri aliyoyafanya, lakini kwasasa ni mavi matupu lakini watu kama Tendwa utakuta wanaunga mkono na watu wanaatilika. Unafikiri ya Congo DRC chanzo chake ni nini? Hapana shaka kina Tendwa. Mie naona wizi wa kura na mizengwe ya kura jina munasaba ni Tendwasim
. Mijinga sio ile ambayo haijasoma Mijinga na Mipumbavu ni wale wasomi wanaoitikia Hewallah Bwana na kushindwa kupambanua ukweli, hawa Ayatullah Khomeni alipoingia madarakani baada ya kumuangusha Shah wa Iran aliwatwanga risasi.

Tendwa wizi wakina EPA, Richmond ulioiweka taifa pabaya umekaa Kwii, na umeufyata. Leo uanategemea nini kwenye Tanzania ya vibaka kukosekana ombaomba? Vimwana vingapi asubuhi wapo maofisini usiku wapo kama Changu Doa? Sababu maisha hayakamatiki, lakini kina Tendwa wapatao utamu mijinga leo kukurupuka watu wanaomba nauli ya daladala. Tendwa soma alama za nyakati.
 
Kulewa madaraka si jambo dogo unaweza hata kuchizika ukadhani hutayaacha .
 
Ati wananuka! vikwapa au pafumu. ukisikia kulewa madaraka ndio huku!
 
Alipoulizwa viongozi hao wakishamuomba nauli hufanyaje, Tendwa alisema hulazimika kuchomoa pochi yake na kuwakatia kitu kidogo.

``Kwa kweli kama kuchacha, kuna viongozi wa vyama vya upinzani wamechacha kwelikweli hadi wananuka, lakini mimi nitafanyaje kwa vile na mimi ni binadamu

- Huyu Tendwa, nilifikiri ni kichwa kumbe ni wale wale vichwa vya panzi kina Makamba, damn it!
 
Back
Top Bottom